"Waganda hawana uhuru kuingia Afrika kusini"

Bunge la Uganda Haki miliki ya picha CHARLOTTE COSSET
Image caption Bunge la Uganda

Wadau katika sekta ya utalii nchini Uganda, hii leo wamepanga kuwasilisha malalamiko kwa spika wa bunge wakipinga changamoto za kupata vibali vya kusafiria (VISA) kwenda Afrika Kusini.

Wadau hao wanasema kwamba licha ya kufanikiwa kushiriki na kupata tuzo katika maonyesho ya utalii ya Indaba yaliyofanyika mjini Durban lakini walikabiliwa na wakati mgumu kupata vibali na wengi wao hawakuweza kushiriki kutokana na masharti na ada za juu za VISA za Afrika Kusini ambazo kwa muda mrefu zimekosolewa na raia mbalimbali wa Uganda.

Ilikuwa ni furaha tele mwishoni mwa wiki kwa washiriki kutoka Uganda katika maonyesho ya kitalii mjini Durban Afrika Kusini kupewa tuzo ya dhahabu baada ya kuibuka kuwa washiriki bora zaidi kuliko wengine.

Hata hivyo tuzo hiyo ilitokana na jitihada zao kubwa zilizoanzia kwenye mchakato wa changamoto kubwa ya kupata VISA kwenda Afrika Kusini.

Awali idadi kubwa ya washiriki ilinyimwa vibali hivyo na waliingiwa na wasiwasi kwamba wangekosa kushiriki hata baada ya kulipia ada zingine husika ikiwemo tiketi za ndege.

Amos Wekesa ambaye ni mmilikiwa wa kampuni ya Great Lakes Safaris ni mdau maafuru katika sekta ya utalii nchini Uganda anasema hakuna usawa kati ya nchi hizo mbili,

"Kupata VISA kwenda Afrika kusini imekuwa ngumu sana kupata wakati wao wanaingia Uganda wanavyotaka na kufanya kazi wanavyotaka, lakini watu wa Uganda hawapo huru kuingia Afrika Kusini" Wekesa aeleza.

Tabia ya mamlaka ya Afrika Kusini kuwanyima VISA raia wa Uganda pamoja na kupandisha ada hiyo kwa asilimia 150 kutoka dola 60 za kimarekani hadi $150 ni miongoni mwa mambo ambayo waganda wamelalamikia kwa muda mrefu.

Wadau hao wamesisitiza kuwa Afrika Kusini inanufaika sana kutokana na biashara kati yake na Uganda kupitia makampuni yanayodhibiti sekta muhimu kama vile benki, mawasiliano, nishati, vinywaji, magari, bima na maduka makubwa ya bishara yaani super Market.

"kitu ambacho wanakifanya ni sawa na kile ambacho Rwanda walichokifanya hivi karibuni, Umoja wa Afrika haupo.

Hii ni sawa na kutuambia tufunge makampuni yao pia ambayo yako hapa", mkazi wa Uganda Jakson Onyango.

"Afrika kusini haipo wazi maana hawajaweka wazi kipi ambacho tunakikosea maana ni kama wana hofu na sisi",Bella Masangano akitoa malalamiko yake.

Hivi leo Wekesa na wadau wengine katika sekta hiyo wanapanga kuwasilisha malalamiko yao kwa spika wa bunge la Uganda kuhusiana na masharti makali ya kupata VISA ya Afrika Kusini ilihali raia wa Afrika Kusini hupata VISA za Uganda mara tu wakiwasili uwanja wa ndege wa Uganda kwa ada ya dola 60 tu bila kutatizwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa

Aidha Ramaphosa amejibu malalamiko hayo yalliyoenea kwenye mitandao ya kijamii na kuhaidi kufanya makerebisho kwa sababu Afrika kusini imejithatiti katika malengo ya Umoja wa Afrika ya visa za bure kwa nchi za Afrika.

Na rais huyo aliongeza kuwa sasa wamejikita kuhamia katika mfumo mpya wa kimataifa wa VISA za kielektroniki.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii