Utafiti: Mamilioni ya watu hutumia namba 123456 kama neno la siri.

Jurgen Klopp and Jordan Henderson

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Liverpool FC ni miongoni mwa majina ya klabu ambazo huwa zinatumika kama neno la siri

Mamilioni ya watu huwa wanatumia 'neno la siri' ambalo ni rahisi mtu kuweza kukisia katika akaunti muhimu, utafiti umeeleza.

Utafiti uliofanyika na kituo cha usalama mitandaoni nchini Uingereza, kimebaini kuwa namba 123456 ndio namba ambazo zilitumika zaidi katika akaunti.

Utafiti huo umesaidia kuibua mapungufu katika utaalamu wa masuala ya kimtandao ambapo unaweza kuwaacha watu wakiwa katika hatari ya kudukuliwa.

Utafiti huo umesisitiza kuwa ni muhimu watu wanapaswa kuwa makini kutotumia namba tatu ambazo huwa zinatumika zaidi lakini wajaribu kutengeneza neno ambalo si rahisi mtu kuifahamu kirahisi.

Taarifa muhimu

Utafiti wa kwanza uliofanywa na kituo hicho cha utafiti umeeleza kuwa taarifa zilizosababisha akaunti kuingiliwa kwa maneno, misemo na masharti yaliyotumika .

Orodha kubwa ilikuwa ni katika namba 123456, ambazo zilionekana katika nywila zaidi ya milioni 23 zilitumia namba hizo.

Na namba nyingine ambazo zinatumika zaidi ni 123456789, ambapo si kazi kubwa kwa mtu kushindwa kuzishika au kuzihisi huku wengine walikuwa wanatumia neno la siri la 1111111.

Majina ambayo yamekuwa yakitumika katika neno la siri ni Ashley, followed by Michael, Daniel, Jessica na Charlie.

Na ukija kwenye ligi za mpira wa ulaya , neno la siri la timu hizo huwa ni rahisi sana , Liverpool ni washindi na Chelsea ni wapili. Na neno la siri ni rahisi 182 ya kujua chati za muziki.

Watu ambao huwa wanatumia maneno au majina katika neno la siri huwa wanajiweka katika hatari ya kudukuliwa , Dr Ian Levy, mtaalamu masuala ya ufundi NCSC.

"Mtu yeyote asilinde taarifa muhimu na neno la siri ambalo mtu anaweza kuhisi kirahisi kama jina la kwanza , timu ya mpira au bendi nzuri.

Neno la siri ambalo gumu

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti huo pia ulihoji namna ambavyo watu huwa wanalinda taarifa zao katika mtandao na uoga waliokuwa nao.

Taarifa zinasema kuwa watu asilimia 42 wanadhaniwa kuwa walipoteza fedha kupitia wizi wa mtandao na asilimia 15 walidai kuwa walihisi kuwa wana usalama wa kutosha kujilinda wenyewe kwenye mitandao.

Imebainika kuwa watu wachache kati ya watu ambao waliojiwa walikuwa walikuwa wanatenganisha , ambapo ikawa ngumu kukisia neno la siri katika akaunti zao hata katika barua pepe.

Mtaalamu wa usalama Troy Hunt, ambaye alizibaini akaunti ambazo zilidukuliwa ,anasema kuwa na neno la siri zuri ni jambo moja kubwa ambalo watu wanapaswa makini kutumia ili kulinda taarifa zao mtandaoni.

Aidha mtaalamu huyo wa mtandao amesisitiza kuwa bado haijafanyika kazi nzuri katika umakini kati ya watu wenyewe binafsi na makampuni ambayo huwa yanawataka kujiandikisha.

Kuwaacha watu kujua neno la siri gani ambalo limetumika zaidi , inabidi iwasisitize watu kuwa na uchaguzi mzuri.