Jinsi ya kumsaidia mtoto wako kupenda kula vyakula vyenye afya

Mtoto anaekula mboga Haki miliki ya picha Getty Images

Mara kwa mara wazazi na walezi wengi wamekuwa wakihangaika kuwashawishi watoto wadogo kula vyakula vinavyousadia mwili kuwa na afya nzuri kama vile mboga ambavyo wengi wao huwa hawazitaki.

Ulaji wa vyakula visivyousaidia mwili kiafya mara nyingi huwafamnya watoto wanaoishi maeneo hasa ya mijini kunenepa mwili kupita kiasi na wengine hata kupata maradhi kama vile moyo na kisukari.

Mfano Uingereza kuna idadi kubwa ya watoto wenye matatizo ya afya yanayotokana na uzito wa kupita kiasi - lakini mji mmoja nchini humo unaonekana kufanikiwa kuwasaidia watoto kula vyakula vyenye afya.

Takwimu zilizotolewa kwenye mkutano kuhusu unene wa mwili wa kupindukia zimeonyesha kuwa wa Leeds imeweza kupunguza viwango vya watoto wanene kupindukia kwa 64% katika miaka ya hivi karibuni.

Sehemu muhimu ya mkakati wa mji huo wa kukabiliana na unene wa mwili kupita kiasi ulilenga zaidi shule za chekechea na kuwapatia mafunzo wazazi juu ya nanma ya kuwasaidia watoto wao kuwa wenye afya.

Lakini si kila wakati wazazi na walezi wanaelewa somo la chakula .

Je ni mambo gani unayoweza kufanya kumshawishi mwanao kula chakula cha afya?

Kuwalisha vyakula vya aina tofauti

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tina Le anasema watoto wanapaswa kupewa fursa ya kuchagua chakula wanachokipenda miongoni mwa vyakula vyenye afya

Tina Le hutoa warsha kama zile ambazo zimekuwa zikifanyika katika mji wa Leeds kwa wazazi mashariki mwa London.

Anasema kumpatia mtoto fursa ya kuchagua vyakula wanavyokula wakiwa na umri mdogo , kwa kuwapatia nafasi ya kuchagua vyakula vya afya vya aina mbili, inaweza kusaidia kutoa mwongozo utakaowasaidia kula vema.

Huwezi kusikiliza tena
Baadhi ya dawa

"Hii inaweza kuwasaidia kupunguza hatari ya wao kukataa kula kitu chochote kabisa na hujihisi wao ndio wenye kauli ya mwisho ," anasema.

"Wakati tunapowanyima watot wetu fursa ya kuchagua chakula wanachokipenda, huwa wanahisi nhawana la kufanya na huwafanya kuwa wenye hasira."

Hatua ndogo ndogo

Anna Groom, Daktari wa masuala ya lishe ya watoto, anakiri kuwa si rahisi kila mara hasa kama mtoto ni mwenye kupenda kuchagua chakula.

Amesema kuanza na mabadiliko ya taratibu ya chakula unachompatia inaweza kupumpunguzia shinikizo ambalo baadhi ya watoto huwa nalo saa za mlo zinapokaribia na kuepusha malumbano wakati wa chakula.

" Ni muhimu wawe na chakula ambacho unafahamu kuwa wanakipenda, lakini pia unaweza kuanzisha kitu kipya kwenye sahani yao kwa kiasi kidogo ," anasema.

Haki miliki ya picha Belinda Mould
Image caption Mwanzoni Belinda alihangaika sana kumshawishi binti yake kula vyakula vya afya

Belinda Mould alibaini mbinu ambayo ilikuwa nzuri ya kumshawishi binti yake mwenye umri w amiaka mitatu, ambaye awali akikuwa anakula Soseji tu na maharage ya kuokwa.

"Ilikuwa tukimlisha vyakula vingine anavitupa sakafuni au anavip[uuza na matokeo yake hali chochote " aliiambia BBC

Lakini anasema kwa kumshawishi kula kiwango kidogo cha chakula kipya mara kwa mara, sasa mwanae anakula karibu kila kitu.

"Ninasema , 'Unaweza kumwambia, kula mara moja tu ujaribu na kama hautakipenda , unaweza kula chakula kingine '," anasema Belinda

"Unahitaji kuwa mwenye subira ," na kuongeza kuwa . "Kwa hiyo ikiwa watakataa, jaribu tena mara nyingine ."

Uwe kielelezo kizuri cha kuigwa

Tina anasema kuwa mfano mzuri kwa mtoto tangu aliwa na umri mdogo ni jambo muhimu.

" kama unakula chakula cha afya wewe mwenyewe, mtoto wako ana uwezekano mkubwa wa kujifunza kutoka kwako kwa kuiga kile unachokifanya," anasema.

Anaongeza kuwa kula pamoja wakati wa chakula au kuwasaidia watoto wadogo kuwaiga tabia ya 'ulaji wa wazazi ' ni muhimu

Anna anasema kuwa ni muhimu kwa wazazi kutokizungumzia vibaya au kutoa maoni hasi juu ya chakula ambacho hawakipendi mbele ya watoto wao, kwani wanaweza kushawishi mtizamo wao juu ya vyakula vipya

Rewards

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tina Le anashauri wazazi watoe zawadi ya kuwapeleka watoto kucheza kuliko kuwazawadia vyakula

Kutoa zawadi na kuwasifu watoto kwa kula vyakula vya afya inaweza kuimarisha tabia nzuri ya mtoto , Tina anasema.

Hata hivyo, anasisitiza kuwa zawadi haipaswi kuhusiana na chakula, na badala yake mtoto apewe zawadi ya kutembelelea sehemu za michezo , kuchora au kupanga vichezeo vya michoro ya vitu mbali mbali kwa mpangilio unaotakiwa.

"Kila mara tunasema epuka kutoa rushwa mwanao ," anasema.

"Usiseme kama ukila chakula hiki nitakupa chokoleti au ice cream kwasababu hilo huwafanya kufikiria kuwa chakula cha afya tunachotaka wale kina thamani ndogo kuliko zawadi unayowapatia ."

Muonekano wa mwili

Hasa kwa watoto wakubwa, chakula na uzito wa mwili huwa ni mada ambayo ina utata kidogo kuizungumzia na hofu juu ya muonekano wa umbo lao la mwili huchangia katika suala la kujiamini.

Utafiti wa hivi karibuni ulibaini kuwa unene wa mwili wa kupindukia na afya ya akili vina uhusiano wa karibu sana, huku watoto wanene kupita kiasi wakiwa na uwezekano mkubwa wa kuathirika kisaikolojia mfano kuw na wasiwasi na kujihisi hawana raha wala matumaini.

Tinaanapendekeza wazazi wabadili namna wanavyozungumzia chakula kwa kuepuka kuhusisha ulaji wa chakula cha afya na muonekano wa umbo la mwili wa mtoto.

"Watie moyo kuwa wenye afyakwasababu inawafanya wajihisi vizuri , badala ya kuwaeleza kuwa chakula wanachokula kitawafanya wawe na muonekano fulani ," anasema.

Anna anaafiki kuwa lugha ni muhimu unapozungumzia suala la uzito wa mwili.

"Ni muhimu familiazishauriwe kufanya mabadiliko kw aujumla ili mtoto asijihisi kuwa analengwa kw akupewa chakula fulani ," anasema.'

Kusema vkauli mfano 'tujitahidi tuwe familia yenye afya' , inamaanisha kuwa mtoto huenda asiwe na wazo kuwa wazazi wana hofia unene wao wa mwili , lakini hilo linaweza kuboresha lishe yao ."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii