Polisi wa New York wamemkamata mtu aliyekua na mafuta ya petroli katika Kanisa la Mtakatifu Patrick

Kanisa la Mtakatifu Patrick Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Kanisa la Mtakatifu Patrick lilijengwa karne ya 19

Mwanaume mmoja amekamatwa baada ya kuingia kwenye kanisa la Mtakatifu Patrick jijini New York akiwa amebeba makopo mawili ya Petroli, kibiriti , Polisi anaeleza.

Walinzi walimkabili mtu huyo mwenye miaka 37 alipokua akiingia kanisa la Manhattan siku ya Jumatano jioni.

Aliyamwaga mafuta chini kisha maafisa wakamkamata kumpeleka korokoroni.

Kadinali katika Kanisa katoliki hatiani kwa unyanyasaji wa kingono

Kasisi aingia matatani baada ya mkewe kushiriki ‘Umiss’

Naibu kamishna wa polisi John Miller amesema tukio hilo linaloshukiwa kuwa baya lilitokea siku mbili baada ya kanisa la Notre-Dame jijini Paris.

''Mtu alikua akitembea usawa wa kanisa amebeba magaloni ya mafuta, na vibiriti, ni jambo la kushukiwa''.Alisema Bwana Miller

Afisa wa intelijensia na masuala ya ugaidi amesema ni 'mapema sana' kueleza kama kusudio la mtu huyo ni kutekeleza vitendo vya kigaidi

Alipokabiliwa nje ya Kanisa, Mwanaume huyo aliwaambia maafisa kuwa gari yake iliishiwa mafuta na alikua akipita mbele ya kanisa hilo ili kulifikia.Alikamatwa na polisi walitazama gari lake na kuona kuwa halikua limeishiwa mafuta.

Haijulikani mtu huyo alikua na mipango gani.