Siku ya Malaria Duniani: Malaria ni nini na inaweza vipi kutokomezwa?

Mbu akiimuuma mtu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Malaria husababishwa na mbu aliye na viini vayugonjwa huo

Malaria ni ugonjwa ambao una tiba lakini unaendelea kusababisha vifo vingi duniani.

Ugonjwa huo unaua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili huku visa vipya zaidi ya milioni 200 vikiripotiwa kila mwaka, kwa mujibu wa Data za Shirika la Afya Duniani(WHO).

Katika miongo kadhaa iliyopita juhudi za kupambana na ugonjwa wa malaria ziliimarika, lakini tangu mwaka 2015 juhudi hizo zimeonekana kutetereka.

Ripoti mpya ya WHO kuhusiana na hali ya malaria duniani (iliyotolewa mwaka 2018) inaashiria kuwa viwango vya maambukizi havijashuka kati ya 2015 mwaka 2017.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Malaria inaweza kukingwa na kutibiwa

Aprili 25 ikiwa ni siku ya Malaria duniani, Haya ndio mambo unayostahili kufahamu kuhusu ugonjwa huo:

 • Malaria ni ugonjwa hatari unosababishwa na vimelea aina nne: P. falciparum, P. malariae, P. ovale na P. vivax.
 • Vimelea hao huingizwa ndani ya mwili wa binadamu na mbu wa kike wanaofahamika kama Anopheles wanapomuuma mtu.
 • Ugonjwa huo unaweza kukingwa na pia kutibiwa.
 • Mwaka 2017, kuliripotiwa visa karibu milioni 219 vya ugonjwa wa malaria katika nchi 87 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
 • Inakadiriwa kuwa watu 435,000 walifariki dunia kutokana na malaria mwaka 2017.
 • Afrika inakadiriwa kubeba sehemu kubwa yagharama ya watu walioathiriwa na malaria duniani -mwaka 2017, bara hilo liliripoti 92% ya visa vya malaria na 93% ya vifo vilivyotokana na ugonjwa huo.
 • Inakadiriwa kuwa karibu dola bilioni 3.1 zilitumika kudhibiti na kuangamiza malaria mwaka 2017.

Dalili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Viwango vya juu vya joto mwilini, kuhisi baridi na kuumwa na kichwa ni dalili za kwanza za malaria

Dalili za Malaria -Kupanda kwa joto mwilini, kuumwa na kichwa na kuhisi baridi -hutokea katika kipindi cha kati ya siku 10-15 baada ya kuumwa na mbu anayesababisha malaria.

Huenda mtu asigundue anaugua malaria, lakini hali hiyo isipotibiwa ndani ya saa 24, inaweza ikageuka kuwa ugojwa unaoweza kusababisha kifo.

Nani yuko hatarini?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Watoto waliyo chini ya miaka mitano wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa malaria

Mwaka 2017, karibu nusu ya idadi ya watu duniani walikua katika hatari ya kupata malaria .

Watoto waliyo chini ya miaka tano walikuwa kwenye kundi la watu walikuwa katika hatari ya kupata malaria: Mwaka 2017, walichangia 61% (266,000) ya vifo mwaka huo.

Watu wengine waliyo kwenye hatari ya kupata malaria ambao wamejumuishwa kwenye kundi hilo ni kinamama waja wazito na watu waliyo na mfumo hafifu wa kinga

Ni maeneo yapi yaliyoathiriwa zaidi?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Malaria huathiri sana mataifa ya kusini mwa Sahara lakini pia huatiri baadhi ya mataifa ya Asia na Amerika ya Kusini

Kwa mujibu wa data ziizotolewa na WHO, visa vingi vya malaria na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo hutokea katika maeneo ya kusini mwa Jangwa la shara barani Afrika, lakini maeneo ya kusini mashariki ya bara Asia, Mashariki mwa Mediterrania, Magharibi mwa Pacific, na Amerika pia yamo hatarini.

Mwka 2017, mataifa matano ya barani Afrika yalirekodi karibu nusu ya visa vyote vya ugonjwa wa malatia duniani.

Mataifa hayo ni:

 • Nigeria (25%),
 • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (11%),
 • Mozambique (5%)
 • India (4%)
 • Uganda (4%).

Maambukizi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mbu anayesababisha malaria

Mara nyingi, mtu huambukizwa malaria baada ya kuumwa na mbu aina ya Anopheles anayebeba viini vya ugonjwa huo- kuna zaidi ya mbu 400 wa aina ya Anopheles, na 30 kati yao huabeba viini vinavyosababisha malaria.

Mbu hao huuma watu kati ya jua linapotua hadi nyakati za alfajiri.

Mbu aina ya Anopheles hutaka mayai ndani ya maji, baada ya kuanguliwa huegeuka kuwa mbu wa kike anayeishi kwa kufyonza damu pekee iliwaendelee kutaga mayai.

Kinga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwaka 2017, karibu nusu ya watu waliyokua katika hatari ya kupata malaria barani Afrika walilindwa dhidi ya ugonjwa huo kwa kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa ( Ripoti ya WHO kuhusu Malaria)

WHO linapendekeza watu wote waliyo katika hatari ya kupata malaria wakingwe kwa kutumia mbinu zilizothibitishwa kuwa bora zaidi.

Mbinu mbili za ulinzi ni - kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa(ITN) na kupuliza dawa nda na nje ya nyumba (IRS) -njia hizi zimetajwa kuwa bora zaidi ya kujikinga dhidi ya malaria.

Kulala ndani ya vyandarua vilivyotiw dawa hupunguza uwezo wa mbu kumfikia ntu nyakati za usiku.

Mbinu ya IRS inahusisha kupuliza dawa ndani na nje ya nyumba na mijengo, angalau mara moja au mbilikwa mwaka.

Malaria pia inaweza kupingwa kwa kutumia dawa za kinga malaria hasa wasafiri, kinamama wajawazito na watoto.

Tiba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Utambuzi wa mapema wa dalili za ugonjwa na jinsi ya kutibu

Malaria ina tiba - dalili za ugonjwa huo zinaweza kuthibitishwa katika muda wa dakika 30 baada ya mtu kuambukizwa. Hilo linafanyika baada ya mtu kufanyiwa vipimo maalum.

Kwa mujibu wa Shirika la WHO, ugunduzi wa mapema na tiba ya malaria, hupunguza vifo na pia kupunguza visa vya maambukizi.

Tiba nzuri zaidi inayopatikana ya malaria aina ya P. falciparum, ni mchanganyiko wa dawa aina ya artemisinin inayofahamika kwa kifupi kama (ACT).

Usugu dhidi ya dawa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Vipimo vya damu kubaini viini ya malaria

Shirika la Afya Duniani,WHO limeonya kuwa mbu anayesababisha malaria anaendelea kuwa sugu kwa dawa za kukabiliana na malaria.

Hofu ni kuwa mbinu za kinga zinazotumika sasa huenda zikashindwa kufanya kazi.

Data za hivi punde zilizotolewa katika ripoti ya dunia kuhusu ugonjwa malaria zinaashiria kuwa nchi 68 zimeripotiwa kuwa na mbu ambao ni suu kwa angalau moja kati ya dawa tano zilizotumika kati ya mwaka 2010-2017.

Usugu wa dawa za kukabiliana na malaria pia ni tatizo linaloendelea kuwa changamoto kwa wanasayansi.

WHO linasema kuwa dawa imara ni muhimu katika juhudi za kuangamiza ugonjwa wa malaria duniani.

Lengo likiwa ni kuhakikisha usugu wowote wa dawa unagunduliwa haraka iwezekanavyo.