Sudan: Je kuna ushawishi au uchochezi wowote wa kigeni katika taifa hilo?

Waandamanaji wa Sudan wakibeba bendera yao mjini Khartoum Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji wa Sudan wakibeba bendera yao mjini Khartoum

Tangu maandamano ya eneo la mashariki ya kati kwa jina"Arab Spring" yazuke yapata miaka minane iliopita eneo hilo limebadilika pakubwa.

Katika visa vingi utawala wa kiimla haukabiliwa vilivyo.

Katika maeneo ,mengine ulirudishwa kwa haraka, kama ilivyotokea nchini Misri ama polepole kama ilivyokuwa Syria.

Lakini ghasia na umwagikaji wa damu nchini Syria kwa kiwango kikubwa ulichangiwa na uchochezi wa nje.

Na sasa kuna hatari kwamba maandamano haya mapya katika eneo hili hususan Sudan huenda pia yanachangiwa na mikono ya kigeni.

Hii haimanishi kwamba Sudan ipo katika hatari ya kuanguka katika makundi na mapigano ya kijamii kama ilivyo Syria.

Lakini sababu nyingi kama hizo ambazo zilichangia maandamano hayo katika eneo la mshariki ya kati pia zinaonekana zikichipuka nchini Sudan, hususan mchango wa Saudia ambayo pamoja na washirika wake wa Ghuba wanatumia kila njia kuwa na ushawishi nchini Qatar na Uturuki.

Uhasama huu wa kieneo unaelezewa kwa upana na urefu na kutokuwepo kwa Marekani ambayo ndio mwanadiplomasia mkuu duniani.

Marekani pia imeshindwa na Urusi ambayo imetumia diplomasia yake nchini Syria kama njia ya kujikita katika meza ya kidiplomasia ya mashariki ya kati.

'Hamu ya sauti za waaandamanaji ipo chini'

Wasaudi wameteka na kusimamia diplomasia.

Wao na UAE wamejitolea kutoa usaidizi wa kifedha kwa Sudan pamoja na mafuta ya bei rahisi , chakula na dawa.

Abu Dhabi imeandaa mazungumzo na makundi tofauti ya wapiganaji kuhusu mipango ya kisiasa ya siku zijazo.

Na washirika wa Riyadh, Misri wamekuwa na jukumu kubwa katika kuonyesha misuli yake katika shirika la la umoja wa bara Afrika AU.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir (kushoto) alikuwa na ushirikiano mzuri na washirika wake wa Saudia

Huku Saudia ikionekana kuunga mkono majenerali wa taifa hilo , Uturuki na Qatar zinashirikiana kwa karibu na wapiganaji wa Sudan.

Inatambulika kwamba hakuna hata taifa moja linalochangia kutoka nje ambalo lina hamu ya sauti za waandamanaji nchini humo ama hata ujenzi wa taifa la Sudan lililo na demokrasia ya kweli.

Wote hatahivyo wana sababu zao za kulitaka taifa hilo kuwa thabiti.

Lakini kile kilichopo ni aina mbili za uongozi wa kiimla ambao unajaribu kuwasukuma wafuasi wao katika nafasi ambapo wanaweza kushawishi hatma ya taifa hilo siku zijazo.

Sudan imebadili ushirikiano wake na mataifa ya kigeni.

Muongo mmoja uliopita, kabla ya maandamano ya mashariki ya kati {Arab Spring}, Sudan ilionekana na Washington kama mfadhili wa ugaidi, ilikuwa ikilengwa sio tu na vikwazo vya Marekani kuhusu vitendo vyake vya mzozo wa Darfur lakini pia makombora.

Sudan ilionekana kuwa rafiki wa wapiganaji wa Islamic State na Iran.

Saudia ilifanikiwa kuishawishi Sudan kuingia katika muungano mkubwa ya mataifa ya Kisuni.

Sio jambo la kushangaza kwamba idadi kubwa ya wananjeshi wa Sudan waliunganna na Saudia katika kampeni yake iliokumbwa na utata nchini Yemeni.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanajeshi wa Saudia pamoja na vikosi vya kijeshi vinavyoungwa mkono na Suadi nchini Yemen

Lakini katika siku za hivi karibuni Sudan imekuwa ikizawadiwa.

Mnamo mwezi Machi 2018, Qatar, Uturuki na Sudan ziliingia mkataba wa kuitenegeza bandari ya bahari ya shamu ya Suakin mbali na uwekaji wa kambi ndogo ya wanamaji wa Uturuki.

Itakumbukwa kwamba Qatar ndio iliokuwa bandari ya kwanza ya rais Omar al-bashir wakati maandamano yalipoanza mnamo mwezi Januari.

Lakini kwa sasa ni Saudia inayozidi kuwa na ushawishi nchini Sudan.

Kutokuwepo kwa washikadau wakuu

Ushujaa hatahivyo unakwenda kwa wale raia waliokongamana katika barabara kuu za mji wa Khartoum kushiriki maandamano.

Washikadau wakuu wa kimataifa ikiwemo - Umoja wa mataifa UN, Muungano wa Ulaya na Umoja wa bara Afrika wamekuwa na ushawishi mdogo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano yameendelea dhidi ya jeshi la Sudan wiki kadhaa baada ya kuondolewa madarakni kwa Omar al-Bashir

Utawala wa Trump hauna hamu yoyote nchini Sudan.

Marekani haina hamu na eneo hilo huku ikitoa ishara kwamba inataka kupunguza idadi ya wanajeshi wake walioko katika eneo hilo.

Marekani inaendelea kuwaweka wanajeshi wake nchini Syria lakini haipo katika usukani kuhusu hatma ya kidiploimasia ya taifa hilo.

Wachanganuzi wengi wanadai kwamba kutokuwa na hamu kwa Marekani nchini Sudan ni fursa iliopotea kwa taifa hilo kuongoza mkakati wa kidiplomasia ambao huenda ukasaidia kuimarisha hali ya taifa hilo ya siku za baadaye.

Cha mno ni kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba rais Trump hataki kwenda kinyume na mshirika wake mkuu Saudia.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii