Iran yajiondoa kwenye mkataba wa nyuklia baada ya Marekani kujiondoa

nuklia Haki miliki ya picha AFP

Iran anasema itaongeza urutubishaji wa madini ya uranium baada ya siku 60, mwaka mmoja baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba huo wa kimataifa.

Rais Hassan Rouhani amesema baada ya siku 60 Tehran itaongeza zaidi urutubishaji wa madini ya uranium yanayotengeneza nyuklia ambayo yamezuiwa na mkataba huo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Awali iliafikiwa kuwa madini ya uranium ya Iran yatapunguzwa kwa 98% hadi kilo 300 baada ya miaka 15

Mkataba huo unalenga kukabiliana na utengenezaji wa nyuklia ili iweze kuondolewa vikwazo vya misaada , lakini uhasama umeongezeka tangu Marekani ijiondoe.

Uchumi wa Iran umeyumbishwa na vikwazo vipya vya Marekani dhidi yake.

Ni kwanini mpango wa nuklia umeingia kwenye mzozo?

Mkataba wa nyuklia uliokubaliwa na Iran na mataifa mengine matano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa -Marekani , Uingereza , Ufaransa , Uchina na Urusi - pamoja na Ujerumani - uliingia dosari pale rais wa Marekani Trump alipotangaza kujiondoa mwaka mmoja uliopita.

Tangu wakati huo thamani ya fedha ya Iran iliporomoka kwa kiwango ambacho hakikuwahi kushuhudiwa, viwango vya mfumuko wa kiuchumi vya mwaka vilikuwa vikubwa na wawekezaji wa kigeni wakaihama nchi.

Image caption Mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa silaha za nyuklia uliingia dosari pale rais wa Marekani Trump alipotangaza kujiondoa mwaka mmoja uliopita

Nchi zinazounga mkono mkataba huo kutoka Ulaya, ambazo zilipinga vikwazo vipya dhidi ya Iran zimekuwa zikijaribu kutafuta njia za kuuendeleza. Hii ni pamoja na kuanzisha mfumo maalumu wa malipo ya kusaidia makampuni ya kimataifa yanayotaka kuendelea kufanya biashara na Iran kwa kukiuka vikwazo.

Lakini pia nchi hizo ziliionya Iran kwamba inapaswa kuendelea kuheshimu vipengele vyote vya mkataba, hususan kipengele kinachohusiana na shughuli za nuklia.

Hata hivyo, chini ya mkataba unaopfahamika kama Mpango wa pamoja wa utekelezaji (JCPOA) - Iran ilisema kuwa itachukulia kuanzishwa upya kwa vikwazo "kama sababu ya kuacha utekelezaji wa mkataba ... wote au sehemu yake ''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Donald Trump alionyesha msimamo wake dhidi ya mpango wa nuklia wa Iran hata kabla ya kuingia madarakani

Kwanini kuna uhasama baina ya Marekani na Iran?

Hali ya uhasama kati ya Marekani na Iran ilianza zamani wakati wa mapinduzi ya Iran mnamo mwaka 1979, ambapo kiongozi aliyependelewa na nchi za magharibi Shah na kuanzishwa kwa utawala uliochukia Marekani kuchukua mamlaka.

Rais Trump amechukua msimamo mkali dhidi ya Iran tangu alipoingia madarakani mwaka 2016.

Utawala wake unataka kuanzisha upya mazungumzo ya mkataba wa nyuklia na kupanua mapendekezo yake zaidi ili pia ikabiliane na mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran ya na "kudhibiti " shughuli za kijeshi katika eneo zima la Mashariki ya Kati.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii