Rwanda: Wahanga wa mauaji ya kimbari ya Rwanda zaidi ya 84,000 kuzikwa leo

Baadhi ya masalia ya miili yatakayozikwa leo yalifukuliwa kutoka majengo ambayo yalibomolewa
Image caption Baadhi ya masalia ya miili yatakayozikwa leo yalifukuliwa kutoka majengo ambayo yalibomolewa

Shughuli ya kuzika kwa heshima miili zaidi ya 84,000 ya wanyarwanda waliokufa wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994 imeanza katika eneo la makumbusho ya mauaji hayo la Nyanza Kicukiro Memorial mjini Kigali.

Miili hiyo ilifukuliwa kutoka kwenye mashimo ya pamoja katika mji mkuu wa nchi hiyo Kigali .

Shughuli ya kufufua miili hiyo ilianza Aprili mwaka jana. Baadhi ya miili ilifukuliwa kutoka majengo ambayo yalibomolewa.

lipangwa kuwa shughuli ya kuwazika wahanga hao kwa heshima ifanyike Machi 29, 2019, lakini iliahirishwa baada ya mamlaka nchi humo kusema kuwa makaburi mengi ya pamoja yalikuwa yamegundulika katika maeneo mengi.

Mabaki ya miili hiyo yatazikwa katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Nyanza Genocide Memorial katika wilaya ya Kicukiro jijini Kigali.

Image caption Baadhi ya makaburi ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya 1994 katika eneo la Nyanza wilayani Kichukiro ambako miili zaidi ya 84,000 inazikwa Jumamosi 04/05/2019

Makamu mwenyekjiti wa jumuiya ya waathiriwa wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda Ibuka- Egide Nkuranga, amesema kuwa mipango inafanyika kuutangazia umma ili kuwapa fursa manusura wa mauaji hayo , hususani wanaoishi nchi za kigeni kurejea nyumbani kuwazika wapendwa wao.

" Kuna majengo mengine ambayo yametambuliwa kuwa chini misingi yake yake kuna miili ya waathiriwa wa mauaji ya kimbari. Sasa , mabaki ya miili ya watoto wachanga waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari inafukuliwa ,"alisema Nkuranga, huku akionyesha nyumba ya mkazi wa jiji la Kigali aliyefahamika kama Safari.

"Tunatumai kuwa kufikia Mei 4, tutakuwa tumekamilisha shughuli ya kufufua miili ,' alisema.

Amefichua kuwa waliouawa walimwagiwa kemikali ya asidi na chumvi, hii ikimaanisha kuwa ni vigumu kutambulika.

Tangu Kumalizika kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, shughuli ya kuzika miili ya ya wahanga wa mauaji hayo, lakini idadi hii ya mazishi ya miili ya watu ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Wazee wanyooshewa mkono baada ya mauaji ya kimbari Rwanda

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii