Uchaguzi Benin: Vyama vya upinzani vyafungiwa kwa kutokufikia sheria mapya ya uchaguzi

Benin imekuwa ikisifika kwa kuwa nchi inayozingatia utawala wa Kidemokrasia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Benin imekuwa ikisifika kwa kuwa nchi inayozingatia utawala wa Kidemokrasia

Wanainchi wa Benin wanashiriki uchaguzi wa wabunge wapya bila wagombea wa upinzani.

Tume ya uchaguzi mwezi uliyopita uliviidhinisha vyama viwili vay kisiasa vinavyodaiwa kumuunga mkono rais Patrice Talon - kushiriki uchaguzi huo baada ya kufukia masharti yaliyowekwa.

Sheria mpya ya uchaguzi ilizitaka vyama kulipa ada ya dola 424,000 ili viruhusiwe kushiriki uchaguzi huo.

Huduma ya intaneti zimedhibitiwa huku mitandao ya kijamii na huduma ya kutuma na kupokea ujumbe mfupi zikifungwa katika taifa hilo lla Afrika Magharibi.

Wapiga kura milioni tano wamesajiliwa kushiriki zoezi hilo katika taifa linalojivunia kuwa na utawal thabiti wa kidemokrasia.

'Hatua inayoweza kuzua ghasia'

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamekosoa hatua ya kuzuiliwa kwa maandamano ya amani na kukamtwa kwa wanaharakati wa upinzani wanaolalamikia hatua ya upinzani kufungiwa uchaguzi huo.

"kuongezeka kwa visa vya kukamatwa na kuzuiliwa kwa wapinzani huenda kukazua ghasia nchini humo," François Patuel, kutoka shirika la Amnesty International, alisema katika taarifa yake.

"Kupiga marufuku maandamano ya amani na kuwakamata na kuwazuiliawale wanaopinga hatua ya upinzani kufungiwa nje ya uchaguzi kutazua hali ya mtafaruku."

Wiki iliyopita, vikosi vya usalama viliwarushia vitoza machozi marais wa zamani wa nchi hiyo- Nicéphore Soglo na Thomas Boni Yayi - walipokua wakiwahutubia waandamanaji kuhusu suala la uchaguzi katika mji wa Cotonou.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Talon, aliingia madarakani mwaka 2016

Mfumo wa siasa ya vyama vingi ilibuniwa miaka mitano iliyopita nchini Benin, na uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo huo ulifanyika miaka ya 1990, ambapo vyama 20 viligombania viti 83 vya ubunge, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la AFP.

Rais Talon, ambaye ni mfanyibiashara wa zamani aliyejulikana kama "mfalme wa pamba", aliingia madarakani mwaka 2016.

Anasema marekebisho ya sheria ya uchaguzi yanalenga kuleta pamoja mamia ya vyama vya upinzani vilivyo na falsafa aina moja kwa lengo la kuimarisha mfumo wa siasa ya vyama vingi.

Bw Talon pia alitia saini sheria ya kuwazuia wafanyikazi wa afya na wafanyikazi wengine wa serikali kugoma kwa zaidi ya siku 10.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mamia ya waendesha piki piki waijitokeza kusikiliza houba ya marais wawili wa zamani waliyokua wakishinikiza kucheleweshwa kwa uchaguzi

Wanahabari wanasema watu wengi walitarajia kuwa uchaguzi huo utaahirishwa ili kuvipatia vyama vya upinzani muda wa kufikia masharti mapya ya uchaguzi.

Lakini katika hotuba yake kwa taifa Aprili 11, rais Talon alisema kuwa hana mamlaka ya kuingilia machakato wa uchaguzi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii