Machafuko Mali : Waziri Mkuu na mawaziri wake waachia ngazi

Wanawake wakiwa kwenye maandamano tarehe 5 mwezi Aprili nchini Mali

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Maandamano yalifanyika mwezi huu dhidi ya serikali ya Mali

Waziri Mkuu wa Mali na Serikali yake yote wamejiuzulu, baada ya kutokea machafuko nchini humo.

Siku ya Jumatano, Wabunge walipiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wakimshutumu waziri huyo, Soumeylou Boubeye Maiga kwa kushindwa kudhibiti matukio hayo.

Mwezi uliopita, wafugaji waliuawa na mahasimu wao.

Rais Ibrahim Boubacar Keita amesema kwenye taarifa yake kuwa amekubali Bwana Maiga na baraza lake kujiuzulu.

''Muda mfupi ujao atateuliwa Waziri Mkuu mwingine na serikali nyingine itawekwa uongozini baada ya majadiliano,'' Taarifa imeeleza.

Mali imekua ikipambana kudhibiti machafuko tangu wanamgambo wa kiislamu wenye uhusiano na al-Qaeda walipoingia kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2012.

Pamoja na kuwepo kwa makubaliano ya amani ya mwaka 2015, wanamgambo bado wanadhibiti maeneo makubwa ya nchi, wakitokea Kaskazini na kuingia kwenye maeneo ambayo yana watu wengi zaidi.

Serikali imekuwa kwenye shinikizo kubwa ikishutumiwa kutokuwa na uwezo wa kurudisha hali ya utulivu, hasa baada ya mauaji ya wafugaji 160 wa kabila la Fulani katika Mji wa Mopti.

Wakiwa wa silaha na mapanga, washambuliaji walibainika kuwa wa jamii ya Dogon, ambao wana historia ndefu ya kuwa na mgogoro na jamii ya Fulani.

Nchi hiyo ilishtushwa sana na mauaji hayo na maelfu ya watu waliandamana mitaani mjini Bamako tarehe 5 mwezi Aprili.

Akizungumza kwa njia ya televisheni alisema ''amesikia hasira yao''.

Maelezo ya picha,

Ramani inayoonyesha nchi ya Mali na mji wa Mopti ambako mauaji