Wamuoza binti yao wa 'miaka mitano' kwa dola 3,500

A man's hand giving Afghan currency to another

Nazanin alichumbiwa akiwa na miaka mitano na alipofikisha mika kumi alikua mke wa mtu.

Familia ya mume wake wa miaka 12 ilimnunua kwa dola 3,500 miaka sita iliyopita.

Wazazi wake walimuuza ili wapate pesa za kugharamia matibabu ya ndugu yake, Nazanin.

"Baba yake Nazanin hakutaka kupokea pesa hizo lakini hakua na budi" anasema mama yake, ambaye anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Shahrak e Sabz karibu na Herat magharibi ya Afghanistan.

Wazazi wa Nazanin wana watoto saba -wasichana watatu na wavulana wanne. Hawana kisomo, hawan pesa wala kazi.

BBC ilizungumza nao ili kufahamu kwanini waliamua kumuuza binti yao mdogo.

Illustration of Nazanin and her brother

Majuto

"Kijana wetu amekua akiugua maradhi ya kifafa tangu alipofikisha miaka minne na hatukua na hela za kugharamia matibabu yake," anasema baba yake Nazanin.

Katika harakati ya kuokoa maisha ya mtoto wao wa kiume familia ailiamua kumuoza binti yao mkubwa.

"Nilikubali kumuoza binti yangu Nazanin na kutumia pesa za mahari nilizopata kumtibu mwanangu wa kiume.

Lakini hakupona, ilihali nimempeana binti yangu," alisema mama yake.

"Mtu anapomuuza binti yake mdogo bilashaka atakuja kujutia hatua hiyo baadae. Mimi pia najuta, lakini nitafanya nini," baba yake aliingilia.

An illustration depicting a wedding cake with a miniature boy and girl sitting on it, surrounded by ten candles

Ndoa za utotoni

Nchini Afghanistan, umri wa kisheria wa wasichana kuolewa ni miaka 16, na wavulana ni miaka 18. Lakini wengi wanaozwa au kuolewa wakiwa chini ya miaka hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Unicef ya mwaka 2018, 35% ya wasichana nchini Afghanistan huolewa kabla wafikishe miaka 18, na 9% huolewa kabla wafikishe miaka 15.

'Mahari'

Afghanistan imekabilia wa miongo kadhaa ya mapigano na ukame wa hivi karibuni umeziacha familia nyingi na matumaini madogo ya kupata ajira.

Kulipisha 'mahari' ni sehemu ya utamaduni wa Waafghanistan nahaimbatani na sheri aya dini ya Kislamu, kwa mujibu wa Faizal Muzhary, mtafiti wa masuala ya kijamii nchini Afghanistan.

Illustration of Nazanin

Ukame

Familia ya Nazanin iliathiriwa vibaya na ukame uliyokumba Afghanistan mwaka 2018.

"Tulikua tukifanya kazi mashambani mwetu na pia tulikua na mifugo. Lakini tulilazimika kuacha kila kitu," anasema baba yake.

"Binti zangu ndio mali pekee niliyo nayo." aliongeza.

An illustration showing a dead cow and a family forced to move away

Ndoa

Baada ya familia kulemewa na shida zilamua kuwaoza babinti zao wadogo ili kikidhi mahitaji yao.

Mwaka jana Nazanin alipotimiza umri wa miaka 10, familia yake ilifanya harusi yake ambayo ilihudhuriwa na watu 100.

"Nilimpatia nbinti yangu kile nilichoweza. Pesa za mahari tulizopokea hazikutosha," anasema baba yake.

"Laiti sio shida, huwezi kukubali kumuoza mtoto mdogo hivi. Kwa kweli singefanya hivyo, lakini nilihitaji pesa. Nililazimishwa na mahitaji yangu," aliongeza baba yake.

"Utafanya nini? Hii ndio njia pekee niliyokua nayo. Si mimi peke yangu - Watu wengine wengi wamefanya hivyo kutokana na matatizo ya kiuchumi."

Illustration showing Nazanin leaving her family home

Makundi hatarishi

Utafiti uliyofanywa mwaka 2015 na Baraza la Wakimbizi la Norway unasema kuwa wasichana wanaoishi maeneo ya mijini wako katika hatariya kuozwa mapema kwa wanaume wakubwa ambao wanauwezo wa kulipa 'mahari'.

Lakini Nazanin, amabye sasa ana miaka 11, hakuozwa kwa mwanamume mtu mzima - pengine, walimuonea huruma.

"Aliishi kwa wakwe zake kwa miezi miwili. Walimchukulia kama binti yao. Mume wake anakaribia miaka 12. Ni mhaya na hapendi kuzungumza sana," anasema mama yake.

Nakuna idhini

Nazanin hakushauriwa kuhusiana na harusi yake. Wazazi pia hawakumueleza binti yao majukumu yanayohusiana na maisha ya ndoa, lakini Nazanin alijizatiti kuyatekeleza majukumu hayo.

"Tuliwaomba wakwe zetu wamruhusi binti yetu aishi na sisi kwa miaka michache," anasema mam yake .

Nazanin amerudi kwa zazi wake lakini wakwe zake wameahidi kumchukua baada ya miaka miwili au mitatu atakapokuwa kidogo.

"Wanaishi mkoa wa Nimruz. Siku kumi zilizopita mume wake alikuja kuishi nasi kwa siku kadhaa," baba yake alisema.

Ongezeko la ndoa za utotoni

Unicef imegundua madanguro 161 yanayendesha ndoa za watoto mjini Herat na Badghis kati ya Julai na Oktoba mwaka jana. kati ya hizo, 155 walikua watoto wakischana na wavulana sita.

"Ndoa za utotoni zimekita mizizi katika baadhi ya maendo nchini humu. Hali hiyo imechangiwa na vita na ukame," anasema mkuu wa Unicef mawasiliano nchini Afghanistan, Alison Parker.

An illustration showing Nazanin and two wedding rings

"Kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba kulikua na ongezeko kubwa la ndo za utotoni. Lakini tangu wakati huo serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na ndoa hizo.''

Serikali ya Afghanistan inapania kutokomeza ndoa za utotoni kufikia mwaka 2021.

Mswada wa sheria umewasilishwa bungeni ili kuongeza miaka ya wasichana kuolewa hadi 18.

Msaada

Mashirika ya kuto misaada yanajaribu Aid agencies are trying to restore the livelihoods of the displaced people. The UN's Food and Agricultural Organization is distributing free seeds to restart farming operations in many provinces.

"Miongo minne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe imeharibu kabisa misingi ya kijamii nchini. Katika maeneo mengi ya nchi wakaazi wa vijijini hawana uwezo wakupata mikopo. Hali ni ngumu na hakuna mtu yeyote anataka kuwekeza," anasema afisa wa kulinda maslahi ya watoto katika shirika Unicef, Alfred Mutiti.

"Nyingi ya familia zilizofurushwa makwao zimejipata na katika lindi la madeni na haziwezi kulipa mikopo.

Hata zikipewa pesa haziwezi kusaidia, ni kama tone nane la maji ndani ya bahari" anasema Alfred Mutiti.

Mwerevu

Katika kambi ya wakimbizi ambako, familia ya Nazanin bado inasubiri kupata msaada kutoka kwa serikali au mashirika ya misaada.

Kitu cha thamani zaidi ambachokinapatikana hapo ni nafasi ya kusoma.

Wazazi wake wake wanajivunia kuwa msichana wao mkubwa anaweza kuandika jina lake na baba yake.

"Nazanin ni mtoto mwerevu. anajua kusoma herufi zote," anasema mama yake.

Ndugu zake wwili pia wanasoma shule.

Kuishi kwa matumaini

Lakini fmilia hiyo bado haijakaribia kupata furaha na inasema kuwa haina mtu wa kuisaidia. Hali ambayo haijamridhisha bi harusi mdogo.

"Nazanin aliniambia : 'Mama, ulinioza nikiwa mdogo lakini ndugu yangu hakupona.' Lakini pia anasema, 'Ndugu yangu atapona na mimi pia nitakuwa mkubwa.' Najua kumuoza akiwa mdogo lakini, lakini nina matumaini kuwa maisha yatakua mazuri siku za usoni,"anasema mama yake.

(Jina la Nazaninlimebadilishwa ili kumlinda asitambulike)

michoro ya Jilla Dastmalchi

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii