Kimbunga Kenneth: Kinaweza kurudia kupiga tena Msumbiji

A large downed tree in Comoros Haki miliki ya picha AFP

Kimbunga Kenneth tayari kimefanya uharibifu kaskazini mwa Msumbiji, huku bado nchi hiyo inatarajia dhoruba nyingine kubwa.

Kimbunga hicho kimepungua katika saa chache zilizopita lakini utabibiri wa hali ya hewa unategemea kuwa kutakuwa na mvua kubwa ambayo itasababisha mafuriko.

Idara ya kuthibiti majanga nchini Msumbiji imesema watu elfu thelathini wamehamishwa katika makazi yao ambapo dhoruba la kimbunga linaweza kupiga tena.

Mwezi uliopita Kimbunga Idai kilisababisha vifo vya mamia ya watu nchini humo.

Haki miliki ya picha Reuters

Watu zaidi ya 900 walikufa wakati ambapo mvua kubwa ilipopiga maeneo ya Mozambique, Malawi na Zimbabwe.

Watu wapatao milioni tatu walikuwa wanapata msaada wa kibinadamu.

Utabiri wa hali ya hewa unatarajia kimbunga kupiga tena eneo la Idai.

Jambo gani jipya?

Kimbunga Kenneth kilipiga kwa kasi kubwa ya upepo wenye kasi ya kilimota 220 kwa saa sawa na tufani ya awamu ya nne na kuwasili kaskazini mwa Pemba.

Shughuli za uokoaji wa lazima kwa familia unafanyika na utaendelea kufanyika mpaka watu wote wafikishwe kwenye eneo salama.

Watu zaidi ya 680,000 wapo hatarini na kimbunga, afisa mmoja wa utawala nchini Msumbiji aeleza.

Mamlaka ya hali ya hewa ilitoa tahadhari juu ya mvua kubwa katika eneo hilo kwa siku kadhaa.

Haki miliki ya picha AFP

Safari za ndege zimesitishwa tayari na shule zimefungwa nchini Msumbiji kwa kuhofia dhoruba hiyo kupiga.

Wakazi wa kusini mwa Tanzania katika mkoa wa Mtwara walitengewa eneo maalum kwa ajili ya kujikinga lakini tahadhari hiyo imesitishwa na watu wamerudi katika makazi yao.

Njia ya kimbunga imebadilika kusini, hii ikiwa ina maana kuwa janga kubwa halitarajiwi tena eneo hilo na ndio maana wamewaruhusu watu waendelee na shughuli zao za kawaida, Kamishna wa kikanda Gelasius Byakanwa aliwaambia waandishi wa habari.

Image caption Wananchi wa Mtwara, Tanzania wakirejea katika makazi mara baada ya kutangaziwa kuwa njia ya kimbunga imebadilika

Kimbunga Keneth kimepiga kisiwa cha Comoro kwa mvua kubwa na upepo na mamlaka ya nchi hiyo imesema watu wapatao watatu wameuwawa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii