Kipande cha nyama ya nguruwe kwa siku 'chaweza kusababisha saratani '

Nyama ya nguruwe iliyokaushwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata kiwango kidogo cha nyama nyekundu na nyama iliyosindikwa - kama vile kipande cha nyama ya nguruwe iliyokaushwa kwa siku -inaweza kuongeza hatari ya saratani ya utumbo , kwa mujibu wa utafiti.

Utafiti wa hivi karibuni wa Chuo kikuu cha Oxford uliodhaminiwa na taasisi ya utafiti wa saratani nchini Uingereza, unaongezea ushahidi kuthibitisha hayo, ukiwemo ule uliotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ,kwamba ulaji wa nyama nyekundu unaweza kuwa na madhara.

Lakini athari ni kubwa kwa kiasi gani? na ni kipi kiwango ni cha ulaji wa nyama ni cha juu?.

Haya ndio unayopaswa kujua:

Kile utafiti ulichobaini:

Watafiti walitatathmini data kutoka kwa watu wapatao nusu milioniwaliohusika katika utafiti uliofanywa na kituo cha Uingereza cha utafiti wa kibaiolojia -UK Biobank

Kwa zaidi ya miaka sita ya uchunguzi wao walibaini kuwa watu 2,609 walipata saratani ya utumbo.

Walikadiria:

  • ulaji wa vipande vitatu vidogo vya nyama ya nguruwe kila siku badala ya kula mara moja tu unaweza kusababisha kuongezeka kwa hatari ya saratani ya utumbo kwa asilimia 20%
  • Kwa kila watu 10,000 katika uchunguzi huo walikula gramu 21 za nyama nyekundu na nyama za kusindikwa, 40 kati yao walipatikana na saratani ya utumbo.
  • Idadi iliyolinganishwa kwa wale waliokula gramu 76 kwa siku , ilikuwa ni watu 48.

Ni kiwango gani cha ulaji wa nyama ni kikubwa kupita kiasi

Haijawa wazi. Taasisi ya utafiti wa saratani nchini Uingereza -Cancer Research UK (CRUK) inasema visa 5,400 kati ya visa 41,804 vya saratani ya utumbo vinavyopatikana nchini Uingereza vinaweza kuzuwiwa kama watu hawali nyama za kusindikwa kabisa.

Kwa mujibu wa Emma Shields, Meneja wa habari katika CRUK, "Utafiri huu unaonyesha kadri unavyozidi kula nyama, ndivyo, hatari ya kupata inavyoongezekana usipokula nyama zaidi matokeo yanakuwa kinyume - kadri unavyokula nyama kwa kiasi kidogo ndivyo unavyopunguza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo,"

Lakini alikiri kuwa uvutaji wa sigara husababisha hatari kubwa zaidi, ukisababisha visa 54,300 vya saratani kila mwaka.

Taasisi ya Uingereza ya afya ya umma inasema kuwa kutokana na utafiri wake watu wengi hula nyama nyekundu kupita kiasi pamoja na nyama za kusindikwa.

Na ushauri wa wataalamu unasema watu wanaokula kiwango kikubwa cha nyama watafute njia za kupunguza kiwango cha nyama.

Wizara ya afya inamshauri yeyote anayekula nyama zaidi ya gramu 90 nyekundu kwa siku na nyama za kusindikwa kupunguza na kula gramu 70.

Ni SAWA kula nyama kidogo ?

Muongozo wa taasisi ya NHS unasema kuna baadhi ya faida za nyama nyekundu - zina madini ya mwili, chuma na protini kwa mfano - ambayo yanapaswa kuepusha hatari zinazoweza kujitokeza.

Watu wanaweza kula nyama na bado wakawa wenye afya.

Ni nini kinachosababisha hatari?

Nyama za kusindikwa -zikiwemo za nguruwe, baadhi ya soseji, hot dog na salami -hubadilishwa kwa kiasi kwamba zinaweza kukaa kwa mudamrefu au kubadilisha ladha - njia kuu ni kuzichoma, kuzitibu au kuziongezea chumvi au kuziwekea kemikali za kuzuwia zisioze.

Pia ni kemikali zinazohusika katika usindikaji zinaweza kuongeza hatari ya saratani. Viwango vya juu vya joto vinavyotumia katika kupika, kama vile wakati wa kuzichoma, pia vinaweza kustengeneza kemikali hatari za carcinogenic kwenye nyama.

Inapokuja katika suala la nyama nyekundu kama vile nyama ya ng'ombe, kondoo na nguruwe, kuna madai kuwa moja ya protini inayosabisha nyama hizo kuwa nyekundu inaweza kuharibu utumbo.

Lakini wataalamu bado wanaendelea kujaribu kuelewa zaidi madai hayo.

Wataalamu wanasema nini?

Profesa Gunter Kuhnle, katika Chuo kikuu cha Reading, walielezea utafiti huo kama wenye tathmini ya uhakika wa uhusiano baina ya ulaji wa nyama na saratani ya utumbo.

Alisema : "Matokeo yanathibitisha matokeo ya utafiti wa awali kwamba ulaji wa nyama nyekundu na nyama za kusindikwa kwa pamoja huongeza hatari ya saratani ya utumbo.

" Huongeza hatari ya takribani 20% kwa gramu 50 ya nyama nyekundu na nyama za kusindikwa sawa na matokeo ya tafiti za awali ambazo zilithibitisha haya.

Carrie Ruxton, kutoka jopo la washauri wa ulaji wa nyama anasema : "Nyama nyekundu hutoa virutubisho vya thamani, kama vile protini, madini ya chuma, zinc, vitamini D na B."

Alisema inafahamika kwamba kuna "mtindo mbali mbali wa maisha huchangia kusababisha hatari za saratani ya utumbo , ikiwemo umri, geni na kutofanya mazoezi ya mwili na unywaji wa pombe kupindukia wa kupindukia ".

Utafiti huu ulichapishwa na International Journal of Epidemiology.