Wasichana wawili wamekamatwa kwa kupanga ''mauaji tisa' mjini Florida

Classroom stock photo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

darasa nchini Marekani (picha ya maktaba)

Wasichana wawili wamekamatwa katika jimbo la marekani kwa madai ya kupanga mauaji ya watu tisa. Vimeripoti vyombo vya habari vya Marekani.

Wawili hao kutoka shule ya sekondari ya Avon Park Middle, wakiwa na umri wa miaka 14 wote. Walitiwa nguvuni Jumatano baada ya mwalimu wao kugundua kurasa za kompyutra ambapo inadaiwa kuwa walikuwa wameainisha mipango yao.

Katika kurasa nane, wasichana hao wanadaiwa kuandika mipango yao ya kupata bunduki na namna watakavyoihamisha miili ya watu waliowauwa na kuitupa.

Wote wawili wanashikiliwa katika mahabusu , huku wakisubili kuanza kwa kesi dhidi yao.

Kila mshukiwa analabiliwa na mashtaka ya kushiriki katika mauaji na makaso mengine matatu ya kuhusika na mauaji ya utekaji nyara.

Mwalimu wao anaripotiwa kuwa aligundua kuwa wasihana hao walikuwa wakifanya ''mambo ya ajabu" ndipo alipoangalia kwenye kurasa zao, na anadaiwa kumsikia mmoja wao akisema "nitawaambia tu kwamba ni mzaha ikiwa watatugundua ".

Baadae mwalimu aligundua faili za kompyuta ambalo zilizokuwa zimepewa jina "taarifa za kibinafsi ", "usifungue" na "Mradi 11/9".

Ndani ya maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwa mkono kulikuwa na orodha ya majina na mipango iliyoainishwa juu ya namna ya kufanya mauaji ,kw amujibu wa shirika la utangazaji habari NBC.

Nyaraka hizo zilielezea namna ya kupata silaha na kuharibu ushahidi kw akuunguza na kuzika miili ya watu waliowauwa.

Kulikuwa na walaka mwingine ambao pia ulikuwa na maelezo ya ni nguo za aina gani wasichana hao wangezifaa ili kutekeleza mauaji hayo.

"HAKUNA KUCHA NDEFU ," ulieleza waraka huo.

"HAKUNA kuonyesha nywele mara baada ya kuvaa nguo zetu".

Haijalishi ikiwa kweli ulikuwa ni mzaha, anasema Scott Dressel, msemaji wa kituo cha polisi cha Highlands, alinukuliwa akikiambia kituo cha habari cha marekani Fox47

"Hakuna utani juu ya kitu kama hiki. Hauweze kuwa na mzaha juu ya kuwauwa watu ."