Mzozo Sudan: Waandamanaji wajitenga na jeshi Sudan

Waandamanaji Sudan

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Waandamanaji wakusanyika mjini Khartoum

Waandamanaji nchini Sudan wamesema kuwa hawatambui utawala wa kijeshi uliyochukua uongozi wa nchi hiyo baada ya kumpindua kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Omar al-Bashir.

Wanadai kuwa baraza la kijeshi lililobuniwa baada ya Bw. Bashir kutimuliwa ni mwendelezo wa utawala wa wake.

Maelfu ya waandamanaji wamepiga kambi nje ya makao makuu ya kijeshi mjini Khartoumwakisubiri kutangazwa kwa baraza jipya la kiraia litakalochukua madaraka.

Huku hayo yakijiri serikali ya kijeshi ya Sudan limewaamuru waandamanaji hao kuondoa vizuwizi walivyoweka barabarani katika mji mkuu wa Khartoum mara moja ili kuruhusu usafirishaji wa bidhaa muhimu.

Jeshi liliwahi kutoa agizo kama hilo lakini waandamanaji walikataa kutii amri hiyo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Waandamanaji wameendelea kupiga kambi kati kati ya mji mkuu wa Khartoum

Hata hivyo msemaji wa waandamanaji hao Mohamed al-Amin amesema wanaonelea kuwa baraza la kijeshi ni "mwendelezo wa utawala wa zamani" na kuapa kuendelea na maandamano.

Je upinzani umeibuka Sudan?

Uchanganuzi wa mhariri wa BBC Afrika Fergal Keane

Umati mkubwa wa watu bado unaendelea kuandamana katika barabara za mji kuu wa Sudan, Khartoum.

Waandamaji hao sasa wanaelekea kubuni vuguvugu la upinzani linalopigania utawala wa kiraia.

Lakini swali ni je nini kitakachotokea endapo matakwa yao hayatatekelezwa na baraza la jeshi lililobuniwa kuongoza sudan kwa miaka miwili?

Viongozi wa mandamano hayo walit arajiwa kutangaza wanachama wao wa baraza la kiraia litakaloongoza Sudan hadi taifa hilo litakapoandaa uchaguzi wa kidemocrasia.

Lakini jana usiku - baada ya walikosa kufanya hivyo .

Hatua hiyo imezua gumzo kwamba huenda makundi kadhaa yanayoongoza maandamano hayo yametofautiana kuhusu suala la sera na nyadhifa zitakazobuniwa.

Kwa sasa majenerali wa baraza la kijeshi tayari wameanza kazi na wamepata uungwaji mkono kutoka Saudi Arabia na Milki za Kiarabu.

Viongozi wa maandamano wanapanga nini?

Kampeini ya kumuondoa madarakani Bw. Bashir iliongozwa na chama cha wataalamu nchini (SPA) ambalo limetoa pendekezo la kubuniwa kwa baraza la kiraia kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha mpito.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Waandamanaji wa Sudan wakipeperusha bendera ya kitaifa

SPA ilifanya mazungumzo na baraza la majeshi siku ya Jumamosi.

Mmoja wa wanachama wa ngazi ya juu wa SPA, Ahmed al-Rabia, awali aligusia kuwa mazungumzo hayo huenda yakafikia kubuniwa kwa baraza la kiraia lakini siku ya Jumapili alithibitisha kuwa maandamano yataendelea mjini Khartoum.

Waandamanaji wanataka baraza lao jipya libuni serikali ya mpito itakayoongoza hadi uchaguzi.

Jeshi limefanya nini?

Siku ya Jumapili jeshi lilisema kuwa litashughulikia ombi la wanainchi la kutaka utawala wa kiraia katika kipindi cha wiki moja, na kuongeza kuwa huenda ikaunda baraza la muungano wa jeshi na raia.

Jeshi pia liliwaachilia wafungwa wa kisiasa lakini siku ya Jumamosi liliwakamata washirika wakuu wa utawala wa wa Bw. Omaral Bashir.

Japo jeshi limeahidi kutowakamata au kuwaondoa waandamanaji barabarani limewaomba kusaidia ''kurudisha hali ya kawaida".

Mwezi Disemba mwaka 2018, serikali ilijaribu kufanya mabadiliko ya kiuchumi kwa kuweka mikakati ya kubana matumizi hatua ambayo ilizua maandamano ya kitaifa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Omar al-Bashir alipinduliwa na majeshi baada ya miezi kadhaa ya maandamano

Maandamani hayo yalichukua mkondo mwingine wa kutaka kumuondoa madarakani rais Omar ala Bashir.

Jeshi la Sudan lilimng'oa madarakani Bw. Bashir Aprili 11 lakini waandamanaji wameapa kutoondoka barabarani hadi pale utawala wa kiraia utakapochukua madarakani.

Waandamanaji ni kina naniho?

Hali ngumu ya kiuchumi iliwaleta pamoja raia wa Sudan kuandamana kwa miezi kadhaa kupinga utawala wa Bashi wa kiaka 30.

Uongozi wa maandamano hayo unawajumuisha madaktari, wafanyikazi wa afya na mawakili.

Idadi kubwa ya waandamanaji hao ni wanawake na vijana.