Nusrat Jahan Rafi: Achomwa hadi kufa kwa kuripoti unyanyasaji wa kingono

Picha ya Nusrat Jahan Rafi

Chanzo cha picha, Picha ya familia

Nusrat Jahan Rafi alimwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto shuleni kwake katika mji wa Bangladesh. yapata wiki mbili kabla, alikuwa amewasilisha malalamiko ya unyanyasaji wa kingonoi dhidi ya mkuu wake wa shule..

Ushupavu wake wa kuzungumzia wazi unyanyasaji wa kingono, kifo chake siku tano baada ya kuchomwa moto na mambo yote yaliyotokea vimeibua hisia tofauti miongoni mwa raia wa Bangladesh na kuonyesha namna waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono wanavyokabiliwa na hatari katika taifa hilo lenye itikadi kali lililopo kusini mwa bara la Asia.

Nusrat, ambae alikuwa na umri w amiaka 19, alikuwa anatoka katika mji mdoto wa Feni, uliopo maili 100 kutoka mji mkuu Dhaka. Alikuwa anasoma katika shule ya Kiislamu ya madrassa, tarehe na 7 Machi alisema kuwa Mkuu wa shule alimuita ofisini kwake na kumtomasa. Kabla mambo hayafika mbali alikimbia nje ya ofisi.

Wasichana wengi na wanawake wenye umri mdogo nchini Bangladesh huamua kunyamaza kimya wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono au kubakwa kwa kuhofia kudhalilisha na jamii au familia zao . Kilichomfanywa tofauti na Nusrat Jahan ni kwamba hakuzungumzia suala hilo kwa sauti tu bali - alikwenda pia kwa polisi kwa msaada wa familia yake katika siku ambayo unyanyasaji huo ulidaiwa kufanyika.

Katika kituo cha polisi mjini humo alieleza mashtaka. Alitakiwa kupewa mazingira salama ili aweze kuthathmini yaliyomtokea. Badala yake alichukuliwa video na afisa wa polisi husika kupitia simu yake huku akielezea yaliyompata.

Katika video hiyo Nusrat anaonekana wazi akiwa na mkanganyiko huku akijaribu kuficha uso wake kwa mikono. Polisi anasikika akisema malalamiko hayo "sio jambo kubwa " na kumueleza nusrat aondoe mikono usoni . Baadaye video hiyo ilivifikia vyombo vya habari nchini humo.

'Nilijaribu kumpeleka shuleni'

Chanzo cha picha, NurPhoto/Getty Images

Maelezo ya picha,

Maandamano yamekuwa yakifanyika mjini Dhaka na katika mji wa Feni - alikoishi Nusrat

Nusrat Jahan Rafi alikuwa anatoka katika mji mdogo, na alizaliwa katika familia yenye ya kihafidhina, na akasomea katika shule ya dini. Kwa msichana kama yeye, kuripoti unyanyasaji wa kingono ni jambo linalokuja na madhara . mara nyingi waathiriwa hukabiliw ana hukumu kutoka kwa jamii zao, udhalilishwaji wa moja kwa moja na kupijtia mtandao , na wakati mwingine hupigwa. Nusrat alikabiliwa na yote haya.

Tarehe 27 Machi, baada ya kwenda polisi, walimkamata mwalimu wake mkuu. Baada ya hapo mambo yakaanza kuwa mabaya kwa Nusrat. Kundi la watu walikusanyika kwenye mitaawakidai aachiliwe. Waandamanaji walikuwa wamekusanywa na wanafunzi wawili wa kiume na wanasiasa wa eneo hilo wanaripotiwa kuwa walihudhuria maandamano hayo . Watu walianza kumlaumu Nusrat. familia yake inasema ilianza kuhofia usalama wake.

Licha ya hayo , tarehe 6 Aprili, siku 11 baada ya unyanyasaji huo unaodaiwa, Nusrat alikwenda shuleni kwake kufanya mitihani yake ya mwisho.

"Nilijaribu kumchukua dada yangu shuleni na kujaribu kuingia shuleni, lakini nikazuwiwana sikuruhusiwa kuingia ," alisema kaka yake Nusrat , Mahmudul Hasan Noman.

"Nisingezuwiwa, jambo kama hili lisingemtokea dada yangu ," alisema.

Chanzo cha picha, Shahadat Hossain

Maelezo ya picha,

kaka yake Nusrat Jahan akiomboleza wakati wa mazishi

Kwa mujibu wa taarifa ya mashtaka iliyotolewa na Nusrat, mwanafunzi mwenzake wa kike alimpeleka kwenye paa la shule, alisema mmoja wa marafiki zakealikuwa amechapowa . Wakati Nusrat alipofika juu ya paa watu wanne au watano, waliokuwa wamevalia burqa, walimzingira na kumshinikiza aachane na kesi dhidi ya mwalimu mkuu. Alipokataa ndipo walipomwagia mafuta ya taa na kumchoma kwa moto.

Mkuu wa Idara ya upelelezi ya polisi Banaj Kumar Majumder alisema kuwa wauaji wanaotafutwa "walitaka kufanya mauaji hayo yaonekane kama Nusrat alijiua mwenyewe ". mpango wao uliharibika wakati Nusrat alipookolewa baada baada ya kutoroka eneo la tukio. Aliweza kutoa taarifa kabla ya kufa.

" Mmoja wa wauaji wake alishindilia kichwa chake chinikwa kutumia mikono yake, kwa hiyo mafuta ya taa hayakumwagika palena ndio maana kichwa chake hakikuungua ," Bwana Majumder aliiambia BBC mjini Bengali.

Lakini wakati Nusrat alipopelekwa katika hospitali iliyopo karibu majeraha mwili wake ulikuwa na 80% ya majeraha ya mwili wake . Hawakuweza kutibu vidonda , na kuamua kutuma katika hosptali ya chuo cha tiba cha Dhaka.

Alipokuwa katika ambilansi, kwa kuhofia kuwa hatapona, alirekodi taarifa katika simu ya mkononi ya kaka yake.

"Mwalimu alinitomasa, Nitapigana vita hivi mpaka pumzi yangu ya mwisho ,"alisikika wazi akisema.

Pia aliwatambua baadhi ya waliomshambulia aliosema ni wanafunzi wa madrasa

Taarifa ya afya ya Nusrat imetawala katika vyombo vya habari vya Bangladeshi . Tarehe 10 Aprili, vilisema. maelfu ya watu walijitokeza kuhudhuria mazishi mjini Feni.

Polisi wamewakamata watu 15, saba miongoni mwao wanadaiwa kuhusika na mauaji . Miongoni mwa wale waliokamatwa ni wanafunzi wawili wa kiume walioandaa maandamano ya kumuunga mkono mwalimu mkuu. Mwalimu mkuu mwenye amesalia mahabusu .Polisi aliyechukua video ya Nusrat alipokuwa akitoa alalamiko ya unyanyasaji wa kingono ameondolewa kwenye cheo chake na kuhamishiwa katika idara nyingine.

Waziri Mkuu Sheikh Hasina alikutana na familia ya Nusrat mjini Dhaka na kuahidi kuwa kila mtu aliyehusika katika mauaji yake atafikishwa mbele ya sheria . "hakuna yeyote kati ya waliohusika atakayekwepa hatua za sheria ," alisema.

Chanzo cha picha, Shahadat Hossain

Maelezo ya picha,

Umati mkubwa wa watu ulikusanyika katika mji alikozaliwa Nusrat wa Fenkuhudhuria mazishi yake

Kifo cha Nusrat kimeibua maandamano makubwa na maelfu ya watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuelezea hasira yao juu ya kisa hicho na na namna waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono wanavyoshughulikiwa nchini Bangladesh.

" Wasichana wengi hawapingi kutokana na uoga baada ya matukio ya aina hiyo . Burqa , wala nguo za chuma haziwezi kuwazuwia wabakaji ," alisema Anowar Sheikh kupitia ukurasa wa Face book wa BBC idhaa ya Bengali.

"Nilitaka kuwa na msichana maisha yangu yote, lakini sasa ninaogopa. Kujifungua mtoto katika nchi hii ina maanisha utaishi maisha ya hofu na wasi wasi ," aliandika Lopa Hossain ikatika ujumbe wake wa Facebook.

Kwa mujibu makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Bangladesh Mahila Parishad, kulikuwa na matukio 940 ya ubakaji nchini Bangladesh mwkaa 2018. Lakini watafiti wanasema idadi halisi huenda ikawa ni ya juu zaidi.

"Wakati mwanamke anapojaribu kupata haki kwa unyanyasaji wa kingono, anakabiliwa na unyanyasaji tena. Kesi inakaa kwa miaka minne, kuna aibu katika jamii , ukosefu wa utashi kutoka kwa polisi wa kupeleleza ipasavyo madai ," alisema Salma Ali, wakili wa masuala ya haki za binadamu na mkurugenzi wa zamani wa chama cha mawakili wanawake.

"hii inawafanya waathoiriwa kuamua kuacha kudai haki ya kisheria. Hatimae wahalifu hawaadhibiwi kwa hiyo wanafanya uhalifu tena. Wengine hawaogopi hawaogopi kufanya uhalifu sawa na huo kutokana na mifano ya aina hiyo "

Sasa watu wanauliza: Ni kwanini kesi ya Nusrat inazungumziwa baada ya kushambuliwa? Na kesi yake itabadilisha mtazamo wa watu juu ya unyanyasaji wa kingono nchini Bangladesh?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Familia ya Nusrat imeachwa katika huzuni

Mnamo mwaka 2009, Mahakama ya ngazi ya juu ilipitisha amri ya kuanzishwa kwa vitengo akatika taasisi za shule ambako wanafunzi wanaweza kuwasilisha malalamiko yaoya unyanyasaji wa kingono ,lakini ni shule chache ambazo zimeweza kuanzisha vitengo hivyo . Wanaharakati sasa wanataka amri hiyo itekelezwena sheria ya kuwalinda wanafunzi iwekwe.

"Tukio hili limetutikisa, lakini kama tulivyoshuhudia miaka ya nyuma, matukio kama haya huwa yanasahaulika baada ya muda. Sidhani kutakuwa na mabadiliko makubwa baada ya tukio hili. Lazima tuone haki inatendekeka," alisema Profesa Kaberi Gayen wa Chuo kikuu cha Dhaka.

"Lazima mabadiliko yaje, kisaikolojia na katika utekelezaji wa sheria . Lazima kuwe na uelewa juu ya unyanyasaji wa kingonokuanzia mtu anapokuwa mtoto shuleni," alisema

"Lazima wajifunze ni kipi sahihi na kipi si sahihi inapokuja katika suala la unyanyasaji wa kingono."