Sanaa: Je kiini macho kinaweza kufunzwa shuleni?

  • Yves Bucyana
  • BBC Africa, Kigali
Msnii wa kisiri macho

Je ni kweli kiini macho ni sayansi inayoweza kufundishwa shuleni?

Fikra za wengi ni kwamba kiini macho ni uchawi, lakini kijana Kwizera Huguo kutoka Burundi ambaye sasa nchini Rwanda, anasema kisiri macho ni sanaa kama muziki,uchoraji na nyinginezo.

Ndoto yake ni kuanzisha shule ya kufundishia sanaa ya kufanya kisiri macho katika nchi za afrika mashariki.

''Hapa Afrika hakuna shule ambayo inafundisha kiini macho lakini watu walio na interneti wanaweza kusoma sanaa hii kupitia mtandao''alisema Kwizera.

Japo alisomea teknolojia ya mawasiliano na kupata shahada ya chuo kikuu cha Burundi, anasema alipendelea zaidi sanaa ya kufanya kiini macho ambayo alijifundisha kupitia interneti.

Anasema kuwa mtu anaweza kufanya mambo mengi katika fani ya kiini macho kwa mfano kumeza pulizo, wembe , mishumaa au kuficha sarafu ndani ya jicho na mengine mengi ambayo huonekana kuzidi akiliza watu.

''Naweza kusimama mbele yako nikiwa na nguo na wewe ukathibitisha hilo halafu nikatoweka na kuacha nguo chini bila ya wewe kuniona nikizivua''aliongeza Kwizera.

Watu wengi hufananisha kisiri macho na ushirikina au matumizi ya nguvu nyingine zisizoonekana lakini Huguo mwenye umri wa miaka 24 anasisitiza kuwa hiyo ni dhana potovu.

Kwizera anasema kupitia uzoefu aliyonayo anaweza kutoweka na kurudi machoni pa watumbuizaji wake lakini mataifa mengi hasa barani Afrika hayana maduka ya kuuza vifaa vya kufanyia sanaa ya kisiri macho'

Kuitwa mchawi

Sawa na sanaa nyingine yoyote pia kiini macho pia ina changamoto zake.

Kijana Kwizera anakabiliwa na wakati mgumu kuwaelezea watu kuwa yeye si mchawi.

''Watu wananiomba niwafanyie dawa ya kuimarisha biashara zao juu washaniona vitu nafanya lakini hiyo ni probleme kwasababu hawtu hajafika level ya kujua kuwa hii ni kama sayansi na mimi niko Artiste'' anasema msanii huyo.

Kwa sasa hivi anafanya kazi na kundi la wasanii wa sanaa ya kiini macho kutoka Burundi linajulikana kama Magic Guards.

Kundi hilo linanuia kuanzisha kituo cha kufundisha vijana sanaa ya kiini macho katika nchi za afrika mashariki.