Mji wa Bugarama ''kitovu cha ukahaba'' Rwanda

Mitaa ya mji wa Bugarama uliopo katika kati ya nchi tatu: Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Burundi
Maelezo ya picha,

Mitaa ya mji wa Bugarama uliopo katika kati ya nchi tatu: Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Burundi

Mji wa Bugarama kusini magharibi mwa Rwanda uliopo kwenye mpaka wa nchi tatu Rwanda,Burundi na DRC umekuwa kitovu cha ukahaba.

Makahaba katika mji wa Bugarama wanasema ukahaba siyo kazi tena kama ilivyokuwa zamani kutokana na kuwa wanawake wengi sasa wanajiingiza katika shughuli hiyo ambayo imekuwa ni njia rahisi ya kujipatia kipato.

Katika ukumbi wa burudani mjini Bugarama makahaba hufurika kwa wingi wakisubiria wateja wao pembezoni mwa lango kuu, anasema mwandishi wa BBC nchini Rwanda Yves Bucana.

'' Ukahaba nilianza nikiwa na miaka 14 , hivi naeneza miaka 25, toka miaka 14 hesabu sijui nimelala na wanaume wangapi na bado ningali nawapata. Nimelala na wanaume wengi sana, inatoikana na jinsi wanavyopatikana kwa usiku mmoja kama wakipatikana hata 10 unaweza kulala nao. Wakikosekana utapata wawili watatu, inatokana na wakati wa pesa, kama kuna pesa unapata wanaume wa kutosha.'' alisema kahaba mmoja.

Maelezo ya picha,

Wanaume Kutoka DRC wanaaminika kwa kutoa malipo mazuri kwa makahaba wa Bugarama zaidi ya wanaume kutoka nchi nyingine

''Siwezi kuwahesabu nijue ni wangapi, ni wengi, usiku unaweza kupata wanaume hadi watano. Tunapata wanaume wanyarwanda, wakongo na wachina''. Alisema kahaba mwingine huku akitabasamu.

Upande wa malipo wanasema wateja wao nambari moja ni wanaume kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambao wanaaminika kumheshimu zaidi mwanamke: '' Wakenya anaweza hata kukupa dola 50, Wakongo ndio wanalipa vizuri na hakuna tatizo , na hataleta kelele, ukiamka asubuhi atakulipa pesa yako, jinsi mlivyoelewana, Wakongo wanaheshimu sana wanawake, Wakongo ndio wanalipa vizuri wanalipa kwa dola, Wakongomani wanawathamini wanawake.'', Alisisitiza kahaba huku akitazama huku na kule kuangalia ikiwa anaweza kumpata mteja.

BBC ilibaini kuwa wateja wengi wa makahaba nchini Rwanda hivi karibuni hutembea na mashine za kujipima wenyewe ugonjwa wa ukimwina ujauzito.

Maelezo ya picha,

Ukahaba haukubaliki na ni kosa la jinai Rwanda

Hata hivyo bei ya kutumia mipira ya kondomu na kutoitumia hutofautiana wanasema makahaba, Bei ya kutumia kondomu ni dola ishirini na bei ya kutovaa kondomu ni dola hamsini, wanasema.

''Leo wikendi kuko show yaani napata raha yaani napataga wa teja wa kujiheshimia Alhamdulillah,wazee, mabwana wa kujiheshimia, ukiona bwana unasema Alhamdulillah yaani kesho sitakuwa na njaa.''Anasema mwanamke huyu ambaye alikuwa akipokea simu za wateja wakati wa mahojiano.

Ukahaba haukubaliki na ni kosa la jinai Rwanda. Makahaba wanasema kazi yao kwa sasa haina tija ikilinganishwa na zamani kwa sababu siku hivi karibuni idadi ya makahaba wanaoingia Bugarama kutoka nchi maeneo mbali mbali ya Rwanda na mataifa jirani imeongeza.