Chelsea yarejea katika nne bora Epl

Jeff Hendrick

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jeff Hendrick

Vuta ni kuvute ya kuwania nafasi nne za juu ya ligi ya England inaendelea kushika kasi huku ligi hiyo ikiwa inaelekea mwishoni

Chelsea wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge wamevutwa shati kwa kulazimishwa sare ya magoli 2-2 na Burnley.

Burnley ndio walikuwa wa kwanza kuandika goli langoni mwa Chelsea kwa goli la Jeff Hendrick ikiwa ni dakika ya nane ya mchezo, lakini katika dakia ya kumi mbili N'Golo Kante aliisawazishia timu yake goli hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji Gonzalo Higuain, aliwapa Chelsea uongozi wa muda kwa kufunga goli la pili katika dakika ya kumi nne

Mshambuliaji Gonzalo Higuain, aliwapa Chelsea uongozi wa muda kwa kufunga goli la pili katika dakika ya kumi nne, Nae mshambuliaji wa Burnley Ashley Barnes akawanyima Chelsea alama tatu muhimu kwa kusawazisha goli hilo kwenye dakika ya ishirini nan ne kipindi hicho hicho cha kwanza.

Licha ya sare hiyo Chelsea wamejisongeza mpaka kwenye nafasi ya nne ya msimamo wa ligi wakiwa na alama 67, wakiwazidi Arsenal kwa alama moja na pia wakiwazidi Manchester United kwa alama tatu, ila wao wako mbele kwa mchezo mmoja wakiwa wamecheza jumla ya michezo 35 huku wanaowania nao nafasi ya nne bora wakiwa na michezo 34.

Ligi hiyo inaendelea tena leo kwa michezo miwili Tottenham Hotspur wanaowania kusalia katika ya nne bora watakuwa na kibarua pevu dhidi ya Brighton & Hove Albion, huku katika dimba la Vicarage Road Watford watakuwa wenyeji wa Southampton.