Vladimir Putin na Kim Jong-un waahidi mahusiano thabiti

Vladimir Putinna Kim Jong-unwalikutana Vladivostok

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Vladimir Putinna Kim Jong-unwalikutana Vladivostok

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na rais wa Urusi Vladimir Putin wameahidi kuboresha mahusiano katika mkutano wao wa kwanza kuwahi kufanyika.

Wawili hao walisalimiana kwa mikono katika kisiwa cha Russky karibu na mji wa bandari wa Vladivostok, mashariki mwa Urusi.

Ikulu ya rais wa Urusi ya Kremlin imesema kuwa watajadili mpango wa kuacha matumizi ya nuklia lakini bwana Kim anasemekana pia yuko huko kuomba msaada baada ya mazungumzo na Marekani kutozaa matunda.

Rais wa Marekani Donald Trump na Bwana Kim walikutana Hanoi mapema mwaka huu lakini wakashindwa kufikia mapatano yoyote.

Kiongozi wa Korea Kaskazini alikaribishwa kwa upendo na maafisa wa Urusi alipowasili Jumatano.

Chanzo cha picha, AFP

Bwana Kim alipokelewa kwa burudani ya bendi ya jeshi, kabla ya kuingia ndani ya gari akiongozwa na walinzi wake a,nao wamezoweleka sasa kwa kukimbia kando ya gari lake wakati linapoondoka.

"Nimewasili Urusi kwa moyo wa upendo wa watu wetu, na kama nilivyosema , natumai ziara hii itakuwa ya mafanikio na ya maana," Bwana Kim aliieleza televisheni ya Urusi mapema baada ya kuvuka mpakakatika mji wa Khasan.

"Nimatumaini yangu kuwa wakati wa mazungumzona rais anayeheshimika Putin, nitaweza kujadili kwa kina masuala yanayohusiana na utatuzi wa swala la rasi ya Korea, na kaendeleza mahusiano yetu ."

Kile tunachokifahamu juu ya mkutano:

Kwa mujibu wa msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov, utawala wa Kremlin unaamini mazungumzo yanayohusisha pande sita juu ya Korea kaskazini, ambayo kwa sasa yamekwama, ndio njia inayofaa kuhtatua suala la silaha za nuklia katika rasi ya Korea.

Chanzo cha picha, Reuters

Mazungumzo hayo, yalihyoanza 2003, yanazihusisha Korea mbili pamoja na Uchina , Japan, Urusi na Marekani.

"hakuna njia nyingine inayofaa ya kimataifa kwa sasa ," Bwana Peskov aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.

"Lakini ,kwa upande mwingine, juhudi zinafanywa na nchi nyingine.

Hapa juhudi zote zinafaa ili mradi ziwe ni za azma halisi ya kuachana matumizi ya silaha za nuklia na kutatua tatizo la Korea kaskazini na Korea Kusini."

Kile pande mbili zinachokitaka

Ziara hii inaangaliwa kwa kiasi kikubwa kama fursa kwa Korea Kaskazini kuonyesha kuwa inawashirika wenye nguvu baada ya mazungumzo la Marekani mapema mwaka huu kukwama, anasema mwandishi wa BBC Laura Bicker.

Nchi hiyo imemlaumu waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo kwa kuvunjika kwa mkutano wa Hanoi ya Februri.

Mapema mwezi huu Korea Kaskazini ilidai Bwana Pompeoaondolewe kwenye mazungumzo ya nuklia, ikimushutumu kwa "mazungumzo yasiyo na maana" na kuomba mtu ambaye "ni makini zaidi" achukue nafasi yake.

Mkutano huo pia ni fugrsa kwa Pyongyang kuonyesha kuwa uchumi wake hauitegemei sana Marekani, meongeza mwandishi wetu.

Mpango wa makombora ya Korea kaskazini na nuklia

Wachambuzi wanaamini mkutano huu ni nafasi kwa Urusi kuonyesha kuwa ni muhimu katika mzozo wa rasi ya Korea.

Rais Putin amekuwa akisubiri kwa hamu kukutana na Korea Kaskazini kwa muda. Huku wakati wa kikao baina ya Kim na Trump, Urusi imekuwa ikitengwa.

Utusi kama Marekani na Uchina haijatulia kuiona Korea kazkazini ikiwa taifa lenye nuklia.

Urusi na Korea Kaskazini zina ukaribu kiasi gani?

Wakati wa Vita Baridi, Muungano wa Usovieti Urusi iliimarisha uhusiano wa kijeshi na mahusiano ya kibiashara na washirika wa kikomunisti, Korea Kaskazini ,kwa sababu za fikra na mikakati.

Baada ya Muungano wa Usovieti kuvunjiaka mwaka 1991, mahusiano ya kibiashara na Urusi baada ya ukomunisti ulipingua na Korea Kaskazini ikaitegemea uchina kama mshirika wake mkuu.

Chini ya rais Putin, Urusi imeborekan kiuchumi na mnamo mwaka 2014 alilipa madeni yote ya enzi ya Korea kaskazini chini ya Usovieti hatua iliyoonekana kuwa ni ishara ya utashi mwema.

Huku kiwango cha ushawishi Urusi iliyonao kwa Korea kaskazini leo likiwa ni swala linalojadiliwa , taifa la kikomunisti bado linaangaliwa kama moja ya taifa la kigeni lisilo hatari.

Chanzo cha picha, AFP