Wanawake wa Afrika wanakabiliwa na aibu ya kukosa nywele kichwani

  • Na Aaron Akinyemi
  • BBC Africa
Kichwa cha Bandile

Chanzo cha picha, Bandile

Miaka kadhaa ya mitindo tofauti ya nywele ikiwemo kutengeza rasta, kusuka , kuchoma nywele na kushona kumemuwacha mwanamitindo mwenye maono mengi aliye na umri wa miaka 31 nchini Afrika Kusini akiwa bila nywele.

''Kila mara nilipokuwa nikitoa nywele zangu bandia saluni nilipendelea kuchoma nywele zangu asili na kemikali kabla ya kuvaa nywele bandia nyengine siku hio hio-sikuwa na nywele zangu asli'', alisema Bandile ambaye sio jina lake.

Ni hali ya kupoteza nywele kwa jina traction alopecia , na alikuwa katika shule ya upili wakati alipogundua kwamba nywele zake zilikuwa zikianguka.

Lakini mkaazi huyo wa Johannesburg hayupo pekee-hali hiyo huathiri thuluthi moja ya wanawake kutoka Afrika, kulingana na utafiti wa jarida la matibabu kuhusu urembo na uchunguzi wa magonjwa ya ngozi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanawake kutoka Afrika wameshauriwa kufikiria kuhusu mitiundo yao ya nywele ili kuepuka kupoteza nywele zao

Utafiti uliofanywa miaka mitatu iliopita wa takriban wanawake 6000 kutoka Afrika na chuo kikuu cha Boston kuhusu sayansi inayoangazia magonjwa pamoja na kuyadhibiti ulibaini kwamba takriban asilimia 48 ya waliofanyiwa utafiti huo walikuwa wamepoteza nywele zao katika komo ama hata katika katikati ya kichwa.

Huku mjadala huo ukidaiwa kukumbwa na usiri mwingi, huenda takwimu hizo ziko juu zaidi.

Iwapo sote tungeweza kutoa nywele zetu bandia kazini, wanawake 8 kati ya kumi wangekuwa na tatizo la nywele.

''Ni kitu ambacho hatupendi kuzungumzia tunahisi aibu'' , alisema Bandile.

Daktari aliniambia nilikuwa nikivuta nywele zangu kutoka katika mizizi yake wakati nilipokuwa nikiweka nywele bandia kwa kutumia gamu. Gamu hiyo haikuondolewa hivyobasi ikaharibu njia za mizizi ya nywele yangu.

Imani potofu kuhusu nywele asili

Bandile analaumu imani potofu kwamba mtu anaposukwa nywele huzifanya nywele hizo kumea.

Imani tulipokuwa nayo ni kwamba nywele bandia zinaweza kuangaliwa rahisi zaidi ya nywele asili.

Na takwimu nyengine zinasema kuwa wanawake barani Afrika hutumia takriban dola bilioni 6 kununua nywele bandia na rasta kila mwaka.

''Kila mwanamke anahisi kuwa wa kisasa anapovalia nywele bandia. Nusu yetu tunahisi kwamba unapokuwa na nywele bandia zilizo ndefu na nywele za kawaida ndefu unaonekana kuwa mrembo na unakubalika zaidi katika jamii'', anasema.

''Kila mwanamke mweusi ninayemjua hupenda nywele zake kuwa ndefu . husuka laini nyembamba nyembamba kando kando ya laini ya nywele, swala linalofanya nywele hizo kuvutika''.

Susan Magai
BBC
Most of the women are using the wrong glue for their weaves or maybe they leave their braids or weaves in for extended periods of time"
Susan Magai
Tanzanian hair salon owner

Ni hadithi ambayo Susan Magai ambaye anamiliki saluni ya urembo katika mji wa Dar es salaam nchini Tanzania anaifahamu.

''Wanawake wengi wanatumia gamu isiostahili kuweka nywele bandia ama mara nyengine huwacha nywele hizo kwa muda mrefu bila kuzitoa'', anasema.

''Tunawashauri wateja wetu kuvalia nywele bandia kwa kipindi cha wiki mbili pekee lakini wengine wanaziwacha hadi kwa kipindi cha miezi mitatu kabla ya kuanza kupoteza nywele zao''.

Saluni ya bi Maiga inatoa huduma ya tiba ya mvuke unaofungua mashimo yaliomo katika ngozi ya kichwa ili kuruhusu nywele kumea.

Huduma hiyo ni sawa na kupika nywele hizo .

''Tunatumia mafuta ya nazi na kupaka katika ngozi ya kichwa . Baadaye tunazifunga nywele na kuzipika kwa kutumia mashine'', anasema, akiongezea kwamba inaweza kuchukua miezi kadhaa kabla ya athari hizo kuonekana.

Kuwa na kipara baada ya kuzaliwa

Bandile alijaribu kutumia tiba ya kutumia pilipili ili kufungua mashimo hayo ya kichwani na ilipofeli alitumia dawa ili kufannya nywele zake zimee.

''Nywele zilikuwa zikimea lakini ilikuwa ghali mno hivyobasi nikashindwa kuendelea'' , alisema mwanamitindo huyo ambaye anapanga kuonana na na mtaalamu wa nywele kwa lengo la kupandikizwa nywele mnamo mwezi Juni.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Biashara ya nywele Afrika inashirikisha mabilioni ya madola

Daktari mmoja nchini Uingereza Jumoke Koso-Thomas, ambaye huangazia na kuchangia katika blogi moja inayoangazia afya ya wanawake weusi anasema kuwa huku mitindo ya nywele ikichangia kwa visa vingi vya alopecia kwa wingine kuna swala la jeni.

''Kwa mfano , ukosefu wa nywele unaweza kuwa dalili za tatizo la tezi ama kibofu cha mkojo'' , anasema.

Chanzo cha picha, Boitumelo Monyaki

Maelezo ya picha,

Boitumelo Monyaki anasema kuwa nywelel zake zinamea lakini bado ni nyepesi mno.

''Nimegundua kwamba wanawake wengi katika familia yangu hupoteza nywele zao baada ya kujifungua'', anasema.

Ni swala ambalo limekuwa likitokea tangu wakati wa bibi yangu.

Bi Monyaki anasema kuwa kupoteza nywele zake kumeathiri imani yake lakini amejifunza kukubali kwamba nywele zake haziwezi kumea tena kama zilivyokuwa.

''Anataka kuona kwamba kuna usaidizi zaidi kwa wanawake wa Kiafrika wanaokabiliana na kupotea kwa nywele. Hata wamiliki wa saluni na wasukaji hawajui kutatua tatizo hili."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chakula kizuri kinaweza kuimarisha nywelele zako kichwani.