Muhubiri wa Kiislamu nchini Indian Zakir Naik ashtakiwa kwa ulanguzi wa fedha

Zakir Naik Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zakir Naik amekana mashtaka hayo dhidi yake

Waendesha mashtaka nchini India wamemshtaki muhubiri wa Kiislamu 'mwenye utata' nchini Indian Zakir Naik kwa ulanguzi wa fedha.

Bwana Naik ambaye anaishi mafichoni , ameshtakiwa kwa kujipatia mali yenye thamani ya $28m kwa njia za uhalifu , madai anayokana.

Mamlaka nchini India pia imemtuhumu kwa kutoa matamshi ya chuki na kuchochea ugaidi.

Bwana Naik mwenye umri wa miaka 53 hukuza Uislamu wenye itikadi kali katika runinga ya Peace TV .

Runinga hiyo imepigwa marufuku nchini India lakini ina takriban wafuasi milioni 200 kote duniani.-ikirusha matangazo yake kutoka Dubai,

Runinga ya Peace TV inamilikiwa na wakfu wa utafiti wa Kiislamu Islamic Research Foundation-kundi linaloongozwa na bwana Naik.

Mataifa mengine yameipiga marufuku runinga hiyo-ikiwemo Bagladesh ambapo kinatuhumiwa kwa kumchochea mpiganaji mmoja aliyeshambulia mkahawa mmoja mjini Dhaka 2016 ambapo takriban watu 22 waliuawa.

Idara inayochunguza uhalifu wa kifedha nchini India ED iliwasilisha mashtaka hayo dhidi ya bwana Naik katika mahakama ya Mumbai siku ya Alhamisi.

Iliambia mahakama kwamba ilitambua mali yenye thamani ya mamilioni ya madola kama iliopatikana kupitia njia ya uhalifu.

''Hotuba za bwana Naik zimechochea idadi kubwa ya vijana wa Kiislamu nchini India kutekeleza vitendo vilivyo kinyume na sheria pamoja na viule vya kigaidi'', ED aliambia mahakama.

Idara hiyo imemtuhumu kwa kutumia fedha kutoka kwa vyanzo vinavyoshukiwa kununua mali nchini India na kufadhili matukio ambapo anadaiwa kutoa hotuba za kuchochea.

Lakini bwana Naik anasema kuwa fedha hizo zilipatikana kwa njia halali.

Je Zakir Naik ni nani?

Njia anayotumia Bwana Naik kuhubiri dini imedaiwa kuwa na utata.

Wafusi wengi wa kundi la al-Qaeda wanaozuiliwa wameripotiwa wakidai kwamba ni yeye aliyewashawishi.

Alipigwa marufuku kuingia Uingereza 2010 kwa tabia ambayo haikubaliki na kutokana na hotuba yake na waziri mkuu wa sasa Theresa May.

Hatahivyo ni mwezi Julai 2016 wakati alipovutia hamu ya kimataifa baada ya shambulio baya katika mkahawa wa Artisan cafe mjini Dhaka.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waandamanji nchini India wanafanya maandamano dhidi ya Zakir Naik baada ya shambulio la Dhaka mnamo mwezi Juali 2016

Vyombo vya habari vya Bangladeshi vilidai kwamba mmoja ya wapiganaji alichochewa na hotuba zake.

Baadaye mwezi huo serikali ya Bangladesha ilipiga marufuku runinga ya Peace TV.

Mnamo mwezi Novemba 2016, idara inayokabiliana na ugaidi nchini India iliwasilisha malalamishi rasmi dhidi ya bwana Naik, ikimtuhumu kwa kukuza chuki za kidini na vitendo visivyo halali.

Bwana Naik alihamia nchini Malaysia 2017.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii