Kwa Picha : Uvaaji wa vazi la kipekee kusherehekea magimbi makubwa Nigeria

Wakishiriki Wanaume katika mitaa ya Arondizuogu wakati wa tamasha lijulikanalo kama Ikeji nchini Nigeria

Imekuwa ni moja ya sherehe kubwa wiki hii katika mji wa Arondizuogu kusini mwa Nigeria, huku watu wakila na kufanya matembezi kwa ajili ya kushukuru kwa mavuno ya msimu uliopita na kuingia katika msimu wa upanzi.

Tamasha la Ikeji Festival, linalodumu kwa siku saba, huwaleta pamoja maelfu ya watu wa kabila la Igbo kutoka maeneo ya mbali na karibu katika mji wa jimbo la Imo.

Wakati wa matamasha, baadhi ya wanaume huidhinishwa na kitamaduni wa jamii ya Igbokuvaa kama roho fulani.

Husindikizwa na mpiga kengele, anayeuelezea umati wa watu ujumbe kutoka kwa ulimwengu wa kiroho - mara nyingi huwa ni ujumbe wa baraka wa mavuno yajayo.

Watu waliovalia sanamu wakichezea umati kwenye mitaa - na kama sehemu ya utamaduni huo, kuku na mbuzi hutolewa kafala kwa ajili ya mababu kuwabembeleza waipe jamii baraka ya mavuno mkubwa.

maboksi ya chumayanayoaminiwa kubeba " uchawi" yakiwa kwenye vichwa vya wanaume wanaopita kwenye vijiji 20 vinavyounda mji wa Arondizuogu, kama njia nyingine ya kuwasiliana na ulimwengu wa kiroho...Tamasha la kutatanisha lafungiwa Urusi

Tamasha hili ni tukio la mwaka- tarehe huchaguliwa na wafalme na wazee wa kijiji. Baadhi ya miaka tamasha hili hufanyika sanjari nasherehe za Pasaka , ingawa sherehe hizi hazina uhusiano. Upakaji wa rangi kwenye mwili ni sehemu ya raha ya tamasha hili.

Baaadhi ya washiriki watamasha hujipaka rangi nyeusi ya nywele , mafuta ya mawese na mkaa kwenye miili yao palm...Thailand yaadhimisha tamasha la mwaka mpya la maji

Ni muda wa kila mtu kuvaa -licha ya kwamba kimila wanawake huwa hawashiriki katika matembezi yoyote . Hutizama pembeni na baadhi huandaa chakula maalumu kwa ajili ya washiriki wa tamasha.

Na kwa kawaida sherehe si sherehe bila chakula. Biashara hunoga huku watu wakiuza nyama na kuku kwa wageni.

Sehemu ya mila za tamasha ni pamoja na kuosha miili kama ishara ya kuosha msimu wa kilimo uliopita na kujiandaa kwa msimu ujao.

Vyakula vikuu maarufu kama magimbi na kasava , na aina mbali mbali za mboga , vitapandwa katika msimu ujao.

Mwanamume mmoja akipiwa amesimama na "okpu agoro", yake yenye rangi nyekundu, nyeusi na nyeupe pamoja na kofia ya uzi inayovaliwa na wanaume wa jamii ya Igbo kusini mashariki mwa Nigeria.

Kila kikundi cha sanamu husindikizwa na ala za muziki kama vile nyimbo na ngoma na sherehe hizo huwa zinaendela hadi usiku sana.

Picha na mwandishi wa BBC idhaa ya Igbo Chiemela Mgbeahuru