Je, komputa inaweza kutengeneza sanaa nzuri zaidi ya binadamu?

This portrait was created by computer, so is it really art and is it any good?

Chanzo cha picha, CHRISTIE'S

Maelezo ya picha,

Picha hii imechorwa na komputa, lakini je hii ni sanaa ya kweli na inavutia?

Ni picha ya ukutani iliyochorwa na msanii ambaye hujawahi kumuona au kumsikia kwa dola 432,000. Na kwa muonekano tu picha hiyo haina mvuto lakini imeweza kununuliwa kwa gharama kubwa.

Maswali mengi yanajitokeza juu ya picha hii ambayo imechorwa kwa komputa;

  • Je, inawasilisha sanaa halisi?
  • Je, kuna utofauti wowote kati ya picha iliyochorwa na msanii na iliyochorwa na mashine kama watu wapo tayari kununua sanaa ya namna hiyo?
  • Akili bandia inayotumika , inaweza ikafikiria au ikakaribiana na akili ya binadamu?
  • Ubunifu huu unamaanisha nini kwa wasanii na tasnia ya ubunifu kwa ujumla?

Tayari komputa imeweza kufanikiwa kutengeneza sanaa ya mashairi na muziki lakini ubunifu huo unatoa taswira ya kile ambacho kilikuwepo na huo sio ubunifu .

Ubunifu ni kutengeneza kitu ambacho ni kipya au kuja na namna mpya ya kutatua tatizo.

Sanaa ni zaidi ya kutatua tatizo

Chanzo cha picha, HELLO GAMES

Michezo ya komputa ambayo haswa inatumia sauti ya kutengeneza imekuwa mifumo mizuri ambayo imetengenezwa ili kutatua tatizo la ubunifu.

Lakini kutengeneza kitu bila kushirikisha ubunifu wa binadamu haiwezi kuleta matokeo chanya ambayo yanaweza kumfurahisha binadamu kutumia.

Swali la je, chombo kinachoongozwa na mfumo wa komputa kinaweza kuleta maana katika dunia hii kwa kutumia ujuzi wake peke yake.

Chanzo cha picha, BRIAN RUGANGIRA

Maelezo ya picha,

Picha ya iliyochorwa na msanii

"Mashine hiyo inastaajabisha jinsi inavyofanya mambo mengi sana ya kushangaza lakini hulka ya binadamu huwa inataka kuwa na kitu ambacho imekitengeneza.

Ubongo wetu una tabia ya kutaka kuhisi nguvu ya ubongo wa binadamu umetumika katika jambo ambalo ni gumu kulitengeneza,"Mtaalam wa Sanaa alieleza.

Huku Dr.Lopez ambaye ni mtaalamu wa Sanaa aliainisha ubunifu wa sanaa ya kweli inavyotofautiana katika kutatua tatizo inapohitajika kwa namna ambayo mashine haiwezi na haina uwezo wa kufanya jambo la namna hiyo.

"Sanaa hiyo haiwezi kuonesha matamanio au uoga .

Inawezekana ubunifu huu unaweza kuwa na maana zaidi kama mashine hizo zitafanya kazi sambamba na wasanii wenyewe.

Ili kuweza kuonyesha utofauti wa fikra, na uhusiano wa ubunifu na teknolojia", mtaalam asisitiza.

Chanzo cha picha, DR ALICE ELDRIDGE

Aidha aliongeza kueleza kuwa teknolojia hii ni tishio kwa wasanii, ingawa anaamini kuwa mashine haziwezi kuchukua au kushindana na wasanii .

Mashine hizo zinaweza kutumika kupunguza ubunifu wa watu wanaotaka kutengeneza fedha lakini sio teknolojia ambayo inawajibika kufanya kazi za sanaa.

Teknolojia haiwezi kuwa nzuri vya kutosha kama haitakuwa inaongozwa na binadamu