Wataalamu waeleza athari za kula chakula katika sinia moja

ugali

Zama za mababu na bibi zetu barani Afrika lilikuwa si jambo geni kwa jamii kula chakula katika sahani moja , mfano ugali ukiisha iva, unabwagwa katika sinia moja, bakuli ya mboga ni moja na tena huwekwa katikati ya ugali huo na familia kulizunguka sinia hilo na kila mmoja kula kwa pamoja.

Mlo wa pamoja namna hiyo awali ulitafsiriwa kama njia ya kudumisha umoja, mshikamano na upendo lakini pia kama njia ya kumfundisha mtoto ama hata kumrekebisha mkubwa namna anavyo chota tonge, anavyotafuta ili asije akaiaibisha familia mbele za watu , ingawa kadri mabadiliko ya dunia tunamoishi utamaduni huu unadumishwa na wachache .

kama hiyo haitoshi,, ikumbukwe kwamba katika baadhi ya familia hasa katika maeneo ya vijijini bakuli ya kunawia mikono kabla ya kula ilikuwa ni moja tu, na kila mwanafamilia alisafisha mikono kwa maji hayo.

Pengine ndiyo kudumisha upendo, kinyaa kiliwekwa pembeni na kwa hakika Mungu aliwasaidia mno, kwani hakuna aliyewahi kulalamikia maumivu ya tumbo kutokana na kunawa maji machafu, ama hata kuendesha,{kuhara} ingawa vimelea vya magonjwa vilikuwepo pengine ni kutokuwa na elimu ya usafi na kujikinga na vimelea vya maradhi yatokanayo na uchafu.

Huwezi kusikiliza tena
Tamasha la chakula Zanzibar.

"Tunakaa duara moja mkekani na kula kwa pamoja na sijawahi kuendesha wala kuumwa tumbo hata siku moja mimi , sasa mambo yamegeuka, kila mmoja anawe mwenyewe tena ale kwenye sahani yake, na tena nawaona wakishachukua chakula kila mmoja anatafuta sehemu yake anakula peke yake.

Hali hii kwa hakika inapunguza ushirika na upendo miongoni mwa jamii haswa sisi waswahili huu usasa si utamaduni wetu" anatoa uzoefu wake bibi Kibena Magoso, ambaye ni hafidhina wa kudumisha mila na tamaduni za asili .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kuna utofauti mkubwa mtoto akila chakula na wenzake na pale anapokula mwenyewe

Faida nyingine ya kula kwa pamoja kwenye sinia mlilolizunguuka ni kumpa mtoto mazoezi ya kutumia akili yake kwa haraka, kwani wakati wa kula hapo zamani ukizubaa unaweza usishibe mlo huo kwani kila mmoja anakuwa na kasi yake ya ukataji matonge.

Hivyo inamlazimu mlaji kwa ujumla kujitahidi kutafuna kwa haraka na hii ilimsaidia mtoto au mtu mzima kutokuwa mzembe kwani ubongo wake ulikuwa ukifanya kazi kwa kasi namna ya kuchota tonge jingine mpaka atakaposhiba.

Image caption Desturi ya kila mmoja kula katika sahani yake

Wakati huu kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na binadamu kuingia katika mtindo mpya wa maisha , imelazimu desturi zenye kujenga umoja na mshikamano kuvunjwa na kuonekana hazifai.

Wataalamu wa afya sasa, wao ndiyo wamekata mzizi wa fitina, kwa kutoa maelekezo ya kujikinga na maradhi ya kuambukiza kutokana na vimelea vya magonjwa hayo.

Kutokana na usasa, mijini hali hii ya mambo leo imeshamiri na kila mmoja kushughulika kujali afya yake kila mmoja anakula kwa kutumia sahani yake na kwa wakati wake na sio kama zamani kula kwa ushirika na kwa wakati mmoja.

Mtaalamu wa sayansi ya chakula kutoka chuo cha Clemson huko South Carolina, amepima uwezekano wa bakteria kusambaa kwa watu kama wakichomvya katika bakuli moja kwa mara kadhaa.

Alifanya utafiti kwa kuwataka watu tisa kujitolea kula kwa ushirika katika sahani moja na kuchonvya mara sita katika bakuli moja.

Idadi ya vimelea vya maradhi ambavyo vilienea vilikuwa elfu kumi.

Aidha mtaalamu huyo amesema kuenea kwa vimelea vya maradhi hutegemea na usafi wa kila mmoja kati ya watu wanaokula chakula hicho kwa pamoja..

Kula kwa ushirika kunaweza kumuweka mtu hatarini kupata maambukizi ya maradhi kutoka kwa mtu mwingine.

Hivyo jambo la muhimu ni kuepuka kula huko kwa pamoja kwa kila mmoja kutumia sahani yake.

Utamaduni wa kula vyakula vikavu kama 'porpcon'

Utafiti uliofanywa chuo cha Clemson umebaini kuwa kuna uhusiano mmdogo wa vimelea kusambaa kutoka kwa mmtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Hata hivyo huwa inategemea na mtu na mtu na vimelea wanaweza kusambaa katika maeneo ya umma zaidi ya nyumbani.

Wataalamu hao wanasema, hatari ya maamukizi huwa inatokea kwa haraka kwa watu ambao mfumo wa kinga wao ni dhaifu kama wazee, watoto wadogo, wajawazito na wagonjwa.

Image caption Kuzima mshumaa katika keki kunaeneza vimelea vya magonjwa

Katika jaribio lingine ambalo mtafiti Profesa Paul Dawson ameliainisha ni wakati ambapo watu wanasheherekea siku ya kuzaliwa kwa kuzima mishumaa katika keki , vimelea huwa wanaenea wakati watu wanapozima mshumaa kwenye mapambo ya keki.

Hivyo ni muhimu kwa watu kuzingatia kila jambo unalolifanya kabla halijakuletea maradhi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii