Osama bin Laden: Miaka minane baada ya kifo chake, al-Qaeda liko wapi?

Protesters in Pakistan following the death of Osama bin Laden Haki miliki ya picha Getty Images

Ni miaka minane leo tangu Osama bin Laden, muasisi wa al-Qaeda, alipouawa na vikosi vya Marekani nchini Pakistani katika mji wa Abbottabad.

Kundi aliloliongoza ni baya zaidi la kijihadi duniani, lililo na maelfu ya wapiganaji.

Linaaminika kuwa na rasilmali si haba za kifedha

Lakini tangu kuuawa kwa kiongozi wake na kuzuka kwa kundi la Islamic State group (IS), nguvu ya kundi la al-Qaeda na ushawishi wake umefifia pakubwa.

Lina ushawishi kiasi gani basi kundi hili leo, na lina tishio lolote kwa usalama wa kimataifa?

Kuzuka kimya kimya

Wakati IS limegubika vyombo vya habari katikamiaka ya hivi karibuni, al-Qaeda limekuwa likitafuta mbinu ya kujijenga upya na kuwana uhusiano na makundi ya kieneo.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni, Shirika la ujasusi Marekani limeonya kwamba viongozi wakuu wa al Qaeda wana "wanaimarisha ushawishi wa mtandao huo duniani na kuendelea kuhimiza amshambulio dhidi ya mataifa ya magharibi na Marekani."

Umoja wa mataifa, katika ripoti iliochapishwa mapema mwaka huu kuhusu tishio la ugaidi duniani, umesema al-Qaeda "linaonekana kuongeza azma .... linasalia kuwa na ustahimili na wapiganaji wapo katika maeneo mengi na inasalia na hamu ya kutaka kujionyeshauwepo wake kimataifa."

Mnamo Februari mwaka huu mkuu wa idara ya ujasusi Uingereza, Alex Young, ameonya kuhusu kuzuka upya kwa al-Qaeda.

Mtandao wa washirika

Opereshenikali ya kutumia ndege zisizo na rubani ya jeshila Marekani, kuuawa kwa kiongozi mkuu, na changamoto ya kundi la Islamic State limelilazimu al-Qaeda kuvumbua mbinu mpya.

Limefanikiwa kuidhinisha mtandao wa washirika au 'matawi' barani Afrika, mashariki ya kati na Asia kusini.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashambulio ya al-Shabaab, mshirika wa kundi la al-Qaeda, hushuhudiwa mara nyingi Somalia

Washirika hawa ni makundi ya wanamgambo walio miongoni mwa jamii na wameapa kuutii uongozi wa al-Qaeda.

Tofauti na IS, al-Qaeda limejihadhari kutoitenga jamii.

Seehmu ya mpango wake mpya ni kujenga uhusiano na kuwasiliana na jamii katika miradi ya maendeleo.

Mnamo 2013 al-Qaeda lilitoa "Muongozo jumla wa Jihad" lililoidhinisha mageuzi muhimu katika kundi hilo.

Waraka huo, miongoni mwa mengine unasisitiza jitihada za kujizuia na mtazamao wa kijamii zaidi , kutoa maelekezi kwa wapiganaji kuepuka tabia zinazoweza kuchochea "mapinduzi ya umma."

Al-Qaeda limekuwa likiongeza mashambulio yake kupitia matawi yake na washirika wake.

Mnamo 2018 lilitekeleza mashambulio 316 duniani, kwa mujibu wa data iliokusanywa na Armed Conflict Location & Event Data Project (ACLED).

Matawi ya Al-Qaeda

  • Al-Qaeda katika eneo la magharibimwa Afrika (AQIM) liliidhinishwa mnamo 2006 wkati kundi lenye makao yake Algeria- la wanamgambo lenye mafungamano na al-Qaeda. Kufuatia msako wa vikosi vya Algeria limesogea kuelekea katika eneo la Sahel na Afrika magharibi.
  • Al-Qaeda katika rasi ya kiarabu (AQAP) liliundwa mnamo 2009 katika muungano kati ya makundi mawili ya kieneo yanayotokana na mtandao huo wa kimataifa nchini Yemen na Saudi Arabia.
  • Al-Qaeda katika bara Hindi (AQIS) linahudumu Afghanistan, Pakistan, India, Myanmar na Bangladesh, na liliidhinishwa Septemba 2014.
  • Jama'at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) ni mshirika wa al-Qaeda-lililoundwa kutokana na muungano wa makundi ya wanamgambo nchini Mali na Afrika magharibi.
  • Al-Shabaab lipo nchini Somalia na Afrika mashariki na limeapa kutii uongozi wa al-Qaeda mnamo 2012.
  • Hayat Tahrir al-Sham (HTS) ni muungano wa makundi kadhaa ya wapiganaji jihadi nchini Syria, na lina mafungamano na al-Qaeda, kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. HTS linadhibiti jimbo la Idlib kaskazini mwa Syria.
  • Al-Qaeda nchini Misrilinajumuisha makundi yenye mafungamano na al-Qaeda yanayohudumu katika rasi ya Sinai nchini Misri.

Idadi ya wapiganaji katika makundi shirika ya al-Qaeda

Takwimu tangu Agosti 2018
Chanzo: CFR/UN/CTC

Mustakabali wa uongozi ni upi?

Katika hotuba mnamo 2015, kiongozi wa sasa wa al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri, amemtambulisha kijana "simba" wa mtandao wa kigaidi wa bin Laden.

Kijana huyo ni Hamza bin Laden, mwanawe Osama bin Laden anayepigiwa upatu na wengi kuwa mrithi wa uongozi wa al-Qaeda.

Marekani imemtangaza Hamza kuwa gaidi wa kimataifa na imetangaza kitita cha fedha za hadi $1m kwa taarifa kuhusu aliko.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hamza Bin Laden hajulikani aliko

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 amesifiwa kama nyota chipukizi katika mitandao ya al-Qaeda, mtu ambaye wanatumai atatazamiwa na kizazi kijacho cha wapiganaji jihadi na kulizindua upya kundi hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni, alitoa kanda ya sauti na ujumbe kwenye video akiwataka wafuasi kuishambulia Marekani na washirika wa mataifa ya magharibi katika kulipiza kisasi mauaji ya babake.

Kwa mujibu wa Lina Khatib, mkuu wa masuala ya mashariki ya kati na Afrika kaskazini huko Chatham House - taasisi ya sera huru Uingereza, " Kuangamizwa kwa IS kumelishinikiza al-Qaeda kujifikiria zaidi na kufanya mipango mizito kuhusu operesheni zake.

"Al-Qaeda linategemea kuwa na kiongozi wa kimikakati. Hili linamsaidia Hamza Bin Laden kuungwa mkono katika azma yake ya kuichukua nafasi ya babake kama kiongozi wa al-Qaeda's leader," anasema.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii