Kupambana na ubakaji na mfumo dume DR Congo

Moises and his wife Jullienne Haki miliki ya picha Fiona Lloyd-Davies/BBC
Image caption Moises alikuwa akimpiga mkewe Jullienne, ikiwemo wakati alipokuwa mja mzito

Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ina viwango vikubwa vya ubakaji na unyanyasaji wa kingono duniani. Lakini mtazamo mpya unajaribu kuitatuwa hali kwa kuwahimiza wanaume wakabiliane na wautathmini mfumo dume walio nao.

Moises Bagwiza ni mojawapo ya wanaume ambao sasa anajutia alivyokuwa, na anakumbuka namna alivyokuwa akimbaka na kumnyanyasa mke wake, Jullienne.

Hii ni simulizi ya kweli, ya kuogofya na huenda ikakukera.

"Ilikuwa kama vita kushiriki tendo la ndoa na yeye. Nilikuwa sijali amevaa nini - Niliziraruwa nguo zote," anasema.

Katika nyumba yao ya wastani katika kijiji chenye utulivu cha Rutshuru, huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Bagwiza anakumbuka kisa kimoja alichomnyanyasa mkewe wakati akiwa miezi minne mja mzito.

"Niligeuka nikampiga teke la tumbo," anasema, akieleza kwamba alianguka sakafuni, akiwa anavuja damu, majirani waliokuwa na wasiwasi wakamsaidia na kumpeleka hospitalini haraka.

Kosa lake? Alikuwa anaweka akiba ya pesa kwa matumizi ya nyumbani kupitia chama cha akina mama.

Haki miliki ya picha Fiona Lloyd-Davies/BBC
Image caption Jullienne Bagwiza anasema hawangeshiriki tendo la ndoa pasi kupigana na mumewe

Kabla ya kutokea shambulio hilo, alikuwa amekataa kumkabidhi pesa hizo , alizotaka kununua viatu.

"Ni kweli, pesa zilikuwa zake," Bagwiza anasema. "Lakini kama unavyojuwa siku hizi wanawake wanapokuwa na pesa wanajihisi kuwa na nguvu na huwa wanalionesha hilo..."

Maadili ya kitamaduni kuhusu kuwa mwanamume

Chuki hii ndio kiini cha tatizo na ambacho baadhi wanakiita mzozo wa mfumo dume katika Afrika ya leo.

Kwa karne kadhaa, wanaume wamelelewa kwa fikra za wazi, kwamba maana ya kuwa mwanamume ni: nguvu, mwanamume sio wa kulia, anayeilinda na kuitafutilia familia riziki.

Haki miliki ya picha Fiona Lloyd-Davies/BBC
Image caption Moises Bagwiza anasema aliamini kwamba mke wake Jullienne ni mali yake

Lakini mabadiliko katika majukumu ya kijinsia, ikiwemo kuwezeshwa pakubwa kwa mwanamke pamoja na kuwepo idadi kubwa ya wanaume ambao hawana ajira , inadidimiza uwezo wa wanaume kufikia maadili ya kitamaduni kuhusu kuwa mwanamume.

Na kwa baadhi ya wanaume kama Bagwiza, mwanamke anayejitegemea kifedha ana hatari kubwa kwa heshima yake kama mwanamume na mara nyingi huishia katika mzozo.

Bagwiza akiwa ni mjenzi katika kijiji hicho, anasema aliona kupigana au vita ndio njia pekee anayoweza kutumia kuwasiliana vyema na mkewe.

"Nilimchukulia kama mali yangu," alisema. " Nilidhani naweza kumfanyia chochote ninachotaka. Nilipokuja nyumbani alafu aniulize kitu, nilimpiga ngumi."

Njia ya kuficha 'kushindwa' kuwa mwanamume kamili

Hali iliyomkabili Bagwiza sio ya kipekee. Nchi ya Congo ina visa vingi vya ubakaji duniani, huku wanawake 48 wakikadiriwa kubakwa kila saa, kwa mujibu wa utafiti wa jarida la Marekani kuhusu afya ya umma.

Haki miliki ya picha Fiona Lloyd-Davies/BBC
Image caption Ilot Alphonse ni muasisi mwenza wa mtandao wa wanaume Congo kutokana na mfano wake katika suala la mfumo dume

Kiini cha tatizo la ubakaji DR Congo ni kikubwa zaidi ya inavyodhaniwa kwa mujibu wa Ilot Alphonse, muasisi mwenza wa mtandao wa wanaume Congo - shirika lisilo la kiserikali huko Goma (Comen).

"Tumerithi njia hii ya kuwachukulia wasichana kama mali zetu. wanaume wanatabua kwamba wana haki ya kushiriki ngono saa yoyote. Chanzo cha unyanyasaji wa kingono ni kuhusu nguvu na nafasi ambayo wanaume wa Congo daima, wametaka kuwa nayo."

Kuwahusisha wanawake katika majadiliano

Haki miliki ya picha Fiona Lloyd-Davies/BBC
Image caption Majadiliano yanagubika 'maana halisi' ya kuwa mwanamume

Jitihada za kukabiliana na ubakaji zimejaribu kukabiliana na unyanyasaji huo katika maenoe yalioathirika Afrika na zimewalenga wanawake, idadi kubwa ya waathirika na kuwatenga wanaume ambao ndio idadi kubwa ya watuhumiwa.

Lakini kwa Alphonse, jitihada hizi zinakabiliana na dalili tu kuliko chanzo cha tatizo lenyewe.

"Tunakabiliana na unyanyasaji kwa misingi ya kijinsia," anasema. "Ili hili liweze kufanikiwa ni lazima tuwahusishe wanaume na wavulana ambao ni sehemu ya tatizo, ili wawe na nafasi ya kuibadilisha hali kutokana na ushawishi walio nao katika jamii."

Na ndilo jambo ambalo Alphonse na wenzake wanalofanya.

Haki miliki ya picha Fiona Lloyd-Davies/BBC
Image caption Moises Bagwiza huhudhuria vikao vya Baraza vinavyoandaliwa na Comen

Wameunda 'Baraza Badilika' - vikao vya kijiweni vilivyokuwepo miaka mingi ya nyuyma ambapo wanaume walikusanyika kukabiliana na matatizo katika jamii na kuwafunza wavulana maana halisi ya kuwa mwanamume.

Wakati mizozo ikizuka katika vijiji na kuangamiza maisha ya wengi, maeneo haya pia yaliondoka, na kuchangia kutokuweko wanaume ambao ni kama kioo kwa jamii kwa wavulana wanaokuwa, Alphonse anasema.

Huenda ukavutiwa na taarifa hii pia:

Tofuati na kwamba katika miaka ya nyuma 'Baraza Badilika' lilikuwa likihudhuriwa na watu wazima pekee, katika karne ya sasa mwamko mpya unawapa wanawake nafasi muhimu za uongozi.

"Wakati umewadia kwa wanawake kuingia katika nafasi hizi," Alphonse anasisitiza.

'Waume wanaobadilika'

Kila wiki, takriban wanaume 20 hukutana katika Baraza kwa saa mbili kujifunza kuhusu manufaa ya kuwa mwanamume, usawa wa kijinsia na namna ya kuwa baba.

Haki miliki ya picha Fiona Lloyd-Davies/BBC

Vikao hivyo huongozwa na mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, wanaotumia falimu, vitabu na michezo ya kuigiza kubadili mtazamo na kutoa 'maana halisi' ya kuwa mwanamume kwa watuhumiwa ubakaji.

Alphonse anasema wanawake wengi wanamuambia kwamba waume zao wamebadilika baada ya kuhudhuiria vikao hivyo vya Baraza.

"Wanasema: 'Tulikwenda kwa imam, mchungaji. chifu wa kitamaduni, lakini hakubadilika. Amekamatwa mara kadhaa lakini hakubadilika, mara tu namona ameacha kuwa na kelel na vurugu na anarudi nyumbani mapema.'"

Bagwiza pia amepiga hatua kubwa tangualipompiga mkewe akiwa mja mzito.

"Ni kweli sio 100% - sisi ni binaadamu- lakini mambo mengo yamebadilika kwa kweli. Tunzaungumza vizuri sasa na uhusiano wetu katika tendo la ndoa umeimarika pakubwa."

Alphonse anatumai kumfikia "kila mwanamume" nchini Congo kwa mtazamo wake kuhusu namna nzuri ya kuwa mwanamume.

"Tunaitamani siku tutakapokosa kushuhudia aina yoyote ya unyanyasaji nchini," anasema. "Ili, wanaume, wanawake, wavulana na wasichana wote waweze kuishi."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii