Nyangumi na wanyama wengine walivyotumiwa kufanya ujasusi

Nyangumi wa beluga katika kichwa cha James Bond Haki miliki ya picha Keith Hamshere
Image caption Licence to krill

Sheria moja ya upelelezi - Usijionyeshe kuwa jasusi.

Nyangumi wa beluga -iwapo hilo ndio jina lake- na anapatikana katika bahari ya Norway basi alitumika sana- Lakini alionekana kufanya makosa mara nyengine.

Sababu ambayo amekuwa akisababisha tashwishi miongoni mwa wavuvi wa Norway na wanasayansi ni kwamba alikuwa akivalia kamba na lebo ilionyesha kwamba kwamba anatoka St Petersburg nchini Urusi.

Urusi imekana kufanya makosa -na kufikia sasa nyangumi huyo amekataa kuzungumza.

Hawezi ama hatoweza?

Licha ya ukweli huo, ni wazi kwamba sio mara ya kwanza wanyama wametumiwa kufanyia upelelezi.

Paka

Haki miliki ya picha SensorSpot

Iwapo kuna kitu kimoja tunachojua kuhusu paka , ni kwamba wao hufanya chochgote wanachotaka na wakati wowote ule.

Kwa hakika, wao huwezi kuwadhania kufanya jambo baya ndiposa shirika la Ujasusi la CIA lilifikiria kwamba wanaweza kuwa wapelelezi wazuri sana.

Mwaka 1960, inakadiriwa takriban $14m zilitumika katika mradi wa kuweka vifaa vya kusikiliza ndani ya paka.

Lengo kuu lilikuwa kuingia kila mahali ili kuweza kukusanya ujasusi wa Urusi.

Lakini mpango huo haukufua dafu katika siku ya kwanza -wakati paka huyo alipogongwa na gari nje ya ubalozi wa Urusi mjini Washington na kufariki.

Mabomu ya popo

Haki miliki ya picha peters99

Ni ndege watulivu ,na wao huendelea na operesheni zao wakati wa usiku huku wakiishi katika maeneo fiche kama vile mapango. Ikiwa ni vigezo vizuri kwa mpelelezi yeyote- na njia nzuri ya Marekani kutumia.

Wakati wa vita vya pili vya dunia ,daktari mmoja wa meno alipendekeza kuwaweka vilipuzi vidogo wanyama hao .

Lengo lilikuwa kuviangusha katika miji ya Japan ili kuchoma nyumba kabla ya kulipuka na kusababisha moto mkubwa.

Majaribio kadhaa yalifanywa -ikiwemo kuchoma hanga ya ndege , lakini wazo hilo halikufaulu.

Vifaa vya kusikilizia

Haki miliki ya picha Windy Soemara

Juhudi zimefanywa kuunda nzi kuwa wapelelezi.

Mwaka 2008 jarida la new science liliripoti vile ambavyo idara ya ulinzi nchini Marekani ilijaribu kutengeza nzi bandia wenye nyaya ndani yake ili kuthibitiwa.

Uwezekano huo ulikuwa unafurahisha-ilikuwa fursa ya kurusha vifaa vidogo vya kusikiliza katika eneo la adui yako.

Miradi kama hyo imejaribiwa , huku ikiwa na ufanisi tofauti, kwa kushirikisha papa, panya na njiwa.

Huku teknolojia ikizidi kupiga hatua, lengo sasa ni kuunda vifaa vinavyosikiliza vinavyofanana na wadudu wadogo.

Alituhumiwa kwa makosa

Haki miliki ya picha Dgwildlife

Matumizi ya wanyama katika ujasusi yamefanyika kwa miaka kadhaa- kupitia njiwa waliotumwa kuwasilisha ujumbe katika vita vya dunia vya kwanza ama hata kupitia utumizi wa pomboo waliotumiwa na mataifa kama vile Marekani, Urusi na Israel ili kufanya upelelezi chini ya maji.

Lakini unaweza kufikiria wanyama ambao wamekamatwa kwa bahati mbaya na adui.

Mwaka 2007 jeshi la Iran lilikamata kundi moja la chindi 14 waliopatikana katika kinu cha kutengeneza nyuklia .

Haikujulika ni nini walichokuwa wakifanya .

Ndege pia wamesababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa idara za ujasusi.

Haki miliki ya picha clu

Mwaka 2013 mamlaka ya Misri ilimkamata ndege mmoja na sio tu mzigo kutokana na mzigo aliokuwa amebeba katika mdomo wake .

Ndege huyo alikuwa na kitambulisho kilichokuwa na kengele kwa wahudumu wa usalama.

Hatahivyo ndege huyo hakuwa na hatia.

Kitambulisho hicho kilikuwa kikitumiwa na wanasayansi wa Ufaransa kufuatilia mwenendo wake

Tumbili wa Hartlepool

Haki miliki ya picha PA
Image caption Tumbili hangus katika klabu ya hartlepool United

Licha ya kwamba tuhuma zozote za ujasusi ni kitu kibaya sana, ndege huyo na chindi waliishi kusema kilichotokeo.

Meli moja ya Ufaransa iliharibika katika ufukwe wa pwani ya kaskazini mashariki ya Uingereza wakati wa vita vya Napoleon.

Wakaazi wa Hartlepool walikuwa hawajawahi kumuona tumbili, ama kuona raia wa Ufaransa.

Na walipogundua kwamba tumbili huyo alikua akizungumza lugha ya adui wao, walimkamata na kudai kwamba alikuwa akiifanyia ujasusi Ufaransa na kumnyonga mnyama huyo ufukweni mwa bahari.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii