Fundi Nyangalio: Mlemavu asiyeona kubuni mavazi ya stara

vazi

Kwa namna ya kipekee , fursa ya kuonesha nguvu ya ubunifu wa mtu mwenye ulemavu wa macho imeoneshwa katika tamasha la tano la maonesho ya mavazi la Stara.

Mlango mmoja wa fahamu ulimuongoza Abdallah Nyangalio kuonesha uwezo wake jukwaani sawa na mtu mwenye viungo kamili bila kutetereka.

Abdallah Nyangalio si jina geni Tanzania na Afrika mashariki, yeye ni mshonaji nguo ambaye anapima kwa kutumia viganja vya mikono yake na kushona bila kukosea.

Kikubwa ni hali yake ya kuwa kipofu kutokana na maradhi lakini ameweza kupata tuzo kadhaa kwa sababu ya uweredi wa kazi yake.

Image caption Fundi Nyangalio akimpima mteja

Mwaka huu 2019, ameonyesha uwezo na uthubutu wa hali ya juu kwa kupanda katika jukwaa la maonyesho la mavazi katika tamasha la mavazi la stara ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo.

Mwandishi wa BBC, Regina Mziwanda alifanya mazungumzo na bwana Nyangalio na kufafanua kazi hiyo aliifanyaje pamoja na changamoto alizokutana nazo wakati wa kuandaa kazi hiyo.

"Zile nguo zote nimeshona mimi mwenyewe kuanzia shati mpaka magauni, na alafu nikawapa mafunzo ya namna ya kutembea jukwaani na kweli waliweza kutembea vizuri sana" Nyangalio aeleza.

Haki miliki ya picha Stara

"Jukwaa halikuwa limetengenezwa maalum kwa watu wenye ulemavu, lakini tulipambana na lile jukwaa ingawa siku nyingine tungepewa fursa ya kutoa maoni ya namna gani ambavyo jukwaa ambalo ni rafiki kwetu walemavu".

Kwa ni ni tamasha la nguo za stara mwaka huu liliamua kutumia mbunifu mlemavu wa macho

"Tulitaka alete mabadiliko katika tasnia ya mitindo na ubunifu maana hiki ni kitu kipya, ni kawaida walemavu kupanda jukwaani kwa ajili ya maonyesho lakini sio wenyewe kuwa wabunifu"Asmah Makau muandaaji wa maonyesho ya stara Tanzania .

Tamasha la tano la mavazi ya stara lilichukua sura mpya kwa kuwa na mavazi yenye mfanano wa wanyama pori

Haki miliki ya picha Mariam Semfuko
Image caption Vazi la stara lenye muonekano wa nyoka
Haki miliki ya picha Mariam Semfuko
Haki miliki ya picha Stara Tanzania
Image caption Mavazi ya stara kwa ajili ya mwezi wa ramadhani
Haki miliki ya picha Mariam Semfuko

Wabuni wengine wakongwe na mahiri katika ubunifu wa mavazi wanaona utofauti huu wa uwakilishi wa mavazi na ubunifu ni fursa kwa wengine.

Fundi Nyangalio ni nani?

Image caption Fundi asiyeona ,Nyangalio

Ni kawaida kuwapata mafundi wa nguo wakitumia utepe wa kupimia kuwapima wateja wao kabla ya kuwashonea nguo.

Lakini ukikutana na Abdallah Nyangalio, fundi hodari nchini Tanzania, mara nyingi hutampata akitumia utepe.

Kwa kukugusa tu, atakuwa tayari amejua vipimo vya nguo inayokufaa, ingawa hali ikizidi hutumia utepe maalum alioukarabati ndipo kupata vipimo kwa ufasaha.

Alianza kufanya hivi baada yake kupoteza uwezo wa kuona 1989, katika hali ya kusikitisha.

Alipatwa na maumivu makali ya kichwa 1988 na akawa anatafuta tiba bila mafanikio.

Mwaka 1989, alikutana na daktari kutoka Urusi aliyeahidi kumtibu na akamfanyia upasuaji.

Lakini badala ya kumpona, alipofuka kabisa na mke wake alimtoroka.

Fundi huyo wa miaka 53 ameibuka maarufu baada ya kumemshonea shati aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Licha ya hili, bado anaikosoa serikali kwa kutotambua vipaji vya walemavu, anaosema wengi wao huishia kuwa ombaomba barabarani.

Kitu pekee anachohitaji kusaidiwa ni katika kuchagua rangi, lakini kazi hiyo nyingine atajifanyia mwenyewe.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii