Milipuko Sri Lanka: Watu 290 wauawa, 500 wajeruhiwa baada ya makanisa na hoteli kulengwa

Chanzo cha picha, AFP
Sri lanka bado imezizima na watu wamejawa na hofu.
Sri lanka iko kwenye siku ya maombolezo kwa ajili ya watu 290 waliopoteza maisha. Mazishi ya watu wengi waliouawa kwa mashambulizi ya mabomu siku ya sikuu ya Pasaka watazikwa.
Polisi walipata vilipuzi zaidi siku ya Jumatatu na moja ya vilipuzi kililipuka hapo hapo wakati wataalamu walipokua wakijaribu kutegua bomu.
Changamoto iliyopo sasa ni kwa vyombo vya usalama kurudisha hali ya kujiamini miongoni mwa wananchi.
Baada ya mashambulizi, serikali ilitangaza hali ya dharura kuanzia usiku wa Jumatatu, hatua ambayo itawasaidia kuvipa nguvu vyombo vya ulinzi na usalama, kuwakamata na kuwahoji washukiwa bila amri ya mahakama.
Serikali ya Sri Lanka imesema kundi la kiislamu lenye msimamo mkali la Thowheed Jamaath, limehusika na mashambulizi ya mabomu. Lakini haijawekwa wazi kama kweli kundi hilo limehusika.
Chanzo cha picha, AFP
Kundi la Thowheed liko na ushirika na makundi ya waislamu wenye msimamo mkali duniani.
Sri Lanka ilikumbwa na mashambulizi ya namna hiyo, mashambulizi ya kujitoa muhanga yalikua yakitelekezwa na waasi wa Tamil Tiger wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.Lakini madhara ya liyojitokeza sasa yameshtua mno kutokana na idadi ya watu waliopoteza maisha kuwa kubwa.
Mashambulizi haya yameacha kidonda katika taifa hilo, kidonda kitakachochukua muda mrefu kupona.
Katika hatua nyingine Ubalozi wa China nchini Sri Lanka leo imewaonya raia wa China kutoingia nchini Sri Lanka siku za hivi karibuni .China ni Mwekezaji mkubwa zaidi nchini Sri Lanka.
Ubalozi umesema itakua vigumu kwake kuhakikishia usalama raia wa china kipindi hiki.
Jumapili ya Pasaka ni moja ya siku kuu muhimu sana katika kalenda ya waumini wa dini ya Kikristo.
Hakuna kundi lolote lililojihusisha na mashambulizi hayo. Lakii ni dhahiri washambuliaji walilenga siku hiyo ili kuumiza watu wengi kadri iwezekanavyo.
Kumekuwa na hofu huenda wapiganaji wa kundi la Islamic State waliorejea kutoka masariki ya kati wakawa tishio kwa usalama wa nchi hiyo.
Chanzo cha picha, Reuters
Tunafahamu nini kufikia sasa?
Watu 24 wamekamatwa kufikia sasa wakihusishwa na shambulio hilo.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumapili jioni, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ranil Wickremesinghe alizungumzia uvumi kuwa maafisa usalama walikuwa na fununu za kiintelijensia juu ya uwezekano wa kutokea mashambulo.
"Lazima yuangalie ni kwanini hatua stahiki hazikuchukuliwa ili kuzuia mashambulizi hayo. Si mimi wala mawaziri wengine ambao walitaarifiwa juu ya uwepo wa taarifa hizo za kiintelijensia awali," amesema Wickremesinghe.
"Kwa sasa kipaumbele ni kuwatia nguvuni wale waliotekeleza mashambulizi hayo," ameongeza.
Chanzo cha picha, AFP
Bomu lilipuka wakati vikosi maalum vikifanya msako katika nyumba moja karibu na mji wa Colombo
Amri ya kutotoka nje imewekwa kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za Sri Lanka (12:30-00:30 GMT).
Serikali pia ilidhibiti matumizi ya mitandao yote ya kijamii kwa muda ili kuzuia taarifa potofu kuenezwa.
Kanisa la St Sebastian mjini Negombo limeharibiwa vibaya na milipuko hiyo.
Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha paa la jengo la kanisa lililoharibiwa vibaya huku damu ikiwa imetapakaa ndani ya kanisa.
Karibu watu 67 wameripotiwa kufariki ndani ya kanisa hilo.
Chanzo cha picha, Reuters
Kanisa la St Anthony Shrine mjini Kochchikade, ni moja ya makanisa yalioshambuliwa
Ni kinanani walioathiriwa?
Wengi ya waliofariki dunia ni raia wa Sri Lanka, ambao wa walikuwa wanashiriki ibada ya Jumapili ya Pasaka.
Laikini pia kuna kuna raia kadhaa wa nchi za kigeni amabao pia wamethibitishwa kufariki aida kwenye makanisa hayo matatu ama kwenye hoteli ambazo pia zilishambuliwa.
Uraia na nambari ya wageni waliofariki kwenye mkasa huo ni kama ifuatavyo:
- Waingereza watano - wawili kati yao wana uraia wa Marekani pia.
- Raia watatu wa Denmark.
- Raia watatu wa India.
- Wahandisi wawili kutoka Uturuki, kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu.
- Mholanzi mmoja.
- Mjapani mmoja.
- Mreno mmoja.
Chanzo cha picha, Reuters
Chanzo cha picha, AFP
Dini ndani ya Sri Lanka
Sri Lanka ina idadi ya wakristo karibu milioni 1.5 ambayo karibu 7% ya watu nchini humo kwa mujibu wa sensa ya mwa 2012.
Dini ya Kibudha inatajwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waumini ambao wanakadiriwa kuwa 70.2% ya watu wote nchini kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni.
Ni dini ambayo pia imepewa nafasi kubwa katika katika katiba ya nchi hiyo ikilinganishwa na dini zingine..
Wahindu na Waislamu wanakadiria 12.6% na 9.7% ya idadi ya watu nchini humo.
Chanzo cha picha, AFP
Historia ya Sri Lanka
Tangu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kukomeshwa 2009, kumeripotiwa ghasia kw amiaka kadhaa nchini Sri Lanka.
Waumini wa kibudha wamekua wakishambulia misikiti na mali inayomilikiwa na waumini wa dini ya Kiislam.
Hali ambayo ilipelekea kutangazwa kwa hali ya hatari mwezi machi mwaka 2018.
Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalimalizika baada ya wapiganaji wa kundi la Tamil Tigers kushindwa.
Kundi hilo lilipigania uhuru wa jamii ya Tamil walio wachache kwa miaka 26.
Mapigano hayo yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu kati ya 70,000 na 80,000.