"Daktari aliainisha jinsia ya mwanangu kwa alama ya kuuliza"

Doctor recording baby's sex as a question mark

Wakati ambapo daktari alipoandika alama ya kuuliza badala ya jinsia ya mtoto kwenye karatasi ya kuzaliwa kwa mtoto wake, bi. Catherine aliamua kwenda kufungua kesi katika mahakama ya juu ili kuhamasisha Kenya kubadilisha namna ambavyo wanatambua watoto wenye jinsia mbili.

Mwaka huu ni 2009.

Ni miaka mitano tangu Catherine(sio jina lake halisi ) ajifungue mtoto wake wa kwanza akiwa nyumbani kwake Nairobi. Lakini kulikuwa na tatizo.

"Kuna kitu ambacho kilikuwa hakiko sawa kwa mtoto", Catherine aeleza.

Catherine alimuita jirani yake ili aje kumuona mtoto wake na alipofika alimuonyesha sehemu za siri za mtoto wake na jirani akainama chini.

Alionekana akiwa kimya.

Bila kutambua tatizo la hali hiyo, jirani huyo alimwambia Catherine asiwe na wasiwasi na kumuhakikishia kuwa mtoto atakuwa mzima.

Lakini Catherine alikuwa anataka kusikia mawazo ya mtu mwingine . Hivyo akamualika binamu yake ili amuone mtoto .

"Binamu yangu aliniuliza tatizo ni nini , nikamwambia aende akamuone mtoto ."

Binamu yake Catherine alikubali kuwa kuna kitu ambacho akionekani sawa na hivyo akamshauri kwenda hospitalini.

Siku iliyofuata Catherine na mume wake ili walienda kumuona daktari wa kijijini kwao, na walipofika daktari aliwapa rufaa ya kwenda kwenye hosptali ya taifa ya Kenyatta.

Majibu ambayo waliyatoa hosptalini yaliwashangaza wazazi wa mtoto wao.

Catherine na mme wake waliambiwa kuwa mtoto wao alikuwa amezaliwa na jinsia mbili. Yaani mtoto ana jinsia ya kike na kiume.

Katika karatasi ya hospitalini sehemu ambayo jinsia inaoneshwa utambulishi, daktari aliandika alama ya kuuliza.

"Baada ya kurudi nyumbani na matokeo ya daktari, mume wangu alianza vituko , Alianza kuacha kutotoa huduma ya chakula nyumbani.

Na hivyo ugomvi ukawa umeanza".

Mume wake Catherine alikuwa anampigia kelele na kumwambia kuwa katika familia yake hakuna historia ya watoto wa namna hiyo ya kuwa na sehemu ya siri ya kiume na kike, hivyo hakuna namna yeyote ambayo mtoto angekuwa wa kwake.

"Alikuwa anitukana sana na kuniambia kuwa mimi malaya. Nilimuuliza kama mtoto sio wake sasa mtoto ametokea wapi?"

Catherine alisema kwa upole. "Ni mipango ya Mungu."

Mume wake alikataa kwenda tena kliniki na mtoto. Catherine alianza kuona kuwa alikuwa ameachwa kumlea mtoto peke yake na hali hiyo ilikuwa inampa hofu .

Nilijihisi upweke na kuchanganyikiwa. Siku moja nilinunua sumu ya panya ili nijiue mimi pamoja na mtoto, nilichanganya sumu hiyo kwenye chakula na nnakumbuka yalikuwa maharage.

Lakini alijizuia mwenyewe na kukimbilia kanisani kuongea na mchungaji.

Mchungaji alimuhakikishia kuwa hayuko peke yake, kuna watoto wengine ambao wapo duniani kama wa kwake, mtoto wake alikuwa hajalaaniwa.

Aliniambia kuwa maisha yataendelea. Mungu atanibariki mimi pamoja na mtoto na wote tutakuwa salama."

Mwezi mmoja baada ya mtoto wake kuzaliwa, Catherine alifanya maamuzi ya kumuacha mume wake na kurudi kwenda kuishi na familia ya dada yake.

Catherine aliona kuwa amenyanyaswa vya kutosha na sio maisha ambayo alikuwa anayataka kwa ajali yake na mtoto wake.

Wiki kadhaa baada ya kujifungua akiwa hana kipata. Catherine alirudi kufanya kazi katika makazi ya watoto huku akiwa na hofu.

Kitu kimoja ambacho kilikuwa kinamsumbua ni mapendekezo ya mtoto wake kufanyiwa upasuaji ulio salama.

Daktari aliniambia kuwa mtoto wangu ana homoni zake za kiume zina nguvu zaidi ya homoni za kike hivyo upasuaji unapaswa kuondoa uke na kuacha homoni za kiume kufanya kazi ."

Kwa muda mrefu alikataa wazo hilo lakini baada ya mwaka mmoja baada ya kujifungua, alitoa ruhusa upasuaji huo ufanyike kama ni jambo zuri zaidi kwa mtoto wake.

Lakini mara alianza kujuta haraka.

Jambo lingine lilikuwa cheti cha kuzaliwa.

Ili kupata cheti cha kuzaliwa nchini Kenya, jinsia ya mtoto inapaswa kutajwa lakini Catherine alikuwa na fomu ambayo hospitalini waliweka alama ya kuuliza tu ili kubainisha jinsia ya mtoto.

Alama hiyo ya kuuliza ilimaanisha kuwa cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake hakiwezi kutengenezwa au alikuwa hana vigezo vya kupata kadi ya utambulisho au hati ya kusafiria nchini Kenya .

Catherine alifahamu kuwa mtu bila kuwa na nakala hizo , hawezi kumuandikisha mtoto wake shule na mtoto wake akiwa mtu mzima hawezi kuruhusiwa kupiga kura.

Hatimaye aliamua kumwambia mfanyakazi mwenzie jambo ambalo linamsumbua.

Aliamua kumwambia mwanaume ambaye aliona anaweza kumsaidia tatizo lake.

Hivyo ndivyo Catherine alipokutana na John Chigiti.

Mapema mwaka 2010, John Chigiti akawa wakili ambaye anafahamika nchini Kenya kwa kumuwakilisha Richard Muasya, mtu ambaye alikuwa ana jinsia mbili na halinyanyaswa kijinsia gerezani.

Mahakama ilikataa kusikiliza malalamiko ya Muasya na kumuamishia kwenye gereza la wanawake lakini Chigiti alipata umaarufu wa kuweza kuwatetea watu ambao wana jinsia mbili nchini humo , wakati ambapo maoni ya watu yalikuwa ya chuki.

Mtoto kuzaliwa na jinsia mbili ilionekana kuwa ni laana katika familia, na wengi waliuwawa kutokana na imani hiyo.

Catherine alikuwa anataka vitu vitatu, kitambulisho cha kumtambulisha mtoto wake aweze kwenda shule, sheria itakayozuia upasuaji wa kuondoa jinsia moja labda kama kuna ulazima sana na kunatolewa taarifa sahihi na daktari anawasaidia wazazi kwa ushauri.

Chigiti alikubali kuwakilisha malalamiko hayo kwa msaada wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali kijijini hapo.

Taasisi hiyo ya The Cradle the Children ilifungua kesi katika mahakama kuu kabla ya mwaka huo kuisha.

Ili kulinda mtoto wake asitambulike , Catherine alimuita mtoto wake A hivyo kesi iliitwa ni ya mtoto A.

Mwendesha mashtaka mkuu alitoa agizo hospitali ya taifa kuandikisha kuzaliwa na kufa.

Mwaka 2014, mahakama iliagiza mahakama kutoa cheti cha kuzaliwa cha mtoto wa Catherine ambaye alikuwa na miaka mitano.

Na kuongeza kwa kutoa amri kwa mamlaka kuweka mfumo nzuri wa kuwasaidia watoto wenye jinsia mbili.

Mamlaka husika imepeleka mapendekezo yake kwa mwendesha mkuu wa mashtaka.

Mapendekezo yao yalijumuisha ucheleweshwaji wa upasuaji mpaka watoto waweze kuchagua wenyewe jinsia wanayotaka kubaki nayo na vilevile kufanya utafiti wa idadi ya watu wenye jinsia mbili nchini humo.

Suala lingine ambalo lilikuwa kubwa ni kuwa na alama ya I inayowasilisha Intersex' kuweza kuwekwa katika nyaraka zote za umma na kupinga taifa kuainisha kuwa inatambua jinsia ya kike na kiume tu katika nyaraka rasmi."

Nchi kadhaa zimeweza kutambua aina hiyo ya jinsia na inaweza kuandikishwa rasmi katika nyaraka pale ambapo jinsia itakapotambuliwa kiuhakika.

Wabunge wameonekana kuunga mkono mapendekeo hayo na mwaka huu 2019 haki ya watu wa jinsia mbili inaweza kutambuliwa, na kesi ya mtoto A ndio ilileta ushawishi.

Kwa sasa Catherine anaendesha maisha yake kwa kutengeneza na kuuza sabuni. Watu wake wa karibu wanafahamu historia ya kiafya ya mtoto A na inamsaidia.

Catherine amemlea mtoto A kama mvulama na sasa ana umri wa mika 10

Bado anahofu kama alifanya maamuzi sahihi ya kumlea kama mtoto wa kiume lakini hakuwahi kumuuliza namna ya kujiwakilisha kwa watu.

Ana wasiwasi juu ya mtoto wake kwa sababu hapendi kujichanganya na watoto wengine, mara nyingi huwa yuko peke yake

Catherne ana ujumbe kwa wazazi kuwa kama wana watoto ambao wana jinsia mbili wawaache bila kuwafanyia upasuaji mpaka wakikuwa wataamua wenyewe.

Hata ushauri wa madaktari unapaswa kutolewa kwa kuangalia utafiti kwa sababu daktari sio Mungu.