Abu Bakr al-Baghdadi: Kwa nini ni vigumu kumkamata kiongozi wa Islamic State?

Abu Bakr al-Baghdadi

Ni mtu anayesakwa zaidi duniani. Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi mkimbizi wa wapiganaji wa Islamic State (IS) na uongozi wake wa kidini amewekewa $25m (£19m) na serikali ya Marekani kwa mtu yeyote atakayempata

Kwa zaidi ya miaka mitatu amekuwa akikwepa kukamatwa huku akiimarisha usalama wake hatua mabyo imefanya hadi kufikia sasa kuonekana mara moja , wakati alipotoa hotuba yake mjini Mosul mwaka 2014 akitangaza taifa la kidini atakalolitawala.

Mpema wiki hii Bahgdad alijitokeza katika kanda ya video ya dakika 18 akiwaomba wafuasi wake kuendeleza juhudi zake lakini akashindwa kutoa ishara za maficho yake.

Je yuko wapi sasa hivi, je anatafutwa vipi na ni kwa nini Marekani na washirika wake walio na vifaa vya teknolojia ya kisasa hawawezi kumpata?

Ripoti zinsema kuwa mnamo mwezi Novemba tarehe 3 2016 , Baghdad alifanya makosa ambayo karibia yahatarishe maisha yake.

Vita vya kupigania mji wa pili wa Iraq Mosul vilikuwa viikiendelea huku vikosi vinavyoongozwa na Marekani vikiendelea kuwasukuma wapiganaji wa Islamic State.

Kutoka eneo lisilojulikana la mji huo, Baghdad alitoa wito wa dakika 45 kwa wafuasi wake kuendelea kupigana.

Ujumbe huo ulishikwa na mawimbi ya ndege za kijeshi za vikosi vinavyoongozwa na Marekani , sauti inayofanana na kiongozi huyo ilibainika na kulikuwa na juhudi za kumshambulia.

Lakini kufikia wakati huo kiongozi huyo wa IS alikuwa tayari ametoweka, akitoroshwa na walinzi wake huku wakimshauri kutofanya tena hivyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Haijulikani ni wapi kiongozi huyo wa IS amejificha

Ilichukua majasusi wa Marekani takriban miaka 10 kumsaka na kumuaa Osama Bin laden , kati ya siku ya shambulio la 9/11 2001 hadi alfajiri ya tarehe 2 mwezi Mei wakati ambapo wanamaji wa Marekani walivamia nyumbani kwake nchini Pakistan.

Kitengo cha Ujasusi nchini Marekani NSA pamoja na kile cha Uingereza cha GCHQ vina uwezo mkubwa wa mawimbi ya kijasusi , wakichunguza na kushika kabla ya kurekodi ujumbe ulio wazi na ule uliofichwa duniani.

Hapo zamani , magaidi waliokuwa katika orodha ya watu wanaosakwa mara nyengine walikuwa wanaweza kujisema waliko kupitia ujumbe wa simu za rununu ama hata kuwa mtandaoni kwa muda mrefu katika eneo moja.

Bin laden alikuwa mwerevu kuhusu hilo huku naye Baghdad pia akifuata nyayo.

Kiongozi huyo wa al-Qaeda hatahivyo alitafutwa na kupatikana nyumbani kwake huko Abbottabad sio kupitia mifumo ya kidijitali bali kupitia muhudumu wake ambaye alikuwa akibeba kanda zake za propaganda na ujumbe mwengine kwa mikono kutoka eneo alilokuwa akiishi hadi kule ambako kanda hizo zilikuwa zikipakuliwa katika intaneti.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hotuba ya mwisho iliotolewa na Abu Bakr al-Baghdadi ndani ya msikiti mmoja mjini Mosul 2014

Kujua ni wapi kanda hizo zinatoka ndio ujasusi ambao Marekani imekuwa ikifanya kwanza kufautia kutolewa kwa kanda za video za Baghdad, lakini kundi lake la usalama lazima linajua hilo.

Ni washirika wake wa karibu sana ambao wanaandamana naye na kuna uwezekano wamekuwa wakisafiri naye mara kwa mara.

Ana usalama wa hali ya juu

Ni mzaliwa wa Samarra, nchini Iraq, mwaka 1971, Jina lake kamili ni Ibrahim Awad al-Badri.

Akiwa mfuasi mkuu wa dini ya Kiislamu tangu akiwa mdogo, baadaye alikuwa amefungwa katika kambi moja ya Marekani kwa jina Bucca 2004 kufuatia uvamizi wa Ufaransa na Marekani.

Akiwa katika kambi hiyo aliweka ushirikiano mzuri na wafungwa wengine wakiwemo maafisa wa zamani wa ujasusi nchini Iraq.

Aliifunza mengi kuhusu jinsi anavyoweza kufanya operesheni zake kutoka kwa maafisa wa ujasusi wa aliyekuwa rais wa Iraq Sadaam Hussein.

Usalama wake ni wa hali ya juu ,kutokana na kiwango cha juu cha wasiwasi alionao.

Lakini anajificha wapi?

Inadhaniwa kwamba bado yuko katika mpaka kati ya Syria na Iraq.

Katika mpaka huo ni raihisi kuanzisha mitandao ya biashara za ulaghai akitumia fedha kuweza kufanya lolote miongoni mwa watu wa makabila ya eneo hilo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alishirikiana na maafisa wa zamani wa ujasusi wa seriikali ya Iraq.

Aliyekuwa rais wa Iraq Sadaam Hussein alitoroka na kwenda mafichoni kwa miezi tisa baada ya utawala wake kupinduliwa.

Kitengo cha operesheni za Marekani cha Red Dawn kilimsaka na kumpata katika eneo la chini la ardhi ambalo alikuwa akilitumia kujificha karibu na eneo alikozaliwa mjini Tikrit baada ya mtoa habari mmoja kumsaliti akitarajia kupewa zawadi ya mamilioni ya madolla.

Lakini kuweza kumpata mshirika kama huyo ndani ya wandani wa Baghdad ni vigumu sana.

Idadi ndogo ya watu walio karibu naye huenda ni watiifu sana kuweza kuvutiwa na majaribio ya fedha.

Hivyobasi iwapo mtu huyo anayetafutwa zaidi duniani anaweza kukwepa mitandao, hapigi simu kwa kutumia simu za rununu na pengine anazunguka kutoka eneo moja la maficho hadi jingine je Marekani na magharibi zina matumaini gani ya kumpata? Pengine kabla ya kupanga shambulizi jingine la IS.

Hatimaye, inaweza kuwa bahati na uvumilivu: uwezekano wa kuonekana na mwanakijiji anayechunguza , au hata mwanachama wa IS aliyechoka na ambaye ameamua kuwa hatimaye wakati wa kuchukua zawadi ya pesa ili kuweza kuishi maisha yake yote, akiwa tajiri mafichoni umewadia.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii