Picha kutoka barani Afrika : 12-18 April 2019

Picha bora zilizochaguliwa kutoka barani Afrika Juma hili:

Kasisi akiwa kanisani siku ya Jumapili tarehe 14 mwezi Aprili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kasisi akifukiza ubani siku ya Jumapili misa ya mitende katika Kanisa Katoliki la Lady of Grace nchini Msumbiji

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanamke jamii ya Samburu akiwa amebeba bango wakati wa kampeni ya kidunia dhidi ya mauaji ya Tembo, Faru, Simba na wanyama wengine walio hatarini siku ya Jumamosi Nairobi , Kenya.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Msichana akipatiwa msaada na daktari wakati akijifunza kutembea na mguu wa bandia nchini Sudani Kusini siku ya Ijumaa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wavulana wakicheza mpira kwenye viwanja vya shule nchini Msumbiji Jumatatu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Msichana akiwa ametapakaa poda ya manjano wakati wa sherehe ya rangi nchini Misri siku ya Jumamosi.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Msanii wa uchoraji Bankslave wa Kenya akimaliza mchoro wake wa graffiti mjini Dakar,Senegal.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Maafisa polisi wakidhibiti kundi la watu uwanja wa ndege walipofika kumlaki Rais Tshisekedi alipokua akiwasili uwanja wa ndege wa Goma nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo siku ya Jumapili.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Wiki ya maonyesho ya mavazi Cape Town, mwanamitindo akiwa amevaa vazi la kitamaduni.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Huku mwenzie akiwa amevalia kofia nzuri siku ya Jumamosi.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Wanaume wakiwa tayari kuanza mchezo wa mieleka jijini Lagos Nigeria

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mpiganaji kutoka Jeshi la taifa la Libya akipasua matofali wakati wa sherehe za kuhitimu mafunzo mjini Benghazi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nchini Sudan, Wanawake wamekua katika Kampeni ya kutaka kufutwa kwa serikali ya mpito ya baraza la kijeshi lililomuondoa Omar al-Bashir juma lililopita.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanawake hawa wameunga mkono wito wa kuwepo kwa serikali ya kiraia nchini Sudan.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mtoto wa Rais wa Marekani Donald Trump, Ivanka awatembelea wajasiriamali nchini Ivory Coast siku ya Jumatano ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne barani Afrika.