Zari Hassan apata mpenzi mpya lakini aficha sura yake

Zari Hassan
Maelezo ya picha,

Mfanyabiashara wa Uganda Zari Hassan

Mfanyabiashara wa Uganda na mpenzi wa zamani wa nyota wa muziki wa bongo nchini Tanzania Diamond Platinumz, Zari Hassan amepata mpenzi mpya yapata mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu alipotangaza kuvunjika kwa uhusiano wake na mwimbaji huyo wa 'Zilipendwa na Hallelujah'

Mpenzi huyo mpya ambaye amemtaja kuwa Bwana 'M' katika mtandao wake wa Instagram ndiye aliyechukua mahala pake Diamond.

Akitangaza uhusiano wake mpya katika mtandao huo wa kijamii siku ya Ijumaa jioni, Zari Hassan alisema kuwa mpenzi wake mpya amemkubali yeye pamoja na watoto wake wote watano.

Chanzo cha picha, Zari Hassan/Instagram

''Kwako wewe mpenzi nimejifunza mengi; Nakumbatia maisha yalivyo kwa sababu ya unyenyekevu wako. Nimekuwa nikifikiria maisha yangu ya baadaye lakini sikuweza kujua maisha hayo yatakuwa vipi. Watoto watano, wanaume wengine lakini bado ukaniona mimi kuwa mwanamke mrembo zaidi'', alisema Zari katika chapisho lake ambalo limevutia majibu 100,000.

''Nakupenda sana bwana M, na sio vitu vyenye thamani unavyonionyesha, nimeviona hivyo na hata vikuu na vizuri zaidi. lakini ni wewe, moyo wako, uwepo wako na vile unavyotufanya mimi na wanangu kukuhisi. Wewe ni jasiri sana bwana M: Watoto watano ; mimi mwenyewe nina umri wa miaka 38...wow...umetumwa kutoka mbinguni mpenzi. Nakupenda bwana M'',aliongezea Zari katika chapisho hilo.

Mfanyabiashara huyo wa Uganda alizungumzia kuhusu nafasi yake katika kujenga maisha ya wapenzi wake wa awali ambao anasema hawakumpenda kwa dhati.

Zari hakusita kuwakemea wale wanaodai wanamjua mpenzi wake mpya katika ukurasa wake wa Facebook.

''Wacheni kile amabcho wanablogu wanachapisha lengpo nlao ni kuvutia usomaji katika blogu zao'', alisema.

Chanzo cha picha, Zari Hassan/ Facebook

''Mimi hupenda na huwajenga wanaume wangu, mimi sio mtu anayekusanya na kuondoka, mimi hutazama kile tulichokubaliana kwa lengo la kuongeza baraka'', alisema.

Chanzo cha picha, Zari Hassan/ Instgram

Tangazo hilo limevunja matumaini ambayo wafuasi wa Zari Hassan na Diamond walikuwa nayo -kwamba siku moja pengine wawili hao watarudiana.

Ni wakati wa siku ya wapendanao ya Valentines Day 2018 ambapo zari Hassan aliingia katika mtandaoi wake wa Instagram ambapo ana wafuasi milioni 5.4 ili kutangaza kwamba alikuwa anasitisha uhusiano wake wa miaka 3 na nyota huyo wa wimbo wa 'tetema'.

Zari Hassan alilaumu uzinzi na ukosefu wa heshima kama kitu kilichomshinikiza kujitenga na Diamond.

Hathivyo Diamond aliamua kuendelea na maisha yake na mtangazaji wa Kenya tanasha Oketch ambaye ameapa kufunga ndoa naye.

Zari Hassan ana watoto wawili na Diamond na wengine watatu na mumewe wa zamani marehemu Ivan Ssemwanga.

Tayari kuna habari kwamba Diamond na Tanasha wameanza maandalikzi ya harusi yao kimya kimya.