Mwalimu Maprosoo muuza mshkaki
Huwezi kusikiliza tena

Mwalimu 'Maprosoo' mchana, jioni muuza mishikaki Mtwara

Josephat Mussa amekuwa mwalimu kwa miaka 16 na Mwalimu mkuu kwa miaka 11 kabla ya kushushwa daraja mwaka mmoja uliyopita kutokana na kutokuwa na kiwango stahiki cha elimu kwa ngazi hiyo. Hali iliyopelekea kipato chake kuporomoka na kuamua kujiingiza kwenye ujasiriamali. Kwa miezi sita sasa mwalimu huyu maarufu kwa jina 'maprosoo' anachoma na kutembeza mishikaki katika mitaa mbali mbali ya mji wa Mtwara, kumuwezesha kuendelea na ujenzi wa nyumba yake na kuipatia familia yake mahitaji bila ya kutegemea mshahara wake.

Mpiga picha: Eagan Salla

Mada zinazohusiana