Kujitoa Uhai: Uchungu wa wale wanaowachwa nyuma Nyandarua Kenya

Ugonjwa wa Sonona unawafanya wanaume wengi kujiua kaunti ya Nyandarua Kenya

Idadi ya watu walioripotiwa kujiua inashtua, inawezekana matukio haya yametokea kwa bahati mbaya au ni ushirikina, bado limebaki kuwa jambo linaloshangaza.

Kwa Kenya simulizi za namna hii, ni nadra sana kuziona kwa sababu kipaumbele huwa kinatolewa kwa taarifa za mauaji lakini suala la mtu kujiua si rahisi taarifa hiyo ukute imeandikwa au kutangazwa kwenye vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwaka jana watu 70 walijiua wenyewe katika nchi ya Kenya. Na karibu watu wote walikuwa wanaume.

Katika kijiji cha Shamata, Mkoa wa Kati Kenya kwa mara ya tatu wiki hii afisa wa polisi Bi Wanja amekuwa akiitwa katika maeneo mbalimbali ya watu waliojiua.

Afisa huyo aliwataka wale waliokuwa wameuzunguka mwili wa marehemu kuufinika kabla ndugu zake hawajafika.

Aliyejiua alikuwa anaitwa Francis. Kabla Francis hajaondolewa, jirani mmoja alimwambia polisi huyo namna ambavyo waliupata mwili wa marehemu.

Polisi huyo aliuliza ni wakati gani ambapo mtoto aliingia chumbani? Naye jirani mwengine alimjibu kwamba hakuingia chumbani kwa kuwa Mlango ulikuwa umefungwa hivyo alichungulia dirishani.

Maelezo ya video,

Kujitoa Uhai: Uchungu wa wale wanaowachwa nyuma Nyandarua Kenya

''Hapo ndipo alipoanza kupiga kelele kuita baba amejining'iniza mwenyewe''.

Kwa mujibu wa rafikiye marehemu kijana huy alijiua mwenyewe kwa sababu alikuwa muathirika wa virusi vya ukimwi. Anasema kwamba alijaribu mara nyingi kujiua.

''Nadhani alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu alikuwa ni mtu ambaye hawezi kuishi bila kunywa pombe.Yani alikuwa hawezi kabisa''.

Kulingana na Chifu wa eneo la Shamata bwana Joseph Mathenge kisa hicho ndio cha hivi karibuni kutokea katika tatizo ambalo linazidi kuwa nyeti.

Nyandarua ni miongoni mwa maeneo yaliopo pembezoni nchini Kenya. Kiwango cha umaskini ni kikubwa kuliko maeneo mengine.

Hii inaweza kupelekea kiwango cha watu kujiua kuwa kikubwa. Kama tukiangalia miaka kumi iliyopita kulikuwa na vifo vingi vya watu kujiua wenyewe nchini.Na sasa vimeongezeka kwa kiwango kikubwa sana.

''Tunapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kupata suluhu ya tatizo lililopo'', alisema chifu wa Shamata

lakini ni kwa nini watu wetu wanafikia hatua ya kujiua wenyewe?

Tunadhani tatizo ni nini? Nilishtuka sana niliposikia kuwa mtu wa mwisho kuripotiwa kujiua alifanya jaribio hilo mara kadhaa.

Walipomuuliza kwa nini alitaka kujiua , alikata kuzungumzia matatizo yake.

''Sisi wanaume huwa tunabeba matatizo yetu wenyewe na tunapoulizwa huwa tunasema 'acha nife na matatizo yangu'. Hilo ndilo tatizo''.

''Wanaume huwa wanakumbana na matatizo mengi lakini hawana ambapo huwa wanaweza kwenda kusikilizwa.Tunapokutana kama hivi ,huwa tunapenda kuongelea zaidi siasa''.

''Tunapobishana , ninataka kuonyesha kuwa mimi ninajua zaidi siasa. Lakini sisi kama wanaume huwa tunashindwa kuona kuwa kuna kitu ambacho hakiendi sawa kwake.

''Kwa mfano, mara nyingine mke wangu huwa anakuwa mkali sana kwangu mpaka inafikia hatua ambayo hata nikijaribu kuongea naye hataki hata kunisikiliza'',alisema mwana kijiji wa tatu..

''Hivyo ni vyema wakati tunapoongea na wanaume, tuongee na wanawake pia kwa sababu wao ndio huwa wanatupa msongo wa mawazo sana'', aliongezea.

Wakati tulipokuwa tukipiga picha maeneo ya Shamata, Polisi walituambia kuwa kuna mtu mwingine amejiua kilomita 15 kutoka eneo tulilopo upande wa kaskazini.

Joseph ambaye ni ndugu wa mwathiriwa anasema kuwa alipigiwa simu alfajiri na alipowasili alimpata nduguye ananinginia kutoka kwa mti.

Sijui cha kusema kwa sababu nimeona watu wengi wakipata sonona, lakini hawaonekani kama wanaumwa. Hii kwetu inamaanisha kuwa mtu amefikia kiwango chake cha mwisho cha kufikiri.

Familia hii imeepuka janga jingine kwa mara ya pili

Francis ambaye ni mwana wa mwathiriwa anasema kuwa alikuwa ameenda kutafuta kuni alipokutana na babake ananinginia kwenye mti.

''Nilienda shule kwa sababu ya wazazi wangu na nilipoona vile hakuna jambo linguine ambalo lilikuja katika fikra zangu'', alisema Francis.

Wakati familia wakihuzunika nje, mtoto wake Francis aliingia ndani, na kuchukua sumu ya panya na kuandika ujumbe wake wa kwa nini anajiua.

''Bora nife kuliko kuhangaika, chomeni masalia yangu'', alindika katika ujumbe wake wa kuaga.

Lakini kabla ya kujidhuru alikutwa na maafisa wa polisi.

''Kwa mujibu wa maelezo ya kuwa bora kujiua kuliko uhangaika. Sina cha kusema kwa sababu nilipokuwa nimedhamiria kufanya hivyo lakini sikuwaza kabla au kupanga kuwa nitajiua. Kwa sababu ninajisikia maumivu ya kuachwa. Sitaki mtu mwingine kuumia kama mimi'', alisema Francis.

Kijana huyo anaelezea kuwa Sonona aliyokuwa nayo baba yake ilianza baada ya biashara yake kuanguka.

''Picha hiyo bado ipo akilini mwangu kila wakati ninapojaribu kulala. Ninajifunza kuwa jasiri kwa ajili ya wengine'', alisema

Tukirudi katika kijiji cha Shamata Joseph anamzika kaka yake.

''Ni siku ya giza kwangu. Ni siku ambayo siwezi kuisahau katika maisha yangu wakati ambapo ilinibidi nimuache kaka yangu aondoke na sitamuona tena. Ni siku ya giza katika maisha yangu''.