Tanzania: Dawa za kuongeza nguvu za kiume zatambuliwa na serikali

Dawa za kiume za vidonge maarufu, Viagra
Image caption Dawa za kuoneza nguvu za kiume za vidonge maarufu Viagra

Serikali ya Tanzania imekiri kuwepo kwa dawa ya kuongeza nguvu za kiume ambayo haina kemikali, ingawa haijatangazwa rasmi.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Hussein Mwinyi amethibitisha hilo leo, bungeni wakati akijibu maswali ya nyongeza.

"Sababu za watu kupungukiwa nguvu za kiume ziko nyingi ikiwemo ugonjwa wa kisukari na msongo wa mawazo, lakini vilevile serikali tayari imeshabaini uwepo wa dawa kwa ajili ya wanaume ambazo hazina kemikali" Dkt. Mwinyi ambaye ni tabibu kitaaluma ameeleza.

Image caption Dawa za nguvu za kiume

Aidha waziri huyo ameonya matumizi ya dawa ambazo hazijafanyiwa utafiti kwa sababu si salama kwa matumizi.

Na kuhusu dawa za kuongeza maumbile ya uume, Dkt. Mwinyi amesema zipo taarifa nyingi za aina hiyo, lakini jambo jema ni kuongeza uelewa wa wananchi ili kutumia dawa zilizothibitishwa.

Mapema mwaka jana baraza la dawa nchini humo lilitangaza dawa za asili zilizothibitiswa kwa ajili ya matumizi ya kuongeza nguvu za kiume.

Hatua ya uthibitisho ilikuja baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na kubaini kuwa dawa hizo hazina madhara kwa afya ya binadamu hivyo hawana budi kuzikubali.

Paul Muhame ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa dawa za asili nchini Tanzania anasema baada ya baraza kupitisha vigezo vyote vilivyohitajika kutoka katika dawa hizo na mamlaka ya dawa na chakula kuthibitisha hilo.

"Suala la muhimu ambalo tumeliangalia zaidi ni usalama wa mtumiaji lakini katika upande wa kuthibitisha kuwa dawa hizo zinaponyesha au la, linabaki kwa mnunuaji na mtumiaji wa dawa hiyo" Makame alisisitiza.

Je, kuna madhara wanaume wanapoongeza uume

Sindano za kuimarisha uume ambazo zimebuniwa kuongeza ukubwa wa uume zimepata umaarufu mkubwa licha ya tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa kuhusu madhara ambayo yanaweza kujitokeza mtu anapotumia dawa hizo.

Imani potofu juu ya uume mkubwa

Utafiti wa mwaka 2015 uliofanywa katika chuo kimoja mjini London iliangalia urefu na upana wa uume kwa wanaume zaidi ya 15,000 duniani kote.

Kitaalamu uume unapaswa kuwa na inchi 5.1 yaani sentimita 13 wakati unaposimama.

Ni 5% peke yake ya wanaume ndio walikuwa na uume wa urefu wa zaidi ya inchi 6.3, wakati 0.14% wakiwa na uume mdogo sana kuliko kawaida ambao ni wa urefu wa chini ya inchi tatu ukisimama.

Kwa upande wa kipimo cha mzingo cha uume (ukubwa wake kwa kuangalia mzunguko ambacho ni kipimo cha kukadiria upana wake), kiwango cha kawaida huwa inchi 3.6 (sentimita 9) ukiwa haujasimama, na inchi 4.6 uume unaposimama.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii