Utafiti: Wapenzi wa jinsia moja wanaotumia dawa za HIV hawaambukizi

wanandoa wapenzi wa jinsia moja Haki miliki ya picha Getty Images

Ushahidi zaidi kwamba wapenzi wa jinsia moja wanaotumia dawa za HIV hawawezi kuambukizana umedaiwa kuwa na ujumbe mzito ambao unapaswa kusambazwa duniani.

Utafiti uliofanyiwa takriban wapenzi wa jinsia moja 1000 ambao ni wanandoa ulibaini kwamba hakuna hatari ya maambukizi katika kipindi cha miaka minane.

Hii inatokana na tiba hiyo ambayo inapunguza viwango vya virusi hivyo kuwa chini zaidi.

''Virusi ambavyo haviwezi kuonekana haviwezi kusambazwa'' , ''ndio ujumbe rasmi unaofaa kupitishwa kwa kila mtu duniani'', alisema mtaalamu.

Utafiti huo uliofanywa Ulaya uliwafuata wapenzi wa jinsia moja wanaume walio katika ndoa-ambapo mmoja alikuwa akiishi na virusi vya Ukimwi na kutumia dawa za kukabiliana na virusi hivyo huku mwengine akiwa hana virusi hivyo- kwa kipindi cha miaka minane kutoka 2010-2017.

Hakuna maambukizi yoyote yaliotokea baina ya wanandoa hao katika kipindi chote.

Na watafiti hao wanasema kwamba takriban visa 472 vya HIV huenda vilizuiwa.

kwa jumla wanandoa hao walishiriki ngono bila kutumia mipira ya kondomu mara 76,088.

Ijapokuwa wanaume 15 waliambukizwa virusi hivyo wakati wa utafiti huo, vipimo vya jeni vilibaini kwamba maambukizi hayo hayakutoka kwa wapenzi wao.

Ugunduzi wetu umebaini kwamba hatari ya maambukizi ya virusi vya HIV miongoni mwa wanaume ambao ni wapenzi wa jinsia moja wakati viwango vya virusi iko chini, watafiti hao walisema.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tiba ya HIV inafaa kuanza punde tu mtu anapogundua ana virusi hivyo

Profesa Alison Rodger, ambaye ni mwanzilishi wa utafiti huo na preofesa wa magonjwa ya maambukizi katika chuo kikuu cha London , amesema kuwa wapenzi wa jinsia moja walio wanaume wamekuwa wakiwa katika hatari kubwa ya maambukizi lakini sasa wamepata hakikisho.

Ujumbe huo mzito unaweza kusaidia kuangamiza ugonjwa huo na kukabiliana na unyanyapaa na ubaguzi ambao watu wengi wenye virusi vya HIV wanakabili.

Amewataka watu wanaoishi na HIV kupimwa kabla ya kupata tiba ya virusi hivyo.

'Ni afueni kubwa kugundua siwezi kuambukiza mtu HIV'

Matt Stokes, 26, alipatikana na virusi vya HIV 2016 na kuanza kutumia dawa wiki nne baadaye.

Vipimo vilibaini kwamba virusi hivyo havionekani katika mwili wake katika kipindi cha miezi mitatu.

''Ni afueni kubwa na inanipatia motisha kujua kwamba siwezi kumuambukiza mtu mwengine virusi hivyo'', alisema.

Miongoni mwa jamii ya wpenzi wa jinsia moja na marafiki zangu kumekuwa na mabadiliko makubwa katika siku za hivi karibuni.

Lakini kuna hatua kubwa ya kupigwa kabla ya kila mtu kujua ina maanisha nini'', anaongezea.

Kuna wengine hawataki kuamini -wana hofu kwamba huenda sio ukweli. Anasema kwamba wana kampeni wanaupiga jeki ujumbe huo na kubadilisha mtazamo wa ngono.

Kukabiliana na unyanyapaa

Deborah Gold, afisa mkuu mtendaji wa shirika la Ukimwi la (National AIDS Trust) alisema kuwa mengi yanapaswa kufanywa ili kuusambaza ujumbe huo kwa maafisa wa afya pamoja na umma.

''Kuna umuhimu wa kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu HIV na vile unavyosambazwa , na kwamba tiba inasitisha maambukizi , tunadhani hilo ni muhimu sana katika kukabiliana na unyanyapaa''.

Utafiti wa awali ulionyesha kwamba hakuna hatari ya kuusambaza ugonjwa huo miongoni mwa wanandoa wa jinsia tofauti iwapo mmoja wao ana virusi na anatumia dawa ya kukabiliana na virusi hivyo vya HIV

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dawa za kukabiliana na HIV hukandamiza virusi hiyo kutosambazwa

Katika utafiti huo wanaume walio na virusi vya HIV wamekuwa wakitumia dawa za kukabiliana na maradhi hayo kwa muda wa miaka minne kabla ya kuanza , hatua iliofanya virusi hivyo kutoonekana .

Wengi hujipata katika hali hiyo baada ya kutumia dawa za kukabiliana na Virusi kwa takriban miezi sita.

Je tiba ya kukabiliana na HIV ni ipi?

Ni mchanganyiko wa dawa zinazotumika kila siku ili kusitisha ueneaji wa HIV mwilini.

Tiba hiyo haiwezi kutibu HIV lakini inaweza kupunguza makali ya virusi hivyo katika kiwango cha kutoonekana katika damu.

Watu wengi wenye virusi hutumia mchanganyiko wa dawa hiyo mara moja kwa siku lakini wengine hutumia hadi dawa nne kwa siku ikitegemea mahitaji ya afya.

Kila mtu anaagizwa kuanza tiba hiyo mara tu anapogunduliwa ana ugonjwa huo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii