Ligi kuu ya England: Ole Gunnar awaomba radhi mashabiki wa Man U

Meneja wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Meneja wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer

Meneja wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, ameomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya timu yake kukubali kichapo kizito cha goli 4-0 toka kwa Everton katika mchezo wa ligi kuu ya England.

United wamepoteza jumla ya michezo sita ya hivi karibuni ikiwa ni michezo nane katika michuano yote waliyokuwa wakishiriki ikiwemo ligi ya mabingwa barani ulaya.

Mchezo dhidi ya Everton ulikuwa ni muhimu sana kwa klabu hiyo katika mbio za kuwania nafasi nne za juu ili kuweza kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.

" Nataka niombe radhi kwa mashabiki wote wa klabu hii tulizidiwa katika kila idara ila tulipata hamasa ya kutosha toka kwa mashabiki wetu na tutajitahidi kufanya vyema siku ya jumatano." Hii ilikuwa Kauli ya Ole Gunnar Solskjaer, baada ya kumalizika kwa mchezo

Kwa Upande wake golikipa wa Man United David De Gea aliyekuwa nahodha katika mchezo huo amesema was " Ni ngumu kuweka katika manene vile anavyojisikia baada ya kipigo hicho kikubwa toka Ole apewe jukumu la kuinoa klabu hiyo."

Manchester United watashuka dimbani tena siku ya Jumatano kuwakabili majirani zao Manchester City wanauwania ubingwa kwa mara ya pili mfulizo.