Kimbunga Kenneth: Waokoaji wahangaika kufikia vijiji vilivyoathiriwa

Kuna hofu kuwa maelfu ya watu wamekwama huku mvua kubwa na upepo vikihofiwa kusababisha hatari ya mafuriko na maporomoko zaidi ya ardhi
Image caption Kuna hofu kuwa maelfu ya watu wamekwama huku mvua kubwa na upepo vikihofiwa kusababisha hatari ya mafuriko na maporomoko zaidi ya ardhi

Wahudumu wa uokozi wanajaribu kufika katika vijiji visivyoweza kufikiwa kwa urahisi ambako kimbunga kikubwa kimesababisha maafa makubwa.

Kuna hofu kuwa maelfu ya watu wamekwama huku mvua kubwa na upepo vikihofiwa kusababisha hatari ya mafuriko na maporomoko zaidi ya ardhi.

Kimbunga Kenneth kipipiga nchi ya Msumbiji tangu siku ya Alhamisi kikiwa na kasi ya kilomita 220 kwa saa , na kimekuja karibu mwezi mmoja baada ya kimbunga Idai kuwauwa watu zaidi ya 900 katika nchi tatu.

Katibu mkuu wa shirika la msaada la kimataifa Amnesty International Kumi Naidoo alisema kuwa vimbunga hivyo viwili ni matokeo ya ,mabadiliko ya tabia nchi kama yalivyotangazwa na wanasayansi walioonya kuwa vimbunga vya aina hiyo vitatokea iwapo wakazi wa dunia wataendelea kuharibu mazingira kupita kiasi ".

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maafisa wanatathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga Kenneth kaskazini mwa Msumbiji

" Kuna mambo tusiyoweza kuyakwepa na ukosefu wa haki ambao hatuwezi kuusisitizia vya kutosha ," alisema na kuongeza kuwa : " Watu wa msumbiji wanalipia gharama yya mabadiliko hatari ya tabia nchi wakati hawajafanya lolote la kusababisha tatizo hili ."

Maelfu ya nyumba zimeporomoka, huku mifumo ya umeme ikiharibika na maeneo ya mabonde yamefukumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na droruba.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Familia zilizosambaratishwa na kimbunga Kenneth nchini Msumbiji

Mwandishi wa BBC Pumza anasema kuwa uharibifu wa mifumo ya umeme katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji umefanya mawasiliano kuwa magumu.

Takribani watu 20,000 wamepelekwa kwenye makazi ya muda ya mahema kwenye vituo vya watu waliosambaratishwa na mafuriko, zikiwemo shule na makanisa, anasema mwandishi wetu.

Kimbunga Kenneth kilikuwa tayari kimewauwa watu watatu katika nchi jirani ya visiwa vya Comoro na walau mtu mmoja ameripotiw akufa nchini Msumbiji baada ya kuangukiwa na mti.

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na lile la Red Crescent Societies yalishirikisha umma uharibifu ulipotokea kupitia mitandao ya kijamii. katika ujumbe huu wa Tweeter , kikundi cha wahudumu wa kujitolea kilionekana na kuthibitisha kuwa kinatoa msaada kw awaathiriwa.

Je maeneo yalioathirika yakoje?

Mkoa wa Cabo Delgado hauna watu wengi kama ulivyokuwa kabla ya kimbunga Idai, na kuna maeneo mengi ya juu katika eneo hilo.

Mbali na onyo lililotolewa na mamlaka kabla ya, kimbunga hicho kinaweza kusababisha maafa makubwa zaidi ya Idai.

Lakini ripoti zimesema kuwa maelfu ya makaazi yameharibiwa na upepo huo huku eneo hilo likishuhudia ghasia za wapiganaji katika miezi ya hivi karibuni.

Maelfu ya wakaazi wametoroka makaazi yao ili kutafuta hifadhi kutoka katika kambi za ghasia za watu walioachwa bila makao.

Kimbunga Kenneth 'kuzikumba Msumbiji, Tanzania Alhamisi'

Na je mataifa mengine katika eneo hilo

Taifa la Comoro bado linajikwamua kutoka katika uhairibifu uliosababishwa na kimbunga hicho ,ambacho kilipigwa na upepo mkali na mvua kubwa.

Upepo umesababisha ukosefu wa umeme na uharibifu katika nyumba.

Katika maeneo mengine ya kusini yanayopakana na taifa jirani la Tanzania , mamlaka zimeagiza shule na biashara kufungwa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kimbunga Kenneth tayari kimeathiri maeneo kadhaa ya visiwa vya Comoros

Licha ya Zimbabwe kuwa ndani , ya nchi kavu , maafisa wanasema kuwa wanaweka maafisa wao waliopo katika idara ya dharura katika hali ya tahadhari.

''Kutokana na Kimbunga Idai hatuwezi tena kuruhusu hali kuendelea bila kutoa tahadhari yoyote'', alisema mkurugenzi wa idara ya ulinzi wa raia Nathan Nkomo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii