Ramadhan: Mwili unafanyika nini wakati ukifunga swaum?

Image of a 3D scan of human anatomy Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waislamu hufunga mawio mpaka machweo wakati wa Ramadhani, lakini swaum inaathiri vipi mwili wako?

Kila mwaka mamilioni ya waislamu duniani hufunga tangu jua linapochomoza mpaka linapotuwa kwa siku 30 mfulilizo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika miaka ya hivi karibuni, Ramadhan hujiri katika miezi ya joto na katika maeneo ya kaskazini hilo mara nyingine humaanisha watu kufunga kwa saa nyingi na katika hali ya hewa yenye joto jingi.

Baadhi ya nchi kama Norway, waumini hufunga kwa hadi saa 20 kwa siku mwaka huu.

Basi hili lina manufaa yoyote? Haya ndiyo yanayofanyika mwilini mwako unapofunga kwa siku 30.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption During the fast, your body first uses blood sugar stored in the liver to provide energy

Mtihani mgumu - siku za kwanza za kufunga

Kimsingi mwili wako hauingii katika hali ya kufunga mpaka saa nane au zaidi baada ya kula chakula chako cha mwisho.

Huu ndio wakati utumbo unamaliza kusaga chakula na kunfyonza madini kutoka chakula ulichokila.

Muda mfupi baada ya hili, mwili wetu huanza kutafuta glucose iliopo kwenye maini na misuli kutafuta nguvu mwilini.

Muda unavyosogea, baada ya glucose iliopo mwilini kumalizika, miwli hugeukia mafuta kutafuta nguvu.

Haki miliki ya picha CHANDAN KHANNA

Mwili unapoanza kuchoma mafuta, hili husaidia kupunguza uzito wa mwili, hupunguza viwango vya cholesterol lna kupunguza hatari ya kuugua kisukari.

Hatahivyo kushuka kwa vinwango vya sukari mwilini inasababisha mwili kudhoofika na kukosa nguvu.

Huenda ukaanza kuumwana kichwa, ukasikia kisunzi, kichefuchefu na harufu mbaya kutoka mdomoni.

Hapa ndipo kiwango cha njaa kipo juu kabisa.

Jihadhari na mwili kupungua maji- Siku ya 3-7

Mwili unapoanza kuzoea kufunga, mafuta yanayayuka na kugeuka sukari mwilini.

Ni lazima ujirudishie maji mwilini kufidia masaa uliokuwa umefunga, la sivyo unapotokwa na jasho unaweza kupungua maji mwilini.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kunywa maji ni muhimu wakati unapokuwa hafungi hususan kukiwa na hali ya hewa ya joto

Ni muhimu chakula chako kijukuisha 'lishe yenye kukupa nguvu' , kama vile vyakula vyenye uwanga na vya mafuta kidogo.

Ni muhimu kuwa na lishe bora, ikiwemo protini, chumvi na maji.

Mwili unaanza kuzoea - Siku ya 8-15

Katika awamu ya tatu, utaona hali inaimarika, kama vile hisia wakati mwili unaanza kuzoea kufunga.

Dkt Razeen Mahroof, mshauri katika hospitali ya Addenbrooke huko Cambridge, anasema kuna manufaa mengine.

"Katika maisha yetu ya kawaida huwa tunakula vyakula vyenye kalori nyingi tu,na hili huweza kuuzuia mwili kutekeleza majukumu mengine kama kujirudisha katika hali yake ya kawaida."

"Hili husawazishwa wakatimtu anapofunga, huruhusu mwili kuangazia kazi nyingine.

Kwa hivyo kufunga huenda kukaunufaisha mwili kwa kuuponya na pia kuzuia na kupambana na maambukizi."

Haki miliki ya picha MOHAMED EL-SHAHED

Kujitakasa mwili- siku ya 16 - 30

Katika nusu ya mwisho ya Ramadhan, mwili wako utakuwa umeshazoea kabisa kufunga.

Maini, figo na utumbo na ngozi yake zitakuwa zinajitakasa kufikia sasa.

"Kiafya, kufikia kiwango hichi viungo vyako ndani ya mwili vimerudi kufanya kazi kikamilifu , huenda kumbukumbu yako ikawa imeimarika na ukawa na nguvu zaidi," anasema Dkt Mahroof.

"Mwili wako hautafuti protini ya kuupa nguvu hili ni wakati uanapokuwa na 'njaa' na kutumia misuli kuupa nguvu. Hili hufanyika iwapo utafunga kwa muda mrefu mtawalia.

"Kwasbabau watu hufunga ramadhan tangu alfajiri mpaka jioni, kuna nafasi nzuri ya kurudisha nguvumwilini kutokana na vyakula na vinywaji. Hii huhifadhi misuli lakini pia husaidia katika kupunguza uzito mwilini."

Basi kufunga kuna manufaa kwa afya yako?

Dkt Mahroof anajibu ndio, lakini kwa sharti moja.

"Kufunga kuna manufaa kwa afya yetu kwasababu inatusaidia kulenga tunachokula na wakati tunapokila. Hatahivyo japo kufunga kwa kipindi cha mwezi mmoja ikawa ni sawa, sio vizuri kufunga mfululizo."

Haki miliki ya picha SEYLLOU

"Kufunga mfululizo sio vizuri katika kutafuta kupunguza uzito wa mwili kwasbabau hatimaye mwili utaacha kugeuza mafuta kuwa nguvu na badala yake utageukia misuli. Hili sio jambo zuri na ina maana mwili wako utaishia kudhoofika kwa njaa."

Anapendekeza kwamba kufunga kando na katika mweiz wa Ramadhani au kufunga kwa siku tano na kupmzika siku mbili ni vizuri kuliko kuamua kufunga kwa miezi kadhaa mfululizo.

"Ukifunga mwezi wa Ramadhan vizuri, itakuruhusu kuirudisha nguvu mwilini, jambo linalomaanisha kwamba huenda ukapunguza kilo mwilini bila ya kupoteza misuli yako.."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii