Msumbiji: Athari za Kimbunga Kenneth kwa Picha

Mwanamke Mjini Macomia, Kaskazini mwa Msumbiji anatazama uharibifu baada ya mbuyu kuangukia nyumba yake wakati wa lkimbunga Kenneth
Maelezo ya picha,

Mwanamke Mjini Macomia, Kaskazini mwa Msumbiji anatazama uharibifu baada ya mbuyu kuangukia nyumba yake wakati wa lkimbunga Kenneth

Kimbunga kikali kimeharibu maelfu ya nyumba na kuwaua makumi ya raia nchini Msumbiji.

Kimbunga Kenneth kiliwasili siku ya Alhamisi kikiwa upepo wenye kasi wa kilomita 220 kwa saa

Imetabiriwa kwamba hali ya hewa nchini humo itasababisha mvua kubwa zaidi ya ile iliojiri baada ya kimbunga Idai Idai, ambacho kilisababisha zaidi ya watu 900 kupoteza maisha yao katika mataifa ya Msumbiji , Malawi na Zimbabwe mwezi uliopita.

Maelezo ya picha,

Athari za Kimbunga kenneth zinaonekana katika wilaya ya macomia , mkoa wa Cabo Delgado Msumbiji

Pemba, mji mkuu wa jimbo la Cabo Delgado limepata mvua yenye kiwango cha zaidi ya milimita 2 na kusababisha barabara kuwa mito.

Maelezo ya picha,

Mwanamke anavuka barabara iliojaa maji kufutaia athari za kimbunga Kenneth, katika eneo la Pemba , Msumbiji

Maelezo ya picha,

Mwanamume anamsaidia mwanamke kupita katika mafuriko katika eneo la Pemba Msumbiji

Maelezo ya picha,

Mwanamume anatembea karibu na nyumba zilizoharibiwa na mafuriko huko Pemba Msumbiji

hatari hiyo ya mafuriko ilisababishwa na kimbunga Kenneth kilichopiga eneo hilo mwisho wa msimu wa mvua wakati ambapo mito ilikuwa imejaa maji , kulingana na afisi ya Umoja wa mataifa inyosimamia maswala ya kibinaadamu (Ocha) .

Maelezo ya picha,

Wakaazi wanatazama maafisa wa zimamoto katika eneo la Mazive, kusini mwa Msumbiji

Mafuriko yamesababisha uharibifu wa miundo msingi na kuzuia usambazaji wa misaada .

Maelezo ya picha,

Wakaazi wamesimama karibu na barabara ilioharibiwa upande mmoja kufuatia mvua kubwa iliosababisha mafuriko

Kimbunga Kenneth tayari kimefanya uharibifu katika taifa la kisiwani la Comoros

Maelezo ya picha,

Watu wamesimama karibu na nyumba zilizoharibiwa na miti ilioanguka baada ya kimbunga Kenneth kupiga Comoros

Msemaji wa Ocha Saviano Abreu alisema kuwa hali katika miji ya Macomia na Quissanga ilikuwa mbaya, akiongezea kuwa kulikuwa na wasiwasi katika kisiwa cha Ibo kilichozungukwa na maji.

Maelezo ya picha,

Picha za Setlaiti zinaonyesha Kimbunga Kenneth kusini mwa Msumbiji

.