Afrika Kusini: Maporomoko ya udongo yaliyotokana na mvua kali yaua watu 60 Durban

A destroyed house by the beach

Chanzo cha picha, Reuters

Maporomoko ya udongo yaliyotokana na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 60, katika mikoa ya Durban na KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini, maafisa wanasema.

Zaidi ya watu 1,000 wameondoka kutoka makaazi yao kwa mujibu wa rais Cyril Ramaphosa ambaye ametembelea maeneo yaliyoathiriwa.

Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika maeneo ya Kusini na Mashariki ya nchi hiyo siku chache zilizopita.

Mafuriko zaidi na upepo mkali unatarajiwa katika maeneo ya pwani huku onyo likitolewa kuhusu hali mbaya ya hewa.

Mafuriko hayo makubwa yaliharibu biashara na nyumba za watu pamoja na vyuo vikuu viwili - huku mamia ya watu wakifurushwa makwao.

Maelezo ya picha,

Watu wamekua wakifarijiana huku wakitathmini uharibifu uliyosababishwa na mafurok ahayo

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amezitembelea familia zilizopoteza wapendwa wao katika mafuriko hayo.

Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko anaarifu kuwa rais aliweka shada la maua katika eneo ambalo watu wanane wallifarika.

Pia alionekana akiwasukuma walinzi waliokuwa wakiwazuia watu kusema nae.

"Ni muhimu kuja kuona kile kilichofanyika au kilichotokea na kuomboleza na familia zilizopoteza wapendwa wao katika janga hili. Kupoteza maisha sio jambo rahisi, hasa maafa yakitokea ghafla," alisema Bw. Ramaphosa.

Maelezo ya picha,

Watu kadhaa wafariki baada ya kuzikwa na maporomoko ya tope

Siku ya Jumatano, alitoa taarifa ya kusema kuwa: "Hali hii inatuhitaji sote kuja pamoja kama taifa kufikia jamii zilizosthirika."

Huku hayo yakijiri, waziri wa utawala wa mkoa Nomusa Dube-Ncube ameiambia maafisa wa kituo cha radio cha SAFM kwamba bado wanaendelea kutathmini kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mkasa huo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Siku zijazo watu watalazimika kuhamishwa kutoka maeneo yaliyoathirika, alisema.

Watu kadhaa wamepelekwa hospitali huku shughuli ya kuwatafuta manusura waliyozikwa chini ya vifusi vya majengo yalioporomoka