Mathew Talbot: Mwanjeshi wa Uingereza auawa na tembo Malawi

Mathew Talbot Haki miliki ya picha MOD

Mwanjeshi wa Uingereza ameuawa na tembo wakati wa oparesheni ya kupinga uwindaji haramu nchini Malawi.

Mathew Talbot, 22, alikuwa akishika doria katika mbuga ya kitaifa ya Liwonde wakati aliposhambuliwa na mnyama hao.

Mkuu wake Luteni kanali Ed Launders, alimtaja Guardsman Talbot "alikuwa mtu muadilifu''.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Penny Mordaunt amesema alifanya kazi yake kwa "ujasiri mkubwa na utaalamu wa hali yajuu".

Aliongezea kuwa: "Kisa hicho kinawakumbusha hatari inayowakabili wanajeshi wao wanapokuwa katika harakati ya kuwalinda wanyama walio katika hatari ya kuangamia duniani mikononi mwa watu wanotaka kujinufaishakutokana nao."

Kensington Palace imesema mtawala wa Cambridge ameitumia risala za rambi rambi familia ya Gdsm Talbot.

Haki miliki ya picha MOD
Image caption Mathew Talbot

Gdsm Talbot,ambaye alikua mkaazi wa West Midlands, alikua akihudumu nchini Malawi baada ya kutumwa huko na wizara ya ulinzi.

Gdsm Talbot alifariki kutokana na majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa na tembo.

Hakuna mtu mwingine yeyote aliyejeruhiwa na mnyama huyo.

Amewaacha wazazi wake Bw. na Bi Steven, dadazake Aimee na Isabel, mpenzi wake Olivia.

Katika taarifa ,wizara ya iulinzi imesema Gdsm Talbot "hakuwa na ufahamu" wa Afrika na alijitolea katika mpango wa kukabiliana na uwindaji haramu nchini Malawi.

Haki miliki ya picha MOD

Oparesheni ya Corded, jina lililopewa wanajeshi waliyopelekwa Malawi, kuwasaidia maafisa wa wanyamapori kukabiliana na biashara ya uwindaji haramu.

Waziri wa zamani wa ulinzi, Gavin Williamson, alitangaza upanuzi wa mafunzo ya kukabiliana na uwindaji haramu katika mbunga mbili zaidi nchini Malawi - hatua ambayo iliongeza idadi ya maafisa waliopata mafunzo hayo kufikia 120 - mwaka 2018.

Uchambuzi wa Alastair Leithead, BBC

Uwindaji haramu wa tembo ni changamoto kubwa kote barani Afrika - inakadiriwa kuwa tembo 30,000 wanauawa kila mwaka - na huenda wanyama hao sasa wamesalia ni 450,000 pekee.

Katika maeneo mengi imegeuka kuwa mapigano dhidi ya wawindaji haramu.

Lakini kumekua na maoni tofauti kuhusiana na jinsi ya kukomesha biashara haramu ya pembe za ndovu.

Kampeini ya kimataifa inayungwa mkono na mataifa kama vile Kenya - inataka biashara ya pembe kutokomezwa kabisa ili kuwadhibiti wahalifu wanaotumia vibaya leseni ya kufanya biashara hiyo.

Baadhi ya mataifa ya Kusini mwa Afrika ambayo yana idadi kubwa ya tembo yanaamini, biashara halali itakayodhibitiwa inaweza kuzisaidia na fedha za kuwahifadhi wanyama hao.

Botswana, ambayo imekuwa iliandaa kongamano kuhusu uhifadhi wa tembo siku chache zilizopita huenda tembo 130,000 - dadi ambayo inasemekana kuwa kubwa zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani inakabiliwa na mzozo mkubwa wa tembo mna binadamu

Zawadi isiyokuwa ya kawaida ya viti vilichotengenezwa kutokana na kwato za tembo vilivyopewa viongozi waliohuduria mkutano wa Botswana ni ishara ya kuunga mkono biashara hiyo.

Chini ya utawala wa rais mpya, huenda kuhalalisha uwindaji ambao ni maarufu sana katika maoneo ya vijinjini ndio mbinu ya kutafuta kura katika mwaka wa uchaguzi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii