Rais Duterte: ''Ufilipino sio danguro la taka'' la Canada

Rais Duterte ametishia kurejesha takataka nchini Canada

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Duterte ametishia kurejesha takataka nchini Canada

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameifokea nchi ya Canada kwa kushindwa kuchukua hatua juu ya takataka ilizosafirisha hadi katika nchi yake iliyopo kusini mashariki mwa Asia miaka kadhaa iliyopita.

Nchi hiyo imewasilisha mara kadhaa malalamiko yake kidiploamasia kupinga hatua ya Canada ya kutuma tani za uchafu nchini Ufilipino kati ya mwaka 2013 na 2014.

Wiki hii rais Duterte alitishia kurejesha takataka hizo nchini Canada.

Canada inasema "ina nia sana" ya kutatua swala hilo na itashirikiana na Wafilipino kufanya hivyo.

Rais Duterte aliikosoa Canada juu ya mzozo huo wa muda mrefu wa kidiplomasia , akisema imeibadilisha nchi yake saying it is kuwa "dangulo la kutupa uchafu".

"Kuhusiana na taka za Canada , ninataka maboti yaandaliwe," alisema Jumatatu, na kuongeza kuwa: "ni bora wavute hicho kitu nje ya nchi yetu au nipeleke meli za uchafu wao huko''.

"Ngoja tupambane na Canada. Nitatangaza vita dhidi yao."

Rais Duterte anafahamika kwa mtindo wake wa kutoa kauli za wazi na mara nyingi hutumia lugha na kauli kali zenye utata.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uchunguzi ulibaini kuwa baadhi ya makontena yalikuwa na chupa za plastiki na mifuko, takataka za nyumbani na nepi za watu wazima zilizotumiwa (diapers)

Kauli zake za Jumatatu zilihusu kontena zilizotumwa kwa meli katika mji mkuu Manila, na kampuni ya kibinafsi ya Canada kwa ushirikiano na wadau wau wa Ufilipino.

Serikali mjini Manila inasema makontena hayo yaliyowasili katika bandari ya kimataifa ya Manila, yaliwekwa utambulisho gushi, ambapo yaliandikwa kuwa yalikuwa na plastiki ambazo zingetumiwa kutengeneza bidhaa nyingine , lakini ukweli ni kwamba yalikuwa yamesheheni vifaa vikuukuu mbali mbaloi vya nyumbani.

Uchunguzi ulibaini kuwa baadhi ya makontena yalikuwa na chupa za plastiki na mifuko, takataka za nyumbani na nepi za watu wazima zilizotumiwa (diapers).

Uchunguzi mwingine iwa kontena zilizosalia 2015 ulibaini kuwa zilikuwa na uchafu mwingine usio hatari, zikiwemo taka za nyumani na mitaani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau (kushoto) akiwa pamoja na rais wa Ufilipino Lodrigo Duterte

Maafisa wa Ufilipino walitoa malalamiko yao kwa Canada kwa mara ya kwanza 2014. Serikali inasema makontena hayo yamesababisha mlundikano katika bandari na ni hatari kwa afya ya umma.

Baadhi yamesalia kwenye magala katika bandari ya Manila na mengine yametupwa kwenye dangulo la wazi.

Mnamo mwaka 2016, mahakama ya Ufilipino iliamuru uchafu huo urejeshwe kwa meli hadi Canada kwa garama ya aliyeyatuma.

Mwaka huo huo, Canada ilifanya mabadiliko ya sheria zake juu usafirishaji wa takataka hatari ili kuzuwia jambo kama hilo kutokea tena.

Mapema mwaka huu, muungano wa makundi ya mazingira katika nchi zote mbili ulimuandikia waraka waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau ukitaka uchafu huo urejeshwe kwa aliyeuleta.

Maafisa wa pamoja wa masuala ya kiufunzi kutoka nchi zote mbili kwa sasa wanachunguza "masuala yote yanayohusiana na kuondolewa kwa taka hizo ", ilisema taasisi ya Mazingira ya Canada katika taarifa yake kwa BBC iliyotolewa Jumanne.

Changamoto ya uchafu wa dunia - na kule unakotiupwa imekuwa ikiendelea kuongezeka kote duniani.

Chinailianzisha marufuku kwa " taka za kigeni" kama hatua ya kuboresha sekta ya taka katika kipindi ch amwaka mmoja tu uliopita.

Kiwango cha plastiki kinachochukuliwa na Uchina kilishuka kwa 94% baina ya mwaka 2016-17 na 2017-18, huku Malaysia, Uturuki Poland na Indonesia zikipunguza kiwango cha taka kutoka nje.

Umoja wa Mataifa unasema soko la taka za dunia kuanzia ukusanyaji wake hadi pale zinapotumika kutengeneza bidhaa nyingine hugharimu $410bn (£316bn).