Chanjo ya malaria kwa watoto kufanyiwa majaribio Malawi

Mtoto akipewa chanjo

Chanzo cha picha, D Poland/PATH

Maelezo ya picha,

Chanjo hiyo tayari imeenza kufanyiwa majaribio kwa kiwango kidogo

Chanjo ya kwanza ya malaria duniani imeanza kufanyiwa majaribio nchini Malawi.

Chanjo hiyo inayofahamika kama RTS,S ina mchanganyiko wa dawa inayoisaidia mfumo wa kinga mwilini kukabiliana na mbu wanaosababisha malaria

Majaribio ya awali ya chanjo hiyo ilionesha kuwa inafanya kazi kwa 40% kwa watoto wa kati ya miezi mitano hadi saba waliyopewa.

Visa vya ugonjwa wa malaria vimeongezeka tena baada ya miongo kadhaa ya kukabiliana nao.

Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibu visa vya ugonjwa huo duniani vinaendelea kuongezeka, hali ambayo imezua hofu huenda ikarudisha nyuma juhudi zilipigwa kukabiliana nao

Zaidi ya 90% ya watu 435,000 waliyopata maradhi ya malaria barani wa Afrika walifariki huku watoto wakiathiriwa zaidi.

Malawi ambayo iliripoti karibu visa milioni tano vya ugonjwa wa malaria mwaka 2017 na imechaguliwa kufanyiwa majaribio ya chanjo ya pamoja na mataifa ya RTS,S.

Mataifa mengine yatakayofanyiwa majaribio ya chanjo hiyo ni Kenya na Ghana.

Mataifa hyo yamechaguliwa kwa sababu tayari yanaendesha kampeini ya kubwa ya kukabiliana na malaria lakini bado visa vya ugonjwa huo bado viko juu.

Chanjo hii imekuwa ikifanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka 30.

Mashirika ya kadhaa yamechangia ufadhili utafiti huo ambao unakadiriwa kugharimu dola bilioni moja.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanaharakati wamekua wakishinikiza kutafutwe mbinu bora zaidi ya kukabiliana na malaria

Majaribio ya chanjo hiyo inaongozwa na shirika la Afya Duniani (WHO), na linasema hii ni mara ya kwanza kinga ya malaria inatolewa kwa watoto.

Inakadiriwa kuwa chanjo hii mpya inafanya kazi kwa 40% ikilinganishwa na chanjo zingine, lakini WHO linasema RTS,S itaimarisha kinga zaidi kwasababu vyandarua vya kuzuia mmbu na dawa zingine tayari zinatumika, ilisema ripoti ya shirika habari la AFP.

"chanjo iliyo na uwezo wa kutoa kinga kwa 90% au zaidi, kwa maoni yangu si kitu tunachokiangazia kwa sasa," kituo cha Bloomberg kilimnukuu afisa wa WHO, Mary Hamel.

"Lakini viwango vilivyofikiwa katika utengenezaji wa chanjo hii inaashiria kuwa hata chanjo ya malaria inaweza kutengezezwa. Itatoa mwelekeo mzuri."

Chanjo hiyo inahitajika kupeanwa mara nnes - mara moja kila mwezi kwa miezi matatu alafu dozi ya nne inapeanwa miezi 18 baadae.

Awamu hii ya majaribio inatarajiwa kukamilishwa mwaka wa 2023, kwa mujibu wa shirika la PATH.

Chanjo hiyo imeanza kufanyiwa majaribio nchini Malawi na mpango huo utaendelezwa Kenya na Ghana katika mda wa wiki chache zijazo.