Mitandao ya kijamii huwaathiri vijana walio katika umri wa kubarehe, wabaini utafiti

Msichana mwenye umri wa kubarehe akitumia mtandao wa habari wa kijamii Haki miliki ya picha Getty Images

Athari za matumizi ya mitandao ya kijamii kwa manufaa ya kuishi maisha yanayowaridhisha vijana ni chache na hasa kwa "walio katika kipindi cha kubarehe ", Utafiti uliowahusisha vijana wa uingereza walio katika umri wa kubarehe 12,000 unasema.

Familia, marafiki na maisha ya shule kwa pamoja huwa na athari bora katika kuboresha maisha, inasema timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Oxford.

Huwezi kusikiliza tena
Wanaowania nyadhfa za kisiasa kupimwa dawa za kulevya Uganda

Na watafiti hao wamezitaka kampuni kutangaza taarifa juu ya namna watu wanavyotumia nmitandao ya habari ya kijamii kuelewa zaidi juu ya athari za teknolojia katika maisha ya vijana walio katika umri wa kubarehe.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la PNAS ulililenga kujibu swali la ikiwa vijana walio katika umri wa kubarehe wanatumia mitandao ya kijamii zaidi ya wastani wanaishi maisha ya kuridhika kwa kiwango cha chini , au ikiwa vijana wenye umri huo ambao hawajaridhika kimaisha hutumia zaidi mitandao ya habari ya kijamii.

Tafiti za awali kuhusu uhusiano kati ya matumizi ya vifaa vya teknolojia ya mawasiliano, teknolojiaa yenyewe na afya ya akili ya watoto ambayo yamekuwa yakikinzana.

Haki miliki ya picha Getty Images

Athari zilizojitokeza

Profesa Andrew Przybylski na Amy Orben, kutoka taasisi ya Intaneti katika Chuo kikuu cha Oxford, anasema nara nyingi ushahidi unaotumiwa hautoshi na hivyo kuto picha ambayo haijakamilika.

Utafiti wao ulibaini kuwa mahusiano kati ya kuridhika kimaifa na mitandao ya kijamii "hayana thamani", faida yake ikiwa ni chini ya 1% katika kuboresha maisha ya vijana wenye umri wa kubarehe - na kwamba athari za mitandao ya kijamii ya habari "hutoa taarifa kwa njia tofauti".

Profesa Przybylski, ambaye ndio mkurugenzi wa utafiti huo katika taasisi hiyo alisema : "99.75% ya kiwango cha kuridhika maishani haihusiani matumizi yoyote ya mitandao ya kijamii ."

Huwezi kusikiliza tena
Habari za Global Newsbeat 1500 11/06/2018

Utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 2009 na 2017, uliwahisha vijana wenye umri kati ya miaka 10 na 15 wakiulizwa waeleze ni muda kiasi gani wanaoutumia katika mitandao ya habari ya kijamii katika siku ya kawaida ya shule na pia kuelezea kiwango cha jinsi muda huo ulivyowasaidia nyanja mbali mbali za maisha yao.

Walibaini kuwa muda wasichana walioutumia katika mitandao ya kijamii miongoni mwa wasichana uliwaathiri zaidi, lakini ilikuwa ni kidogo na hazikuwa za juu kuliko za kiwango cha wanaume.

Chini ya nusu ya athari hizi zilikuwa muhimu sana kwa takwimu, alisema.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Wazazi hawapaswi kuwa na wasi wasi juu ya muda wa matumizi ya mitandao ya kijami - kufikiria juu ya hilo kwa mtizamo huo ni kosa ," Profesa Przybylski anasema.

"Tumenatawaliwa na muda - lakini tunapaswa kuacha fikra hii ya muda wa matumizi ya skrini.

"Matokeo hayaonyeshi ushahidi wa wasiwasi mkubwa."

watafiri wamesema ni muhimu kwa sasa kuwatambua vijana wenye umri wa kubarehe walio katika hatari kubwa ya kupatwa na athari mbaya fulani za mitandao ya kijamii, na kubaini mambo mengine ambayo yanayoathiri ubora wa maisha yao.

Wanapanga kukutana na makampuni ya mitandao ya habari ya kijamii hivi karibuni kujadili namna wanavyoweza kushirikiana kujifunza zaidi namna watu wanavyotumia programu - na sio tu ni kwa muda gani wanazitumia.

'Hatua ncdogo ya kwanza '

Bi Orben, mtafiti mwenza na mwanasaikolojia mhadhiri katika Chuo kikuu cha Oxford, alisema kuwa makampuni lazima yatangaze data na ushahidi huru wa utafiti.

"Kupata taarifa ni muhimu katika kuelewa nafasi nyingi ambazo mitandao ya kijamii inachukua katika maisha ya vijana wadogo " alisema.

Dkt. Max Davie, afisa anayehusika na ubora wa afya katika chuo cha afya na tiba ya watoto wadogo - Royal College of Paediatrics and Child Health, aliunga mkono wito wa kuzitaka kampuni kushirikiana na wanasayansi na kuutaja utafiti huo kama "hatua ndogo ya kwanza".

Hata hivyo kuna mambo mengine ya kuchunguzwa zaidi, kama vile ni kiwango gani muda wa kutumia vifaa vya mawasiliano kama vile simu unachukua muda wa kufanya shughuli nyingjine muhimu kama kuala, kufanya mazoezi na muda wa kuwa na familia na marafiki

"Tunapendekeza familia zizingatie mwongozi wetu ikiwemo kuepuka matumizi ya vifaa kama komputa na simu saa moja kabla ya kulala ili kupata usingizi mzuri hasa kwa watoto."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii