Mkutano wa Korea Kaskazini : Kim aishutumu Marekani kwa 'kupotosha ukweli' kuhusu mpango wa nyuklia

Huwezi kusikiliza tena
Putin and Kim toast at the summit in Vladivostok

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameishutumu marekani kwa "kupotosha ukweli" wakati wa mkutano mapema wiki hii na rais Donald Trump, kwa mujibu wa shirika la habari la Korea -Korea Central News Agency.

Amesema pia kwamba amani katika rasi ya Korea itategemea utawala wa Washington.

Bwana Kim aliitoa kauli yake katika mkutano wa Alhamisi na rais wa Urusi Vladimir Putin katika mji wa Vladivostok.

Rais Putin alikubali mwaliko wa kuizuru Korea Kaskazini, KCNA limeripoti

Ziara hiyo itafanyika "katika wakati unaofaa ," shirika hilo la habari limeongeza kusema.

Kim Jong-un anaripotiwa kumwambia Vladimir Putin kwamba "hali katika rasi ya Korea peninsula na kanda hiyo kwa ujumla tete na imefikia wakati mgumu".

Alionya kuwa hali "inaweza kurejea mahali ilipokuwa kwasababu Marekani imeamua kuchukua mkondo wa ''kupotosha ukweli " wakati wa mazungumzo ya hivi karibuni.

Hii inakuja wiki moja baada ya Pyongyang kuishutumu Marekani kuvuruga mazungumzo ya amani.

Mazungumzo baina ya nchi mbili yalivujika wakati wa kikao cha Vietnam mwezi Februari, bila kufikiwa kwa mkataba juu ya silaha za nuklia za Korea kaskazini .

Mazungumzo hayo yaliripotiwa kukwama kutokana na madai ya Korea Kaskazini kudai kuondolewa vikwazo kamili vya kiuchumi ndio iweze kuahidi kuachana na silaha hizo - mkataba ambao Marekani haiko tayari kuukubali.

Haki miliki ya picha AFP

Kwa mujibu wa msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov, utawala wa Kremlin unaamini mazungumzo yanayohusisha pande sita juu ya Korea kaskazini, ambayo kwa sasa yamekwama, ndio njia inayofaa kuhtatua suala la silaha za nuklia katika rasi ya Korea.

Mazungumzo hayo, yalihyoanza 2003, yanazihusisha Korea mbili pamoja na Uchina , Japan, Urusi na Marekani.

"hakuna njia nyingine inayofaa ya kimataifa kwa sasa ," Bwana Peskov aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.

"Lakini ,kwa upande mwingine, juhudi zinafanywa na nchi nyingine.

Hapa juhudi zote zinafaa ili mradi ziwe ni za azma halisi ya kuachana matumizi ya silaha za nuklia na kutatua tatizo la Korea kaskazini na Korea Kusini.

Haki miliki ya picha AFP

Ziara hii inaangaliwa kwa kiasi kikubwa kama fursa kwa Korea Kaskazini kuonyesha kuwa inawashirika wenye nguvu baada ya mazungumzo la Marekani mapema mwaka huu kukwama, anasema mwandishi wa BBC Laura Bicker.

Nchi hiyo imemlaumu waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo kwa kuvunjika kwa mkutano wa Hanoi ya Februri.

Mapema mwezi huu Korea Kaskazini ilidai Bwana Pompeo aondolewe kwenye mazungumzo ya nuklia, ikimushutumu kwa "mazungumzo yasiyo na maana" na kuomba mtu ambaye "ni makini zaidi" achukue nafasi yake.

Mkutano huo pia ni fugrsa kwa Pyongyang kuonyesha kuwa uchumi wake hauitegemei sana Marekani, meongeza mwandishi wetu.

Mpango wa makombora ya Korea kaskazini na nuklia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vladimir Putinna Kim Jong-un walikutana Vladivostok

Wachambuzi wanaamini mkutano huu ni nafasi kwa Urusi kuonyesha kuwa ni muhimu katika mzozo wa rasi ya Korea.

Rais Putin amekuwa akisubiri kwa hamu kukutana na Korea Kaskazini kwa muda. Huku wakati wa kikao baina ya Kim na Trump, Urusi imekuwa ikitengwa.

Utusi kama Marekani na Uchina haijatulia kuiona Korea kazkazini ikiwa taifa lenye nuklia.

Urusi na Korea Kaskazini zina ukaribu kiasi gani?

Haki miliki ya picha Reuters

Wakati wa Vita Baridi, Muungano wa Usovieti Urusi iliimarisha uhusiano wa kijeshi na mahusiano ya kibiashara na washirika wa kikomunisti, Korea Kaskazini ,kwa sababu za fikra na mikakati.

Baada ya Muungano wa Usovieti kuvunjiaka mwaka 1991, mahusiano ya kibiashara na Urusi baada ya ukomunisti ulipingua na Korea Kaskazini ikaitegemea uchina kama mshirika wake mkuu.

Chini ya rais Putin, Urusi imeborekan kiuchumi na mnamo mwaka 2014 alilipa madeni yote ya enzi ya Korea kaskazini chini ya Usovieti hatua iliyoonekana kuwa ni ishara ya utashi mwema.

Huku kiwango cha ushawishi Urusi iliyonao kwa Korea kaskazini leo likiwa ni swala linalojadiliwa , taifa la kikomunisti bado linaangaliwa kama moja ya taifa la kigeni lisilo hatari.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii