Google itafuta moja kwa moja matukio yanayofuatiliwa katika mtandao

Google logo Haki miliki ya picha Getty Images

Mtandao wa Google unatoa fursa kwa watumiaji wake kutumia kipengele ambacho kitaweza kufuta taarifa moja kwa moja katika mtandao huo na historia ya eneo lilipotokea baada ya miezi mitatu.

Mfumo huo mpya tayari umeruhusu watumiaji kufuta wenyewe wakiwa wanatumia Youtube , ramani au wanatafuta jambo katika mtandao.

Kwa sasa , mfumo huo umetoa nafasi kubwa zaidi kwa mtandao wenyewe kufuta baada ya miezi mitatu au kumi na nane.

Google imesema kitendea kazi hicho kitaanza kutumika wiki zijazo.

Mwezi novemba , mtandao huo ulishutumiwa kwa kuweza kutambua watu walipo licha ya kuwa walikuwa hawajawasha sehemu ambayo inatoa historia ya eneo.

Na kilichoshangaza zaidi mwaka huu ni kuwa watu wengi waliripoti kuwa kuna wakati wakati huwa wanasikia sauti zikiwarikodi.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Google inatoa fursa kwa watumiaji kujiongoza katika mtandao wao

Kwa sasa , historia ya ya mtandao wa Google na kuonesha mahali mtu alipo umesimamishwa kwa muda kwa kila mtumiaji.

Lakini katika wiki zijazo mtandao huo utatoa fursa kwa taarifa kujifuta moja kwa moja kama miezi mitatu itakuwa imepita tayari.

Ingawa haitatoa nfuno huo wa taarifa kujifuta moja kwa moja katika youtube au sauti.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii