Mbunge wa upinzani uganda Bobi Wine kutoa taarifa ya maandamano leo

Wafuasi wa mbunge wa Kyadondo Bobi Wine

Msanii Bobi Wine anatarajiwa kuwasilisha rasmi barua kwa polisi kuwafahamisha kuhusu maandamano yake ya amani kupinga kuminywa kwa vyazo vyake vya mapato.

Hatua yake inafuatia polisi kuzuwia tamasha lake kwa madai kwamba hawakuwa na uwezo kudhibiti maelfu ya mashabiki wake.

Jana Bobi Wine ambaye ni mbunge wa upinzani ,alitiwa nguvuni kwa saa kadhaa baada ya baada ya kumkamata alipokuwa njiani kuelekea kwenye hoteli iliyoko ufukwenye mwa ziwa viktoria wambako alikuwa akipanga kuzungumza na waandishi wa habari kuzunguzia hatua ya mamlaka za serikali kumzuwia kufanya tamasha lake la Pasaka.

Nyimbo zake juu ya haki za kijamii zimemfanya kuwa maarufu hususan miongoni mwa vijana.

Rais Museveni anasema hatavumilia matamasha yanayochanganywa na siasa. Bwana Wine alisema Museveni anataka kuwazuwia wanamuziki wote ambao hawamuungi mkono.

''Rais Museveni amewaagiza polisi kuzuwia tamasha zangu kwasababu hapendi kile ninachokiimba. Alitaka mimi niwe kama baadhi ya wasanii wengine wanaoimba nyimbo za kumsifu na nilipokataa akaamua kuwa hataniruhusu kufanya onyesho lolote la mziki wangu nchini Uganda. Na kwa kuwa muoga alivyo, serikali yake hata imependekeza kuanzisha masharti kunizuwia hata kufanya tamasha nje ya nchi bila idhini ya serikali yake'', Alisema Bobi Wine

Video ya kukamatwa kwake ilionyesha polisi wa kuabiliana na ghasia wakiingia kwa nguvu ndani ya gari lakekatika eneo la Busabala.

Bobi Wine alikamatwa na kuingizwa katika gari la polisi na kupelekwa eneo lisilojulikana.

Polisi walifyatua gesi za kutoa machozi na kuwatawanya wafuasia wa Bobi Wine. Mwanamuziki huyo aliyegeuka na kuwa mwanasiasa ni miongoni mwa watu maarufu wanaomkosoa rais Yoweri Museveni.

Waandalizi wa tamasha hilo nao pia walidaiwa kukamatwa.

Wawili hao walikamatwa mapema siku ya Jumatatu na kuzuiliwa katika gari moja la maafisa wa polisi kabla gari hilo kuondoka nao.

Kukamatwa kwa Bobi Wine kunajiri baada ya rais Yoweri Museveni kusema kuwa hatokubali matamasha ya muziki uliojaa siasa na kuonya kwamba katika siku za usoni hakuna mtu atakayefidiwa kwa matamasha ambayo yamefutiliwa mbali kutokana na siasa.

Rais huyo alitoa onyo hilo wakati wa mkutano na wanachama na mapromota wa muziki nchini Uganda pamoja na wamiliki wa maeneo yanaopigwa muziki huo katika Ikulu ambapo alitoa shilingi bilioni mbili za Uganda kama fidia ya hasara waliopata baada ya maafisa wa polisi kufutilia mbali matamasha ya muziki wa Bobi Wine.

Awali polisi walitumia nguvu kulifungua gari ambalo mbunge huyo alikuwa akiabiri kabla ya kuvunja vioo vyake na kumtoa nje.

Hatahivyo mwanamuziki Nubian Li ambaye alikuwa akiandamana naye katika gari hilo hakukamatwa.

Hii sio mara ya kwanza kwa tamasha la Bobi Wine kuzuiliwa na maafisa wa polisi,

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Bobi Wine mwanamuziki mbunge Uganda

Mnamo tarehe 26 mwezi Disemba tamasha la nyota huyo lilizuiliwa na maafisa wa polisi

Msemaji wa polisi nchini Uganda, Emilian Kayima alisema kwamba Bobi Wine alikuwa hajaandika barua ya kuomba ruhusa kufanya tamasha hilo ndio maana hawakuweza kumruhusu.

"Tutakuwa katika ufukwe wa Busabala kuzuia shughuli hiyo na kuhakikisha usalama upo. Tamasha hilo halikuwa limeruhusiwa kufanyika kwa sababu ya kutokidhi vigezo", Kayimba alisema.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda limeeleza kwamba , Bobi Wine aliandika kwenye mtandao wa kijamii kuwa kikosi cha usalama kimevamia tamasha lake la 'One Love Beach huko Busabala'na kuwakamata wafanyakazi wake.

Hili lingekuwa tamasha la pili la Bobi Wine kufanyika, tangu ashtakiwe na kufungwa kwa mshtaka ya uhaini.

Mwanzoni mwa mwezi Novemba mwanamziki huyo aliruhusiwa kufanya tamasha lake la kwanza kwa sababu lilikuwa la kiburudani na halikuwa la kisiasa.

Maelfu ya watu waliohudhuria tamasha hilo walivaa nguo nyekundu, rangi inayohusishwa na vuguvugu za Bobi Wine.

Chanzo cha picha, AFP

Lakini vilevile tamasha hilo lilikuwa na idadi kubwa ya polisi.

Bobi Wine anadaiwa kuteswa na kupigwa akiwa kuzuizi mwezi Agosti, madai yanayokanwa na mamlaka.

Chanzo cha picha, Getty Images

Bobi Wine na wenziwe 32 walikamatwa baada ya kudaiwa kushambulia msafara wa Rais wa Yoweri Museveni mjini Arua mwezi uliopita na kuwekwa katika kizuizi cha jeshi.

Watuhumiwa hao waliwekwa chini ya ulinzi wa jeshi huku Bobi Wine awali akipandishwa katika mahakama ya kijeshi kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Rais Yoweri Museveni alijitokeza na kukanusha taarifa kuwa Bobi Wine ameumizwa vibaya na kuvishutumu vyombo vya habari kwa kueneza taarifa za uongo.

Baada ya kelele za upinzani kupazwa ndani na nje ya Uganda pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, kesi yake mbele ya mahakama ya kijeshi ilifutwa na kuachiwa huru kabla ya kukamatwa tena na kufunguliwa mashtaka ya uhaini katika mahakama ya kiraia.

Ni kipi kilisababisha mashtaka ya uhaini?

Chanzo cha picha, Getty Images

Kabla hajakamatwa, Bobi Wine, alichapisha picha ya dereva wake ambaye alisema alipiwa risasi na kuuliwa na polisi waliodhani kuwa aliyekuwa ni yeye.

Bobi Wine alikamatwa tarehe 13 Agosti baada ya mkutano wa kampeni kaskazini-magharibi kwenye mji wa Arua ambapo kuna madai kuwa msafara wa rais ulitupiwa mawe.

Mwanamuziki huyo mwenye miaka 36 awali alishtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi kwa makosa ya umiliki wa silaha kinyume cha sheria, mashtaka ambayo yalifutwa baadaye. Kisha akafunguliwa mashtaka ya uhaini kwenye mahakama ya kiraia.

Bobi Wine ni nani?

Chanzo cha picha, AFP

Nyota huyu wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, na anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.

Alizaliwa 12 Februari 1982, Bobi Wine na alikuwa na miaka minne pekee Museveni alipoingia madarakani mwaka 1986.

Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu.

Alilelewa katika mtaa duni wa Kamwokya kaskazini mashariki mwa Kampala na alianza kujihusisha katika muziki mapema miaka ya 2000.

Nyimbo zake za mtindo wa dansi za 'Akagoma' na 'Funtula' zilikuwa maarufu sana miongoni mwa vijana.

Ana shahada ya muziki, dansi na uigizaji kutoka Chuo Kikuu cha Makerere ambapo alihitimu mwaka 2003.

Aprili 2018 alifuzu na stashahada ya masuala ya kisheria kutoka Kituo cha Maendeleo ya Sheria, Kampala.

Alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka 2017 wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.

Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).

Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kuangazia zaidi kuwaunganisha raia.

"Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki...Ninataka siasa zitulete pamoja... jinsi muziki ufanyavyo."

Ufuasi wa Vijana

Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kuwa changamoto kubwa kwa rais wa miaka mingi Yoweri Museveni.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Bobi Wine anajiita "Ghetto President" na anaungwa mkono zaidi na vijana

"Chama chake kitawaza iwapo sasa huu ni msururu. Bobi Wine sasa amemshinda Museveni na kiongozi wa upinzani Kizza Besigye mara nne'' katika uchaguzi mdogo.

"Bobi amepata ufuasi kwa nemba yake ya 'nguvu za watu', na ananuia kushinikiza na kupanga liwe vuguvugu," anaongeza.

Mchambuzi wa kisiasa Robert Kirunda anasema mvuto wa Wines unatokana na kuwepo 'pengo la uongozi' Uganda.

"Kuna vijana wengi Uganda ambao hawana haja ya kujua vita vya kihistoria vilivyoiingiza NRM uongozini, au ukaidi wa upinzani mkuu. Wengi wanataka ajira na wanahisi uchumi hauwasaidi."

Kirunda anasema Wine 'anapigia upatu sana'. "Anaweza kushinikiza watu pakubwa, lakini bado hajapata nguvu kama alizonazo Besigye katika upinzani".